Hivi Lowassa ni Waziri Mkuu Mstaafu au ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu?
Mie hakuna mtu minaye mchukia kama Edward ngoyai lowasa,huyu ni nembo ya uharifu nchini,matatizo yoote ya umeme yanatokana na yeye,vyama vyoote vikuu vya kisiasa ccm na chadema vilishawahi kuusema ufisadi wake hadharani.leo ninajiuliza,sijui hii heshima kaipata wapi huyu mwizi.mie ninafikiri huu niushirikiano wa mafisadi wenzie.
 
Kama kuna ukakasi kusema aliyejiuzuli ni bora waseme aliyewahi kuliko kusema aliyestaafu. Kwanza hakuna mtumishi wa ngazi ya juu anayestaafu. Hata hao marais na mawaziri wakuu huwezi kusema ni wastaafu, ni marais waliomaliza muda wao. Wanaostaafu ni wale walioacha kazi kwa mujibu sheria kwamba umri wao umefika ukomo kufanya kazi yaani miaka 60
 
"Alikubali kupoteza kunusuru serekali, kubalance serekali,kujitwisha mzigo mzito wa watu wengine, hakuwa mjinga, hakuwa fisadi, alifanya hivyo kwa sababu kwa wakati huo, tatizo lilikuwa ni Uwaziri mkuu"
Hata kama alikuwa fisadi kitengo cha kujiuzuru kilitosha kufuta yote. Haijawahi kutokea waziri mkuu kujiuzuru hapa Afrika. Mungu amuweke pema peponi
 
Hata kama alikuwa fisadi kitengo cha kujiuzuru kilitosha kufuta yote. Haijawahi kutokea waziri mkuu kujiuzuru hapa Afrika. Mungu amuweke pema peponi
Point! tuwanapiga mpaka makaburi aisee, hivi kuna mtu ambae hajawahi kuiba kweli? Hata watoto wadogo kabisa utakutana nae jikoni mdomoni kuna sukari na usoni pia, oya! si umesikia huko? Paroko kajiongeza, dah noma sana man!
 
Mbona mchizi aliweka wazi kabisa mwenye ushahidi ampeleke mahakamani vinginevyo mpige kimya. Tena aliongea kipindi yupo upinzani. Mkafyata team buku 7 wote.
Hivi mahakama ni za kuendea tu kama unaenda kukojoa kichochoroni?

Unazijua adha zisizo za lazima apatazo raia mwema mahakamani?

Kwanini watu hawapendi kuhusianishwa na kesi yoyote kwenda kuzitolea ushahidi, unaijua sababu yake au unajifanya haujui?

Je hakuna vyombo vinavyoendeshwa kwa kodi za wananchi vyenye jukumu la kufuatilia ishu za mafisadi papa hadi raia ashirikishwe kukamata bango?

Na kama taasisi hizo zipo, zilifuatilia kuona kama tuhuma hizo ni za kweli, walitoa majibu gani kwa umma?

Jambo lolote kutofikishwa mahakamani hakufanyi sababu ya jambo hilo kutokutendeka.
 
Mbona mchizi aliweka wazi kabisa mwenye ushahidi ampeleke mahakamani vinginevyo mpige kimya. Tena aliongea kipindi yupo upinzani. Mkafyata team buku 7 wote.
Kwani hujamsikia makonda niambie hapa tanzania na wizi wote uliokithiri kuna hata kiongozi mmoja mkubwa aliwahi kufikishwa mahakamani ? Au kufungwa , jela zipo kwa ajili ya masikini
 
Hata kama alikuwa fisadi kitengo cha kujiuzuru kilitosha kufuta yote. Haijawahi kutokea waziri mkuu kujiuzuru hapa Afrika. Mungu amuweke pema peponi
Haijawahi Waziri mkuu kujiuzulu Afrika kwa sababu hakuna Waziri mkuu Afrika aliyewahi kufanya ufisadi mkubwa na wazi kama aliofanya Lowasa. Mpaka leo tunateseka na madhara ya alivyofanya
 
Ni kweli. Mimi nashangaa sana watu wanavyomtukuza Mkapa.

Huku mkapa mwenyewe amekiri na kuomba msamaha kwenye kitabu chake kwa ufisadi alioufanya.

Mtu unaiba mabilioni unatia nchi hasara harafu kirahisi tu unaomba msamaha na unatukuzwa
 
Oh kumbe lowasa ndo alikuwa fisadi pekee hapa tanzania? Na baada ya kifo chake ufisadi umeisha?

Lowassa kazaliwa kwenye mipesa mpaka anakufa mipesa kwao ipo.

Wengine wamezaliwa kwenye umasikini kama mimi, hao ndo fisadi wa kutupa , walisoma peku miguuni kwa sasa wana pesa za wizi.

Tofautisha mtoto alozaliwa kwenye pesa na aliezaliwa maisha ya kuunga.

Rip Lowassa.
 
Mbona mchizi aliweka wazi kabisa mwenye ushahidi ampeleke mahakamani vinginevyo mpige kimya. Tena aliongea kipindi yupo upinzani. Mkafyata team buku 7 wote.
Unamaanisha Lisu alimsingizia alipotuambia ana ushahidi juu ya uhusika wa Lowwassa Richmond?
 
Back
Top Bottom