Hivi Makonda ndio wakuishi kama digidigi kweli?


Tofautisha maigizo na uhalisia. Makonda kajificha hakuna Cha kula Bata Wala Nini. Maana hiyo kesi Ni mtego kwake itazaa zingine.
 
Hata hapa kwenye huu uzi wapo nimewaona wengi tuu.. Wanalipa fadhila japo kwa mbali na kwa kujificha nyuma ya ID feki na wengine ni ma home boy!
Hata hawa walioko madarakani sasa wajifunze kuwa anayewabeba sahizi ataondoka kwenye nafasi yake nao watakuwa kama Bashite.
Dunia ya Mungu hii tujifunze kukanyaga hii ardhi kwa adabu.
Huwa nikisoma hadithi ya Mfalme Suleiman huwa naelewa ni kwa nini aliamua kuomba hekima kabla ya kitu kingine chochote. Alijua kuwa madaraka huwa yanalevya
 
 
Amekuwa "fugitive" (sijui kiswahili chake).
 
Bashite ni ndezi.
 
Hehe hili ni shauri la kiraia na sio la serikali. Halina mashiko yoyote aliepeleka amefanya kwa nia za kisiasa ila kila siku asikike katika habari anamuomba Makonda aende mahakamani.

Makonda anapiga mazoezi kila siku uwanja wa Oysterbay.
Mwingine yuko A town, wewe unasema O'bay, nani yuko sahihi? Kwa kutangazwa tu anatafutwa na mamlaka rasmi ya mahakama inatosha kumdhalilisha.
 
Ukute huo uhuru mwenzetu ndo anazidi kudidimiza umaskini kwa miburungutu myekundu!.

Me siyajui sana haya Mambo!
Umenikumbusha mbali miaka ile jamaa anatafutwa nchi mzima hapatikani. Kumbe jamaa wanachukua mbesai wanamwachia. Lakini mbesai ilipokwisha wakamkamata harakaharaka na kumsweka lupango. Ila alivyokuwa smart alijitetea mwenyewe na kushinda ile kesi!
 
Tatizo ni katiba mbovu inayoweza kutupatia rais mbovu na akateua viongozi wabovu sababu hakuna vigezo
 
Mlezi wa wasafi😁
 
Na 'refugee' kiswahili ni nani? Labda ndo 'uswila'[emoji125][emoji125]
Kuna ukimbizi wa kukimbia ukiwa unatafutwa fugitive

Kuna ukimbizi wa kivita kujiokoa refuge..kutafuta hifadhi refugee ni mkimbizi wa kivita mtafuta hifadhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…