Hivi Manqoba bado ni kocha wa Yanga?

Bawshee mlipiga mpira mkubwa sana mpaka nikawa nashangaa hawa makolo huu mpira wameutoa wapi!

Daah kuanzia ball possession shots on target mpaka passes uko kote mmetukaanga.

Ila ndio soka acha tujipange tutarudi tena tukiwa strong.
Huo ndio mpira wetu kipindi cha kina mikson alhali ya misri walibana mbupu kumbuka🤣
 
Huo ndio mpira wetu kipindi cha kina mikson alhali ya misri walizipa mbupu kumbuka🤣
Hatari sana.

Mpaka huruma.

Yani ilifika kipindi mchezaji wetu akipata mpira hata wa kumpasia hamuoni.

Kupiga pasi tatu kwa mbinde sana.

Hakika mliupiga mwingi makolo.
 
Hatari sana.

Mpaka huruma.

Yani ilifika kipindi mchezaji wetu akipata mpira hata wa kumpasia hamuoni.

Kupiga pasi tatu kwa mbinde sana.

Hakika mliupiga mwingi makolo.
Hahaha asante sana na jana tulikunya jangwani mliona?😁
 
Tatizo siyo kufukuza je stahiki zake baada ya kuvunja mkataba atalipa nani? Ndo unakuta klabu inadaiwa madeni kabao chanzo ni kuvunja mikataba mbalimbali ya makocha .
 
Mbona mechi ya ngao ya jamii Simba alinyanyaswa na hujaongelea hilo!
Kocha apewe mda ajenge timu yake, Gamond alitembelea misingi aliyojenga Nabi, naona mnamsifu sana bila kutoa credit kwa mtangulizi wake!
 
Simba si timu ya kuifinga yanga;lakini ukiamua kupaki nyuma ili kulinda goli Moja.Forwad ya Simba ni wepesi na Wana spidi kufungwa ni lazima.Baada ya hafutaimu yanga ilipasa kuimarisha katikati ili kuzuia na kupeleka mipira mbele.Asante Boka kwa kurudisha mipira mbele mara kwa mara
 
Mbona mechi ya ngao ya jamii Simba alinyanyaswa na hujaongelea hilo!
Kocha apewe mda ajenge timu yake, Gamond alitembelea misingi aliyojenga Nabi, naona mnamsifu sana bila kutoa credit kwa mtangulizi wake!
Mkuu kwenye mpira wa miguu, hakuna kitu kinachoitwa kutembelea misingi ya kocha fulani, ingekuwa ipo hii kitu basi kazi ya makocha ingekuwa ni nyepesi sana. Hakuna kazi ngumu kama ku maintain standard iliyowekwa na mtangulizi wako. Ingekuwa ni jambo rahisi basi yule Folz tusingemuona ni tapeli, ingekuwa ni rahisi basi yule kocha aliyefuata baada ya Gamondi asingeonekana miyeyusho. Pamoja na Sir Alex Ferguson kuiongoza Man united kwa miaka kibao na kuipa mafanikio ila alipo staff tu aliyechukua nafasi yake (Dadid Moyes) alishindwa kuifanya Man united ibakie na ubora ule ule na akatimuliwa.
 
Siupendi ule msemo wa... Coaches are hired to be fired
 
Nyinyi Simba mnataka tumwache kocha aili tusichukue ubingwa wa Afrika njama zenu tumezigundua.
 
Wabongo mpira hamjui kkenge nyie
 
Ila wabongo hatuna uvumilivu kabisa, yaani hata kocha awe mzuri vipi tutamtia preassure + kumchafua hadi aonekane hafai. Sasa kocha kafungwa gemu moja tu kwenye ligi tayari anaonekana ni tapeli hafai kabisa! Ndugu zangu wananchi wenzangu huu ni mpira wa miguu kuna matokeo ya kufungwa pia. Acheni hizo tumpe nafasi afanye kazi yake.
 
Manqoba sio kocha mzuri tusidanganyane.

Kocha mzuri anaonekana tu hata timu ikifungwa kuna vitu vinakupa matumaini.

Leo hii Barcelona ya Hansi Flick ikifungwa huwezi kumwita kocha mbaya.

Timu inavyocheza unaona leo tumefungwa ni siku mbaya tu kazini tu.

Lakini kocha wako Manqoba kadiri siku zinavyokwenda anazidi kuiua timu badala ya kuikuza.

Hana mpira wowote wa kuvutia wala wa kuweka matumaini kwamba timu itakaa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…