Hivi lini hii dunia wajinga wataisha? Hivi msomi nae anaweza kuwa na vivyo hivyo ukawa mjinga! Dada Betty ujinga umekufanya upoteze maisha

MAREHEMU BETTY AJENTA CHARLES:

Hadithi ya Betty Ajenta Charles (pichani), inasikitisha. Mwili wake umefukuliwa baada ya kufunga mpaka kufa katika sakata linaloendelea nchini Kenya la Mchungaji Paul Mackenzie ambaye anawafungisha Wakenya hadi umauti ("Fasting to Death") ili wafike Mbinguni kirahisi.

Mwili wake ni kati ya miili 73 iliyofukuliwa katika zoezi la kiuchunguzi linaloendelea kwenye jimbo la Kilifi - Kanisa la Shakahola. Marafiki na ndugu za Betty wamepata mshtuko mkubwa sana.

Betty alikuwa mfanyakazi wa Shirika moja kuubwa la ndege duniani, ambaye aliamua kuacha kazi yake, akauza ardhi yake kwa Kshs 7,000,000 = Tzs 121,170,000 na kumkabidhi "Mchungaji Wakala wa Shetani" Paul Mackenzie wa Malindi - Kenya.

Betty alirejea Kenya kutoka ughaibuni baada ya mtoto wake aitwaye Jason kulazimishwa kufunga hali iliyopelekea mtoto huyo aage dunia. Wakati mtoto huyo wa Betty anafunga kula hadi kufariki, Betty alikuwa nchini Qatar. Mtoto wa Betty, Jason, alikuwa akiishi na babu na bibi yake wakati huo. Haijulikani ni nani alimfungisha mtoto huyo hadi kufa.

Baada ya kupokea taarifa za kifo cha mwanaye, inaelezwa Betty alifunga safari kutoka Qatar hadi Kenya kwa ajili ya mazishi ya mwanaye lakini akapotea na hakujulikana alipo tena.

Dada ya Betty anayeishi eneo la Umoja - Nairobi, anasema Betty aliacha barua ya hisia kali kwa Mume wake akionesha asingelirejea tena milele. Baada ya kuandika barua hiyo Betty aliondoka na wanaye kuelekea Malindi.

Inaonekana alifuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii, akauza vitu vyake vyote kabla ya kupanda Ndege kuelekea Malindi - Kenya.

Rafiki ya Betty anasema, Betty alimuaga akimjulisha kuwa anaenda kuonana ana kwa ana na Yesu siku ya tarehe 08 Aprili 2023 na kwamba alilazimika kuondoka tarehe 07 Aprili 2023. Rafiki ya Betty alipoifuatilia tiketi yake ya ndege akagundua ni tiketi ya moja kwa moja na siyo ya nenda rudi.

Katika msako unaoendelea katika eneo la ekari 800 linalomilikiwa na "Mchungaji Feki" Paul Mackenzie, polisi wamemkamata Mchungaji mwenza anayejulikana kama "Zablon wa Yesu". akiwa anasoma Biblia akieleza yeye angelianza kufunga Juni 2023!
Screenshot_20230425_222118.jpg
 
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Neno la Mungu limebainisha hayo. Tatizo watu wanapokea mafundisho potofu, hawajui kupambambanua wahubiri feki. Wakiambiwa Yesu yuko kule wanaamini hivyo. Yesu mwenye alionya kuhusu kutokea kwa manabii wa uongo watakaotumia jina lake kudanganya wengi. Watu wamekosa mafundisho sahihi, wanafundishwa uongo huku maandiko hawajui, hatari tupu
 
MAREHEMU BETTY AJENTA CHARLES:

Hadithi ya Betty Ajenta Charles (pichani), inasikitisha. Mwili wake umefukuliwa baada ya kufunga mpaka kufa katika sakata linaloendelea nchini Kenya la Mchungaji Paul Mackenzie ambaye anawafungisha Wakenya hadi umauti ("Fasting to Death") ili wafike Mbinguni kirahisi.

Mwili wake ni kati ya miili 73 iliyofukuliwa katika zoezi la kiuchunguzi linaloendelea kwenye jimbo la Kilifi - Kanisa la Shakahola. Marafiki na ndugu za Betty wamepata mshtuko mkubwa sana.

Betty alikuwa mfanyakazi wa Shirika moja kuubwa la ndege duniani, ambaye aliamua kuacha kazi yake, akauza ardhi yake kwa Kshs 7,000,000 = Tzs 121,170,000 na kumkabidhi "Mchungaji Wakala wa Shetani" Paul Mackenzie wa Malindi - Kenya.

