Hivi lengo la Hamas lilikuwa ni nini ile Oktoba 7, 2023?

Hivi lengo la Hamas lilikuwa ni nini ile Oktoba 7, 2023?

Umemjibu vyema.

Watu wengi wasichokijua ni kuwa wengi wa tunaowaita wapalestina leo wana damu ya kiyahudi, ila tu waliamua kuukubali uislamu na baadhi yao kuukubali ukiristo.

Hawa walowezi kutoka ulaya wanadhani wana haki zaidi.


Was Palestine a country before Israel?


From a purely historical perspective, “Israel” predates “Palestine” by more than a millennium. But, with the Jewish people then dispersed from their homeland, “Palestine” became home to a substantial Arab population, again for more than a millennium.
 
Israel miaka nenda miaka rudi walikuwa wanawanyanyasa wapalestine kuwauwa kuwapiga na kuwanyanyasa ndani ya ardhi yao, maeneo yao muhimu ya kiibada hawana uhuru nayo kufanya Ibada yoyote mara wanazuiwa na kufanyiwa unyanyasaji lakini yote ardhi yao kila uchao walikuwa wanaimega, maeneo kadhaa kama West bank, hapo Gaza nk. walishasiginwa hadi ukutani hivyo subira ilifikia mwisho wake ndio hichi kinachoendelea kutokea muda huu
Okay, but, are Gazans better off today than they were before 10/07/2023?
 
Vitoto vya 2000 vinajadili vita ya Palestina na Israel, vinaona vita vimeanza Oct 7.

Havijui Wapestina wameanza kuuliwa na Israel toka mwaka 1948 baada Israel kuchukuwa ardhi ya Wapalestina.
 
Vitoto vya 2000 vinajadili vita ya Palestina na Israel, vinaona vita vimeanza Oct 7.

Havijui Wapestina wameanza kuuliwa na Israel toka mwaka 1948 baada Israel kuchukuwa ardhi ya Wapalestina.
Hakuna unachokijua. Hiyo siyo ardhi ya wapalestina oekee, bali Wayahudi na wapalestina.

Hakuna wakati hata mmoja ambapo ardhi hiyo ilikosa Wayahudi

Kiasili ardhi hiyo ni ya aayahudi kakini demograohy ilibadilika kutikanana Wayahudi kutawanyika.

Was Palestine a country before Israel?


From a purely historical perspective, “Israel” predates “Palestine” by more than a millennium. But, with the Jewish people then dispersed from their homeland, “Palestine” became home to a substantial Arab population, again for more than a millennium.
 
Dah nikikumbuka iyo October 7 walivyokuwa wakibweka Allah akbar Allah akabar na kukata mauno hadharani. Basi huyo Allah angewasaidia sasa anawaogopa wayahudi ambao amewaumba?
Nimegundua wewe Mgerasi una ugomvi binafsi na Waquraish weusi!

Au nasema uongo adriz?
😁😁
 
Hammas ni wapumbavu.
Nafikiri walivuta Bangi.
Hata kama mnapigania HAKI yenu huwezi pigania HAKI alafu ukaacha AKILI pembeni.
Ndicho walichofanya Hammas. Kupigania HAKI yao bila Akili
Bangi iheshimiwe mkuu.
Sisi wavuta bangi hatuna maamuzi ya kingese kama hao wanywa gongo
 
Na hasa ndio approach iliiotakiwa.. mbona Jordan wanashare mipaka na israel hakuna migogoro.. tatizo palestina upande wa gaza wamekubali kutawaliwa na watu radicals ambao wanaamini katika dawa ya moto ni moto..

hamas wanataka israel ifutike kabisa kitu ambacho haiwezekani. Matokeo yake kwa kadiri wanavyojaribu ndio wanaIdi kupoteza.. na tatizo wanatumika na waraabu wenzao .. kungekuwa na nia ya dhati ya waarabu kuwapa utaifa palestina ingeshatokea zamani sana

We fikiria sudan tu hapo walipoanza kuchapana kwa misingi ya dini .. mara likatolewa wazo.. dunia ikalisimamia sudani ikagawanywa.. kwa nini ishindikane kwa palestina kuwa na utaifa
Jibu ni kuwa Israel hakubali kwa sababu anajua nia ya Hamas wao wanataka kufuta taifa la israel same to Iran. Maana yake ikiwa palestina itakuwa taifa.. italindwa na soverignity laws.. inaweza hata ikamruhusu iran akaweka silaha kali pale waka cordinate na Lebanon .. waka attack israel na kuifuta maana hilo
Ndio lengo mama .. hata vitabu vyao vya dini vinataka iwe hivyo.. na kijiografia Israel ni ndogo sana..

