Hivi Manqoba bado ni kocha wa Yanga?

Hivi Manqoba bado ni kocha wa Yanga?

Bawshee mlipiga mpira mkubwa sana mpaka nikawa nashangaa hawa makolo huu mpira wameutoa wapi!

Daah kuanzia ball possession shots on target mpaka passes uko kote mmetukaanga.

Ila ndio soka acha tujipange tutarudi tena tukiwa strong.
Huo ndio mpira wetu kipindi cha kina mikson alhali ya misri walibana mbupu kumbuka🤣
 
Huo ndio mpira wetu kipindi cha kina mikson alhali ya misri walizipa mbupu kumbuka🤣
Hatari sana.

Mpaka huruma.

Yani ilifika kipindi mchezaji wetu akipata mpira hata wa kumpasia hamuoni.

Kupiga pasi tatu kwa mbinde sana.

Hakika mliupiga mwingi makolo.
 
Hatari sana.

Mpaka huruma.

Yani ilifika kipindi mchezaji wetu akipata mpira hata wa kumpasia hamuoni.

Kupiga pasi tatu kwa mbinde sana.

Hakika mliupiga mwingi makolo.
Hahaha asante sana na jana tulikunya jangwani mliona?😁
 
Wengine tunaupenda,tunaujua na uvumilivu tunao.

Manqoba hatosho kuinoa Yanga.

Badala ya kukuza viwango vya wachezaji anaviua.

Timu inapata tabu sana kupata ushindi.

Ukiona mechi Yanga kashinda nne ujue tulitakiwa kushinda 8.

Kwenye sub hata mimi namzidi maarifa.

Akifanya sub tu timu inakosa balance na kufa kabisa.
Tatizo siyo kufukuza je stahiki zake baada ya kuvunja mkataba atalipa nani? Ndo unakuta klabu inadaiwa madeni kabao chanzo ni kuvunja mikataba mbalimbali ya makocha .
 
Unyanyasike na timu za daraja dogo kina Geita na Gaborone.

Uje unyanyaswe na Simba inayojitafuta bado haijafika kilele chake cha ubora ndio ipo njiani.

Halafu uje utarajie ubingwa wa afrika.

Hiyo nbc tu ipo mshakani kuna uwezekano mkubwa simba akapita nayo.
Mbona mechi ya ngao ya jamii Simba alinyanyaswa na hujaongelea hilo!
Kocha apewe mda ajenge timu yake, Gamond alitembelea misingi aliyojenga Nabi, naona mnamsifu sana bila kutoa credit kwa mtangulizi wake!
 
Simba si timu ya kuifinga yanga;lakini ukiamua kupaki nyuma ili kulinda goli Moja.Forwad ya Simba ni wepesi na Wana spidi kufungwa ni lazima.Baada ya hafutaimu yanga ilipasa kuimarisha katikati ili kuzuia na kupeleka mipira mbele.Asante Boka kwa kurudisha mipira mbele mara kwa mara
 
Mbona mechi ya ngao ya jamii Simba alinyanyaswa na hujaongelea hilo!
Kocha apewe mda ajenge timu yake, Gamond alitembelea misingi aliyojenga Nabi, naona mnamsifu sana bila kutoa credit kwa mtangulizi wake!
Mkuu kwenye mpira wa miguu, hakuna kitu kinachoitwa kutembelea misingi ya kocha fulani, ingekuwa ipo hii kitu basi kazi ya makocha ingekuwa ni nyepesi sana. Hakuna kazi ngumu kama ku maintain standard iliyowekwa na mtangulizi wako. Ingekuwa ni jambo rahisi basi yule Folz tusingemuona ni tapeli, ingekuwa ni rahisi basi yule kocha aliyefuata baada ya Gamondi asingeonekana miyeyusho. Pamoja na Sir Alex Ferguson kuiongoza Man united kwa miaka kibao na kuipa mafanikio ila alipo staff tu aliyechukua nafasi yake (Dadid Moyes) alishindwa kuifanya Man united ibakie na ubora ule ule na akatimuliwa.
 
Huyu tapeli wa kuitwa Manqoba mngqithi bado ni kocha wa Yanga?

Kama bado anasubiri nini?

Engineer fukuza haraka sana huyu tapeli before it's too late.

Hawezi kuivusha Yanga makundi ya klabu bingwa wala kutetea ubingwa wa NBC.

Ameshaonesha si kocha anayetoshea hata kama mechi na Simba tungeshinda.

Yanga sio timu ya majaribio na kukuza profile za makocha.

#Ukicheka na nyani utavuna mabua.
Siupendi ule msemo wa... Coaches are hired to be fired
 
Unyanyasike na timu za daraja dogo kina Geita na Gaborone.

Uje unyanyaswe na Simba inayojitafuta bado haijafika kilele chake cha ubora ndio ipo njiani.

Halafu uje utarajie ubingwa wa afrika.

Hiyo nbc tu ipo mshakani kuna uwezekano mkubwa simba akapita nayo.
Nyinyi Simba mnataka tumwache kocha aili tusichukue ubingwa wa Afrika njama zenu tumezigundua.
 
Huyu tapeli wa kuitwa Manqoba mngqithi bado ni kocha wa Yanga?

Kama bado anasubiri nini?

Engineer fukuza haraka sana huyu tapeli before it's too late.

Hawezi kuivusha Yanga makundi ya klabu bingwa wala kutetea ubingwa wa NBC.

Ameshaonesha si kocha anayetoshea hata kama mechi na Simba tungeshinda.

Yanga sio timu ya majaribio na kukuza profile za makocha.

#Ukicheka na nyani utavuna mabua.
Wabongo mpira hamjui kkenge nyie
 
Ila wabongo hatuna uvumilivu kabisa, yaani hata kocha awe mzuri vipi tutamtia preassure + kumchafua hadi aonekane hafai. Sasa kocha kafungwa gemu moja tu kwenye ligi tayari anaonekana ni tapeli hafai kabisa! Ndugu zangu wananchi wenzangu huu ni mpira wa miguu kuna matokeo ya kufungwa pia. Acheni hizo tumpe nafasi afanye kazi yake.
 
Manqoba sio kocha mzuri tusidanganyane.

Kocha mzuri anaonekana tu hata timu ikifungwa kuna vitu vinakupa matumaini.

Leo hii Barcelona ya Hansi Flick ikifungwa huwezi kumwita kocha mbaya.

Timu inavyocheza unaona leo tumefungwa ni siku mbaya tu kazini tu.

Lakini kocha wako Manqoba kadiri siku zinavyokwenda anazidi kuiua timu badala ya kuikuza.

Hana mpira wowote wa kuvutia wala wa kuweka matumaini kwamba timu itakaa sawa.
 
Back
Top Bottom