Yaani mtu kajiuzuru mwenyewe kutokana na Ufisadi wake ambao Umeigharimu nchi pakubwa (hasa kwa kuitia hasara) halafu leo kafariki tunasema/tunamuita ni Waziri Mkuu Mstaafu!
Lowassa alistaafu Uwaziri Mkuu wake kama wengine au alijiuzuru kutokana na Kashfa zake za Ufisadi alizojaribu kuzizima kwa Utajiri wake mkubwa na wa kutukuka?
GENTAMYCINE hiki kikombe cha Unafiki na Upuuzi (Ujuha) kilichopo kwa Watanzania wengi (hasa kwa huu msiba) wala sitokinywa kabisa kutokana na Dhambi zake kubwa za Ufisadi na Utajiri wake wa Mashaka ambao Ulimshtua na hata Kumuumiza Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Kwa Mataifa mengine (hasa yenye Watu na Viongozi Werevu) kama ya Rwanda, Ghana, Namibia na Botswana huenda tokea mwaka 2010 hadi juzi Anafariki Lowassa angekuwa yuko jela kutokana na kashfa zake za Ufisadi ambazo zilitetewa mno na Mafisadi wenzake ambao walikuwa katika Utawala na katika System ya nchi.
Tanzania ndiyo Taifa pekee duniani ambako Fisadi na Mafia husifiwa na hutukuzwa kwa kila namna na Kundi kubwa Raia ambao ni Majuha (Walemavu wa Akili na kutokujua Kufikiri) tofauti na Mataifa mengine yenye Viongozi makini na Raia Werevu kama la Rwanda, Ghana, Namibia na Botswana.
Kikatiba ya JMT, mtu huhesabika "Mstaafu" katika wadhifa au kazi aliyokuwa nayo mara tu anapokoma kua na wadhifa au kazi hio, haijalishi madaraka hayo yamemtokaje.
Mfano Hayati Dr J P Magufuli ni Rais Mstaafu, ambae madaraka yake yalimuondoka baada ya kufa.
"Alikubali kupoteza kunusuru serekali, kubalance serekali, kujitwisha mzigo mzito wa watu wengine, hakuwa mjinga, hakuwa fisadi, alifanya hivyo kwa sababu kwa wakati huo, tatizo lilikuwa ni Uwaziri mkuu"
Mbona mchizi aliweka wazi kabisa mwenye ushahidi ampeleke mahakamani vinginevyo mpige kimya. Tena aliongea kipindi yupo upinzani. Mkafyata team buku 7 wote.