Hivi Lowassa ni Waziri Mkuu Mstaafu au ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu?
"Alikubali kupoteza kunusuru serekali, kubalance serekali,kujitwisha mzigo mzito wa watu wengine, hakuwa mjinga, hakuwa fisadi, alifanya hivyo kwa sababu kwa wakati huo, tatizo lilikuwa ni Uwaziri mkuu"
na huu pia ni ujinga mwingine , ushawai ona wap mmasai anashiriki uongo?
 
Mbona mchizi aliweka wazi kabisa mwenye ushahidi ampeleke mahakamani vinginevyo mpige kimya. Tena aliongea kipindi yupo upinzani. Mkafyata team buku 7 wote.
unahisi upinzan alienda kwa kupenda ? wajinga nchi hii wakiisha ndo tutaanza songa mbele , atoke ccmu hlf arudi ccmu , asipinge matokeo ya 2015 bado umwamini
 
Tanzania ina wajinga wengi kila kona kutafuta kick, wanajifanya wanamjua Lowasa kuliko hata anaokaa nao hapo CCM.

Mtu ana kashfa kibao wanakataa haijalishi ni ukweli au uongo ila yeye ndio alikuwa waziri mkuu, mbona kujengwa shule za kata mnadai ni yeye kwa vile alikuwa waziri mkuu ,mna uhakika gani kwamba yeye ndio kaanizisha shule za Kata?

lowasa na CCM ni damu damu hawana ugomvi maana alipokelewa kwa shangwe baad ya kuhama .
 
Waziri Mkuu pekee aliye achia ngazi huku akiwa bado anaushawishi mkubwa na kupendwa na watanzania wengi zaidi.

Lowasa kwa watanzania ni shujaaa mwenyw akili kubwa ya kuleta maendeleo kwa watanzania.

Ni waziri Mkuu pekee baada ya Sokoine.

Wale wote walio tengeneza fitina hadi akaachia ngazi hakika walikatisha matunda mazuri ambayo watanzania wangeyafaidi kupitia Lowasa.
 
Mawaziri wakuu wastaafu waliobaki ni kama wanne hivi,NAO WATAZIKWA kwa heshima hii hii ya presidetal ceremonial.(state cereminial).naona hata Warioba akawa haelewi elewi.
 
Ukweli huuma, hasa kwa wasiojielelewa, ifike hatua tuelewe kua lazima ote waliodumaza maendeleo ya nchi yetu pendwa waishe ili kije kizazi kingine chenye uwezo wa kuendana na speed ya dunia ya leo kije kiingoze taifa hili
Kizazi kipi, cha Makonda?
Unafiki na uongo huleta laana ya kudumu. Mzee Lowasa amesingiziwa saaana. Ilikuwa ni wivu tuu kwa vile Watanzania hatupendi elites [werevu].
Hadi leo tofauti na wengine hatujawahi kuambiwa Mzee Lowasa alifisadi fedha kiasi gani!!!!. Za Escrow, Meremeta nk tuliambiwa na wahusika ni kina nani.
 
Wivu umewajah Sana maskini

Mwamba wa kasikazini huyo

Hakunaga maboya Kanda hyo watu wanapesa vibaya mno iwe ufisadi halali ila juwa tu hakunaga boya Kanda hyo siyo kamaa ninyi huko musoma Mara ndio manaanza kuchimbiwa shimo matunddu ya vyoo Ni watu wajinga mno wkt serekali mmejazana

Kasikazini hakuna boya

Pole mzee wa chuki binafsi
 
Mleta mada huo.ujinga wenu wa visasi upeleke kule nchini kwako ulikotokea watazania huo upumbavu Huwa Hatuna mtu akifa tunamzika Kwa heshima zote
 
Kikatiba ya JMT, mtu huhesabika "Mstaafu" katika wadhifa au kazi aliyokuwa nayo mara tu anapokoma kua na wadhifa au kazi hio, haijalishi madaraka hayo yamemtokaje.

Mfano Hayati Dr J P Magufuli ni Rais Mstaafu, ambae madaraka yake yalimuondoka baada ya kufa.
"aliyekuwa"rais wa jmt.john pombe Magufuli.
 
Yaani mtu kajiuzuru mwenyewe kutokana na Ufisadi wake ambao Umeigharimu nchi pakubwa (hasa kwa kuitia hasara) halafu leo kafariki tunasema/tunamuita ni Waziri Mkuu Mstaafu!

Lowassa alistaafu Uwaziri Mkuu wake kama wengine au alijiuzuru kutokana na Kashfa zake za Ufisadi alizojaribu kuzizima kwa Utajiri wake mkubwa na wa kutukuka?

GENTAMYCINE hiki kikombe cha Unafiki na Upuuzi (Ujuha) kilichopo kwa Watanzania wengi (hasa kwa huu msiba) wala sitokinywa kabisa kutokana na Dhambi zake kubwa za Ufisadi na Utajiri wake wa Mashaka ambao Ulimshtua na hata Kumuumiza Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Tulikubaliana hii iwe awamu ya sita ili naye atawale miaka miwili kulingana na utaratibu wa chama.
 
Back
Top Bottom