Hivi Manqoba bado ni kocha wa Yanga?

Hivi Manqoba bado ni kocha wa Yanga?

Simba walikuwa na matatizo yote.

Tatizo la wachezaji duni(Mukwala,Mutale,nk) na makocha duni.

Kwa sasa wamebaki na baadhi ya wachezaji duni mfano Doumbia ila kocha wanaye.

Yanga wana tatizo na kocha sio wachezaji.

Wachezaji hao hao nakuhakikishia ukimpa mtu kama miloudi au Gamondi utaona timu itakavyobadilika kiuchezaji.

Ligi ya ndani huwa haina majibu, hata Simba uhalisia haswa ulionekana kwenye makundi ya CAFCL, ngoja mwezi ujao makundi yaanze ndo tutafahamu mbichi na mbivu..
 
Man U bado wana Carrick , na timu nyingi za Ulaya wanavumilia sana makocha .

Bongo mashabiki Wanataka kila siku ushinde , Arteta angekuwa bongo kipindi kile anafanya vibaya tayari Hana kazi
Ndio hivyo
Kwanza mpira ni kushinda,kushindwa ama droo.
Sasa wao kupoteza ajabu ni ipi?
Wanapoteza Barca sembuse YANGA?
Wajifunze uvumilivu.warekebishe penye mapungufu
 
Wengine tunaupenda,tunaujua na uvumilivu tunao.

Manqoba hatosho kuinoa Yanga.

Badala ya kukuza viwango vya wachezaji anaviua.

Timu inapata tabu sana kupata ushindi.

Ukiona mechi Yanga kashinda nne ujue tulitakiwa kushinda 8.

Kwenye sub hata mimi namzidi maarifa.

Akifanya sub tu timu inakosa balance na kufa kabisa.
Kama shida ni kocha basi
Msipojiangalia na uwekezaji wote huu ligi ya mabingwa mnaenda kupoteza
 
Kama shida ni kocha basi
Msipojiangalia na uwekezaji wote huu ligi ya mabingwa mnaenda kupoteza
Hivi unaamini kabisa Yanga hii itachukua klabu bingwa?

Kabisa unaamini hivyo?

Chini ha huyu kocha hata tukitoboa makundi ni jambo la kushkuru sana.

Kama Geita,Gaborone fc na Simba wanakutoa jasho na kukunyanyasa fikiria hiyo klabu bingwa itakuwaje na unakutana na timu zenye quality ya juu.

Kwa kifupi hakuna matumaini ya Yanga kufanya vizuri klabu bingws kama tunabaki na Manqoba.
 
Wabongo wengi mpira hatujui, kocha hata miezi 6 hajafikisha, timu wachezaji wengi wageni wanataka afanye nini!

Kocha wa Simba ana mwaka na maingizo kwenye timu yake hayazidi 2 timu lazima iwe vizuri!
Tuwe na subra!
Tupo desperate na matokeo tunayotala ni ya aina Moja tu.
Mkimfukuza mnqoba akaletwa mwingine kipigo kikiendelea tutasema shida Nini?
 
Hivi unaamini kabisa Yanga hii itachukua klabu bingwa?

Kabisa unaamini hivyo?

Chini ha huyu kocha hata tukitoboa makundi ni jambo la kushkuru sana.

Kama Geita,Gaborone fc na Simba wanakutoa jasho na kukunyanyasa fikiria hiyo klabu bingwa itakuwaje na unakutana na timu zenye quality ya juu.

Kwa kifupi hakuna matumaini ya Yanga kufanya vizuri klabu bingws kama tunabaki na Manqoba.
sijui ila lolote linawezekana
Enzi za gamondi na yule wa kabla yake aliewafikisha final confederation cup YANGA ilikuwa fierce.inatembeza kichapo bila huruma
Siku hizi mpaka NBC imekuwa legelege
 
Mjomba una hoja nzuri. Sema tu umeileta jukwaani huku ukiwa una hasira kali. Huyo kocha ni ukweli uwezo wake siyo mkubwa kihivyo (na hasa kwenye kipengele cha mbinu).
Jamaa ni mbahatishaji tu. Sub zake anazofanya ni ushahidi tosha.

Lakini kusema yeye ni TAPELI! Kwa hapa nakataa. Kwa sababu ameajiriwa kihalali na uongozi wa klabu baada ya kujiridhisha anafaa kama ilivyokuwa kwa yule Roman Folz. Kwa hiyo tusimuite majina asiyostahili.

Natambua fika haya matokeo ya kufungwa yametuumiza mashabiki, wachezaji, wanachama, viongozi, benchi la ufundi, na hata wachezaji wenyewe.
Tukubali mpira ni mchezo wa makosa. Tumefanya makosa, tumeadhibiwa. Tujipange kwa michezo mingine ya ligi.

Beki zenyewe ni akina Mwamnyeto waliofungwa magunia ya misumari miguuni! Hata akija Pep Guardiola unategemea ataweza kuwakimbiza akina Libase Gueye na Ellie Mpanzu?