Ndio maana netanyau alisema palestina kuwa na utaifa its a death sentence kwa Israel

sasa hivi dunia imebadilika.. ili kumuwin Israel wangeleta approach ambayo israel wangeona kuwa hawa jamaa sio Threat kisha wakaja na proposal ambayo wangewekeana mipaka basi Palestina ikawa nchi kamili
Wakaanza kupata wawekezaji na misaada.

Hapo Hata Israel wangeona aibu.. na dunia nzima ingekuwa upande wa Palestina kama ingetokea Israel kafanya ndivyo Sivyo.. lakini toka enzi na enzi approach ya wa palestina imekuwa ni jino kwa jino..

Arafat alijaribu kutafuta suluhu ya mezani hadi wakaingia mkataba na israel.. ila hamas wakagoma
Ndio chanzo cha Mgawanyiko na alipokufa gaza ikabaki kwa Hamas. Kule west babk wakabaki Fatah chama ambacho kinaongozwa na Abbas..
Unawalaumu wapalestina peke yao na unawatoa katika hatia mazayuni. Mazayuni ni tatizo kubwa. Unasema kuwa vitabu vya dini vya wapalestina vinataka dola ya kizayuni iliyoanzishwa mwaka 1948 na wazungu ambao wengi waliikimbia Ulaya kuwakimbia "ndugu" zao waliokuwa wakiwatesa, ifutwe, ila husemi kuwa mazayuni wanatumia vitabu ambavyo wengi wao hata hawaviamini kuhalalisha kuunda taifa Lao pale na kufanya mauaji ya kimbari pale! Au unafikiri reference ya "kuangamiza mbegu za amalekites" wanazitoa Geneva Conventions?

Hamas na Iran (dola ya kishia) ni tatizo pia, na ndio wanaowaponza wapalestina zaidi na kuharibu fursa za amani zinapojitokeza. Ila fursa hizo za amani zinapopotea hata mazayuni wanafurahi pia. Kwa sababu agenda zao zinasonga. Akina Netanyahu walipinga Oslo Accords na wakati ule waliona uwepo wa Hamas ni fursa ya kuwadondosha akina PLO. Waliona Hamas inaweza kutumika kama "tool" yao. Na ndio maana kila hata Oct 7 , attack imefanywa na Hamas lakini mazayuni wanashambulia mpaka West Bank iliyo chini ya Fatah.

Mazayuni ni watu wa khiana, hilo linajulikana, ila fursa za kupata amani zinapopatikana wapalestina japo wana haki lakini wafanye tu amani na mazayuni na nchi za kiislam zifanye tu amani na mazayuni. Na waheshimu hiyo mikataba ya amani kwa dhati kabisa (wakijua moyoni kuwa mazayuni ni watu wa khiana). Na warudi katika Dini yao kwa sawa. Mazayuni wakifanya khiana, baada ya hiyo amani, basi wapalestina watasaidiwa tu na Mola Mlezi wa viumbe vyote.

Mtume alifanya amani na mayahudi wa Madinah na akaheshimu mikataba, ni mayahudi ndio walivunja mikataba hiyo, na wakapata sehemu ya yale yaliyofanywa na mikono yao.

Mtume alifanya mkataba wa amani na washirikina wa Kiquraish na akauheshimu, na terms za ule mkataba zilikuwa zinaonekana harsh kwa Waislam, ila aliuheshimu mkataba kwa uaminifu. Ni.maquraish ndio waliuvunja mkataba huo, na yakawapata yaliyowapata.
 
Weka hapa huo ushahid
Ushahidi kutoka kwa Vyombo vya habari vya Israel

1. Haaretz

2. Times of Israel (wameelezea report ya Haaretz na zaidi)

3. Chanel 12 tv ya Israel pia ilireport Hamas hawakuwa na Mpango wa Kuvamia Music Festival na Polisi wa Israel waliua Raia wao

4. Jerusalem post

Huo ni Ushahidi toka Israel kwenyewe.

Kuna ushahidi mwingine toka Ufaransa, Usa na waandishi wa habari wengine ila wote huo hauna nguvu kuliko Israel wenyewe.