Betty alirejea Kenya kutoka ughaibuni baada ya mtoto wake aitwaye Jason kulazimishwa kufunga hali iliyopelekea mtoto huyo aage dunia. Wakati mtoto huyo wa Betty anafunga kula hadi kufariki, Betty alikuwa nchini Qatar. Mtoto wa Betty, Jason, alikuwa akiishi na babu na bibi yake wakati huo. Haijulikani ni nani alimfungisha mtoto huyo hadi kufa.

Baada ya kupokea taarifa za kifo cha mwanaye, inaelezwa Betty alifunga safari kutoka Qatar hadi Kenya kwa ajili ya mazishi ya mwanaye lakini akapotea na hakujulikana alipo tena.

Dada ya Betty anayeishi eneo la Umoja - Nairobi, anasema Betty aliacha barua ya hisia kali kwa Mume wake akionesha asingelirejea tena milele. Baada ya kuandika barua hiyo Betty aliondoka na wanaye kuelekea Malindi.

Inaonekana alifuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii, akauza vitu vyake vyote kabla ya kupanda Ndege kuelekea Malindi - Kenya.

Rafiki ya Betty anasema, Betty alimuaga akimjulisha kuwa anaenda kuonana ana kwa ana na Yesu siku ya tarehe 08 Aprili 2023 na kwamba alilazimika kuondoka tarehe 07 Aprili 2023. Rafiki ya Betty alipoifuatilia tiketi yake ya ndege akagundua ni tiketi ya moja kwa moja na siyo ya nenda rudi.

Katika msako unaoendelea katika eneo la ekari 800 linalomilikiwa na "Mchungaji Feki" Paul Mackenzie, polisi wamemkamata Mchungaji mwenza anayejulikana kama "Zablon wa Yesu". akiwa anasoma Biblia akieleza yeye angelianza kufunga Juni 2023!
😳🤔🙌Jmn Kuna mambo duniani
Sa huyo si wapige risasi tu wanasubiri nn?
Na Mali zitaifishwe
 
Pengine huyo mchungaji alikuwa akitumia na madawa/ majini. Mtu unafungaje kavu siku zote hizo? Akili inakuwa wapi muda huo? Udini wa mchongo huo ni hatari sana
Pengine watu walikuwa wakishikiliwa mateka huko maana wengi wamekuwa excommunicated na jamii walikotoka
 
Huyo mchungaji achunguzwe atakuwa anachukua hela zao waumin na kuwaua,haiingii akilin mtu auze kila kitu akampe mchungaji then afunge kula ili afe akamwone Yesu [emoji120]there is more to that story
Labda biashara ya viungo vya binadamu live live huko
 
Unasemaje wewe?
Hao uliowataja wameamua nani? Au wapi uliona wametapeli Watu km huko Kenya?
Au wapi uliona wamewaamrisha Watu kufunga?
Au ndo umejisikia TU kuchafua majina ya Watu?
We mpuuzi kweli, na usipotubu , utashangaa sn!
Hukumbuki tukio la mmoja wao kuigiza akifufua mfu? Au na wewe ni blind follower.
 
Pengine huyo mchungaji alikuwa akitumia na madawa/ majini. Mtu unafungaje kavu siku zote hizo? Akili inakuwa wapi muda huo? Udini wa mchongo huo ni hatari sana
Hakuna cha madawa wala nini!!hivi unajua ukishakubali kuwa brainwashed??wewe?!upande ule mwingine ndio wale wazee wa itikadi kali mtu anajilipua live!!!
 
I sense labda kuna biashara ya viungo vya binadamu huko
Sidhani kwa mazingira yale, na pia kama ungekuwepo huo uhuni basi maiti pia kwa namna moja au nyingine zingeonyesha.

Huyo mchungaji na wasaidizi wake ni wauwaji na waporaji wa mali za watu kwa kigezo cha dini.
 
Pengine huyo mchungaji alikuwa akitumia na madawa/ majini. Mtu unafungaje kavu siku zote hizo? Akili inakuwa wapi muda huo? Udini wa mchongo huo ni hatari sana
Inawezekana pia kuna ka ushirikina hapo, maana ukiangalia scenario ya huyo dada alivyo chotwa ni fikirishi sana.

Yani badala ya kumshitaki mchungaji kwa kumfungisha mtoto mdogo mpaka kufa matokeo yake na yeye akaenda kufungishwa hadi kufa.
 
Back
Top Bottom