Ikitokea makosa na madhaifu yake yakaendelea kutawala basi uongozi una haki ya kusitisha mkataba wake.
 
Huyu tapeli wa kuitwa Manqoba mngqithi bado ni kocha wa Yanga?

Kama bado anasubiri nini?

Engineer fukuza haraka sana huyu tapeli before it's too late.

Hawezi kuivusha Yanga makundi ya klabu bingwa wala kutetea ubingwa wa NBC.

Ameshaonesha si kocha anayetoshea hata kama mechi na Simba tungeshinda.

Yanga sio timu ya majaribio na kukuza profile za makocha.

#Ukicheka na nyani utavuna mabua.
Kama bado yupo Hadi Sasa itakuwa anatumia ndumba sio Bure

Timu imekatika kati Baada ya kuumia Abuya alafu anamtoa na Mudathiri kumalizia kabisa
Hamna kitu mule box tu lile
 
Wabongo wengi mpira hatujui, kocha hata miezi 6 hajafikisha, timu wachezaji wengi wageni wanataka afanye nini!

Kocha wa Simba ana mwaka na maingizo kwenye timu yake hayazidi 2 timu lazima iwe vizuri!
Tuwe na subra!
Mkuu ni hivi; maendeleo ni muonekano hata kama ni jambo la hatua ila tunapima kwa mwenendo unaelekea nao. Yanga jinsi ilivyoanza na jinsi inavyokuwa kadri siku zinavyozidi kwenda sio mwenendo mzuri bali ni mwenendo mbaya. Kwenye mpira kabla ya matokeo huwa tunaangalia performance ya timu. Mfano ile mechi ya juzi hata Simba wangekuwa wamefungwa goli moja hadi mwisho lakini walichoonesha kiwanjani ni performance ya hali ya juu dhidi ya mpinzani wake na wangetoka na kitu positive.

Yanga imecheza na Fountain gate, Pamba unaona kabisa timu inachemea chemea. Imecheza na Geita na Gaborone kisha mashabiki tunaomba msaada wa refa apulize filimbi mpir uishe. Hapo ni against timu za kawaida tu, imekuja mechi ya Simba ikamalizia kuonesha madhaifu ya timu. Halafu unasema apewe muda upi wakati kadri siku inavyozidi kwenda timu haisogei mbele kwenye performance?

Tuliona kwa Nabi, Gamondi na Miloud hata timu ikiwa haijapata matokeo ila unaona mwanga kuwa tunaelekea kuzuri hivyo tumpe muda kocha. Sasa tumpe muda kwa lipi? La kufanya Yanga sehemu ya kukuzia vipaji vya watoto ndilo la maana kwa timu? Mkuu embu nishawishi ni kipi positive kwa huyu kocha ulichokiona ili tumvumilie.
 
Kwamba mechi moja tu afukuzwe? Vyura mna shida kubwa
Uliangalia mechi na Geita?

Uliangalia mechi na Gaborone Fc?

Mechi na Simba umeona unyanyasaji aliofanyiwa Yanga?

Uliangalia Yanga ya Gamondi iliavyompeleka puta Mamelodi?

Kwanini licha ya Yanga kutolewa na Mamelodi watu hawakupiga kelele Gamondi afukuzwe?

Simply because Yanga alionesha kiwango cha juu sana ambacho mtu yoyote akiitazama timu anaona ina kitu kikubwa na very promising inacho.

Sasa hii Yanga ya mpigwa miti kila siku inazidi kuwa mbovu.

Mechi na Gaborone FC tumenyanyasika kibahatibahati tukaokolewa na Mwalimu.

Mechi na Simba ni zaidi ya unyanyasaji.

Yanga tulizidiwa kila angle na hata ukiitazama timu uoni inachokupromise zaidi ya kuona inazidi kuelekea shimoni tu.

Kwa kifupi akiendelea kubaki huyu mpigwa miti Yanga itaaibika sana tu.
 
Bwashee sitaki kusema sana kwa sababu wewe ni ndugu yangu wa damu😅😅 ile kiukweli tuliwabaka bila kilainishi😁
 
Bwashee sitaki kusema sana kwa sababu wewe ni ndugu yangu wa damu😅😅 ile kiukweli tunawabaka bila kilainishi😁
Bawshee mlipiga mpira mkubwa sana mpaka nikawa nashangaa hawa makolo huu mpira wameutoa wapi!

Daah kuanzia ball possession shots on target mpaka passes uko kote mmetukaanga.

Ila ndio soka acha tujipange tutarudi tena tukiwa strong.
 
Hatuwezi kufukuza kocha anayetaka kutupa ubingwa wa afrika au wewe hutaki tuwe mabingwa wa Afrika.
Unyanyasike na timu za daraja dogo kina Geita na Gaborone.

Uje unyanyaswe na Simba inayojitafuta bado haijafika kilele chake cha ubora ndio ipo njiani.

Halafu uje utarajie ubingwa wa afrika.

Hiyo nbc tu ipo mshakani kuna uwezekano mkubwa simba akapita nayo.
 
Back
Top Bottom