Hii Picha inaonesha aftermath ya music festival
GQOjIgCXYAAYtEo.jpg

Hamas hawana silaha yoyote inayoweza kuleta impact kubwa kama hio, hio picha Pia haitendei haki Angalia hii video kuona impact

View: https://twitter.com/Megatron_ron/status/1723041286578462953

Kila mtu mwenye ABCD za vita anajua nani kaunguza hilo eneo kiasi kwamba Maiti ilibidi zikapimwe Dna kutambulika,
 
Hili swali niliuliza sana.. kwamba kama kigezo ni kuwa mnakandamizwa na kunyang'anywa ardhi yenu.. sasa kwa nini muanzishe shambulio ambalo ndo litazidi kuwaumiza zaid.. kama
Lengo ni ukomboz maana yake mnatakiwa mkajipange mkitoa
Kipigo adui awe hana uwezo wa kurudisha.. ila Inaonekana
kuwa Hamas walipewa na maelekezo na kaka mkubwa iran.. kwa kigezo kuwa israel ikijibu basi iran, na proxy wake hizbolah na houthi waishambulie..

Ndio maana u unaona baada ya shambulio iran akaanza kupiga mkwara
Mzito israel asivuke Mpaka kuingia Gaza.. ila Iran hakuwa na nia ya dhati kuwasaidia Hamas alikuwa anawatumia tu kisiasa .. Iran angekuwa kweli anajitoa walau nusu tu ya USA anavyojitoa kwa Israel hamas walau wangekuwa na pakushika.. fedha na uwekezaji ambao iran ametumia kwa zaid ya miaka 16 kuijenga hizbola angeutumia kwa hamas kama alikuwa na nia.. hizbola nae kakubali cease fire wakat alisema kigezo ni lazima Israel aondoke Gaza

It was a cordinated mission ingawa mafanikio yanaonekana ni less than 50% hamas kaachwa peke yake
Fredwash umeandika bila ushabiki uchambuzi mzuri sana
 
Mbona tumeichakaza Israel vya kutosha, Au huoni mkuu...

Nenda kaangalie Al-shabab Tv, utaona kinachojiri huko Israel .. 🥴🥴
Sasa kama mmeichakaza Israel, malalamiko kama Yale ya tamko la Arab league yanatoka wapi?

Gaza imekuwa vifusi huku unadai Israel inapigwa?
 
Labda walikuwa wakiichukulia poa Israel
It is assumed That, the October 7th was Inside job to get the excuse of exterminating Phalestines from Ghaza so that the elites of West and Israel can do exploration of oil and gas in that area then later have oil and gas wells to feed the starving Energy industry of the West!!!
 
Okay, but, are Gazans better off today than they were before 10/07/2023?
Hapana sio bora sasaivi na inawezekana maisha yakawa mabaya zaidi hapa lakini suali zuri ni je kwa mfano Nchi zingeendelea kutawaliwa duniani? Mapinduzi hayakuwa bora kupata uhuru wao? watu waliuliwa sana kwenye hayo mapinduzi lakini leo generation yao inafaidika na matunda ya na uhuru uliopatikana kwa shida na dhiki ya waliopigania nchi yao.
 
Lengo lao lilikuwa zuri tu kwa mustakabali wao, sema walimis-calculate reaction ya muisrael.
Hesabu ilikuwa kutumia mateka kama turufu ya kupush madai yao kwa Israel, walidhani Israel atakuja mezani kwa majadiliano. Badala yake Israel akaja kwa kipigo kikali.

Baba yao (Iran) naye akaingia na hesabu hizo hizo, naye akakumbana na revenge ya hatarii.

Sasa Trump ndo majuzi kawavuruga zaidi kutoa ile ultimatum ya mateka kuachiwa
 
Kwa nini Hamas walianzisha chokochoko ambayo msukosuko wake hawawezi kuustahimili?
We naye haujitambui, huko westbank kuna chokochoko mbona kila siku wanapigwa? Hiyo ni justification tu ya Netanyahu ku annex Gaza na kuwapa makazi settlers. Otherwise Hamas walivamia sababu ya kutuma ujumbe kuwa wamechoka kukandamizwa na nadhani imepata attention waliyotaka kwahiyo its a win kwenye hiyo angle.

Ni sawa na useme Mkwawa alikua mjinga kisa kuleta chokochoko kwa wajerumani. Kila rebellion lazima iwe na mwanzo hata kama itakua crushed ila ina-set basis ya future redemption. Kwahiyo hakuna hasara hata Kurds pia wanapigwa!! Lakini sio sababu ya kuwakatisha tamaa kuwa ipo siku patakucha
 
Hammas ni wapumbavu.
Nafikiri walivuta Bangi.
Hata kama mnapigania HAKI yenu huwezi pigania HAKI alafu ukaacha AKILI pembeni.
Ndicho walichofanya Hammas. Kupigania HAKI yao bila Akili
Mbona Mandela alifanya hivi hivi, alikua wanatega mabomu na kuteka makaburPu ila mnamuita Baba wa Afrika na sio Gaidi?
 
Back
Top Bottom