Hivi mamlaka husika zilikuwa wapi mpaka kipande cha "unyanyasaji wa kingono" kinaandikwa kwenye kitabu cha Kabendera?

Nimeisikilaza clip ya Erick Kabendera yote. Nimemuelewa kiasi. Alipata taarifa nyingi kuhusu mambo mengi. Kuna maelezo yake yana utata. Amesema eti Magufuli hakupenda kuhojiwa na wana habari. Lakini nakumbuka kuna mkutano wake aliulizwa maswali na waandishi na mmojawapo ni Pascal Mayala, mpaka akamtania kuwa jina lake lina maana ya njaa. Kuhusu Azory Gwanda kule Kibiti, naiunga mkono Serikali kwa dhati ya moyo wangu kukomesha mauaji ya maafisa wa serikali na Viongozi mbalimbali. Kama Jeshi au taasisi yoyote isingeingilia kati, leo hii Tanzania ya kusini au kote kabisa ingekuwa haitawaliki na tungekuwa tunakimbia na magodoro kama Congo na Nigeria kuwakimbia magaidi. Sikuwahi kuogopa kama kama kipindi hicho. Mashamba yalitelekezwa, watu waliacha kazi. Kabendera yuko sahihi kwa sehemu, ila mengine hapana.
 
Sasa mbona na wewe unazidi kulisambaza?
 
Yupo kwa mabeberu huko serikali yako haina la kumfanya.
Hukuona hata kale kadada ka Marekani kalivyokua kanaandika upupu na kutweza utu wa viongozi waziwazi.
Serikali yako ikaishia kupeleka malalamiko kwa Mark Zuckerberg
 
Usidhani Kabendera ni kichaa. Yule bwana alikuwa nusu mnyama.
 
Ulitaka apige picha za pajama? Wee ukiwa unachepula hua unatangaza watu waje wapige picha?
 

Acha kumkashifu rais wetu miaka 60 ya samia kuishi kwenye kiyoyozi unafikiri ni sawa na miaka 60 mtu baki raia wa kawaida ?mama samia ni pisi ya kwenda ni mzuri looh
 
Kwa nchi yetu hii, Mambo ya hovyo mengi Sana, Mkapa alipigwa na mke wake akavunjwa mguu, Kuna CEO, mmoja, Mambo ya unyanyasaji kijinsia yamejaa Sana kwenye serikali,
Nikikimbuka yale ya RC Simiyu na Mwanajeshi Dodoma. Yapo mengi kweli
 
Sasa hivi tutakuwa tukimwangalia mara tunaanza kupata hisia za kile alichokiandika bwana kaflag!
Kwa kweli amemkosea sana heshima Mh. Rais
 
Yaani Mnamwongelea magu kama vile aliishi enzi za nyerere. As if sisi wengine hatukuwepo.

Mnajidanganya tu
 
Acha kumkashifu rais wetu miaka 60 ya samia kuishi kwenye kiyoyozi unafikiri ni sawa na miaka 60 mtu baki raia wa kawaida ?mama samia ni pisi ya kwenda ni mzuri looh
Marehemu aliwahi kukiri mama anamvuruga🤣🤣🤣 itakuwa hiyo siku upwiru ulikaba koo, ila baba ajifunze, wakati yeye kaenda kulala mitala huku wenzie wanataka kumsolea mke🤣
 
M

Mwaka wa uchaguzi huu.... Nasikia KULE kwa kijani Kuna makundi.... Kambi ya mwendazake na ya aliyepo, ili kunyong'onyeza Kambi pinzani... Yamemwagwa haya!
Inawezekana kina baraka na jumba jeupe
 
Taarifa sio ya hovyo, bali aliyetaka kutenda tendo hilo ndiye wa hovyo.
 
Amefanya mengi kwa kutoa roho za watu sio kwa kujitoa
Nyinyi wanaharakati wa humu jamvini akili zenu zinaeleweka, mwananchi wa kawaida anayefaidika na zahanati huko mikoani hana kabisa fikra hizi za kwenu.

Mfanyabiashara wa kule Njombe anayeuza matikiti nje ya nchi kwa kuyabeba kwenye ndege za ATC zilizonunuliwa na hayati JPM hana muda wa kuziamini hizi hekaya zenu wasomi wa X.

Anayetumia treni ya SGR kila wiki kwenda Dodoma na kurudi hana muda wa kuziamini hizi habari za kipuuzi mnazozisambaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…