Hakika majaji wanaweza kuwa na rasimu ya hukumu vichwani mwao. Hata sisi wafuatiliaji wa mwenendo wa ushahidi mahakamani wa kesi hiyo tuna hukumu zetu (zisizo rasmi) vichwani mwetu. Tunasubiri hukumu ya mahakama kulinganisha na za kwetu, kama tulivyoshangazwa na ruling of prima facie case iliyosema TL has a case to answer.
Nakumbuka Mhe Jaji Mkuu Mstaafu, mzee wangu Barnabas Albert Samatta aliwahi kuwaambia hivi mahakimu ktk ufunguzi wa moja ya mikutano yao, ambao mimi nilihudhuria kama mwandishi wa habari za mahakama:-
"Hakimu au Jaji unaposikiliza kesi ya jinai katika mahakama ya wazi, wasikilizaji makini hufuatilia ushahidi wote kwa kiwango cha upeo wao wa uelewa. Hivyo, kabla hujatoa hukumu, hao wananchi na hasa mshitakiwa mwenyewe anakuwa na hukumu yake. Wanachosubiri tu ni wewe hakimu usome hukumu yako wao walinganishe na hukumu ya kwao.
Ikiwa hukumu yako ipo sawa na ya kwao, wanaamini haki imetendeka. Ikiwa tofauti, wanasikiliza kwa makini uchambuzi wako wa ushahidi unaotofautisha na wa kwao pamoja na sababu unazotoa za kumtia hatiani mshitakiwa au kumwachia huru.
Wakiridhishwa na uchambuzi wako wa ushahidi pamoja na sheria ilivyokuongoza, wanaweza Kuaminishwa haki imetendeka. Lakini ikiwa hukumu yako haielezi vizuri ushahidi wote na kueleza kosa lilivyodhibitika bila shaka yoyote au kutodhibitika bila shaka yoyote, wananchi wafuatiliaji (msikilizaji wa kesi yote mahakamani) wataona Hakimu au Jaji hakutenda haki.
Hivyo hakimu jitahidi kuwa makini wakati wa kusikiliza kesi ukitambua kuna wasikilizaji ambao nao wataandika hukumu zao. Aidha, sheria haiwazuii watu wengine kusikiliza kesi unayoendesha na kutoa maoni yao baada ya hukumu.
Kwa upande wa mshitakiwa akitiwa hatiani na kupewa adhabu, huwa ana haki ya kukata rufaa. Wewe mwenyewe unapaswa kutamka unampa hiyo haki meaning ya hukumu yako. " (Hiyo nukuu sio rasmi ila nimeparaphrase kwa kumbukumbu niliyonayo ya about 30 yrs ago).
AAK Jnr, SC, Esq. 16th September, 2026