Hivi mbona watoto wa siku hizi hawachezi michezo tuliyocheza zamani kama kombolela?

Kombolela ulikuwa wa kiboya ila kuteneneza maari illikuwa poa sana. Siku hizi watoto wanaishia kuchezea ready made na kutazama makatuni.
 
Hivi mkuu marekani na sisi Tanzania yupi mbunifu na wenye uwezo wa kutumia akili?
 
Mkuu hicho ni kitu cha msingi kabisa ni creativity, yani mtoto kuona gari naye akatengeneza la kwake siyo kitu kidogo. Kuona pikipiki akatengeneza yake ni kitu kikubwa. kinachangamsha ubongo
Mtoto ni wewe, wewe ni mtoto uliyekuwa nawewe ndio yule mtoto alitengeneza magari ya migomba tunekubaliani.

Weka connection ya list yako yote ya hiyo michezo na maisha ya sasahivi. Imesaidia nini kwako binafsi na kijamii ?!
 
Kuna mdau humu anaona ni kama ujinga. Mimi niko mtaani siku hizi sioni kabisa watoto wakicheza kama sisi zamani. Ni kweli mazingira yamebadilika lakini si mazuri kwa makuzi ya watoto wetu
 
Michezo ya watoto ya kiswahili ni gender based!! wasichana wanacheza peke yao na wavulana peke yao.Hakujawahi tokea michezo ya mchanganyiko ya watoto wa kiume na wa kike ya kiasili.Ya kizungu ndio ina shida ya hiyo mitatizo ya ngono

Kwa taarifa nchi zote zinazothamini mambo ya zamani ndizo ziko developed.Mfano uingereza bado wana ufalme sisi uchifu tuliua, Japan pia,Norway,Sweden,DENMARK nk

Ukienda china wengi hawamezi panadol wanakunywa chinese traditional medicine dawa zao za zamani ni ziko juu hasa

Mwaka 1949 CHINA KULIFANYIKA kitu kinaitwa cultural revolution ambako mao tse tung alifunga mipaka yote ya china akasema marufuku ku import kitu chochote toka nje ya nchi na marufuku ku export chochote kiwe mila na destuiri dini nk akafunga uchumi (closed economy) Wakasema mzee tutaishije akasema bunini vya kwenu.Ndipo wachina waliopanza ugunduzi wa hali ya juu kwenye kila eneo ili watimize mahitaji ya wachina sasa hivi china soko limefurika wamekuwa giants wa exports hakuna nchi afrika hata tanzania hakuna nyumba isiyo na kitu cha kichina iwe cha ujenzi,jikoni ,stationary nk

Ona wahindi wanavyoenzi vitu vya zamani vya kwao wana hadi vyuo vikuu vya traditional medicine wanatoa hadi PHD wana maandishi yao ya zamani wanafundisha elimu kwa kutumia lugha yao na maandishi yao toka chekechea hadi phd

WACHINA,WAJAPAN,WAHINDI NA WAARABU wana maandishi ya kwao yasiyo haya ya mzungu ya a,b,c,d nk na lugha yao vitu vya zamani na wanavitumia kufundishia kuanzia chekechea hadi PHD kwa lugha na maandishi yao

Sisi waafrika ni homeless ni breed isiyo na chake cha zamani kazi kudakia dakia tu vya wengine kama mabwege.Hata michezo tu mtu una import video games si ubwege huo.Huwezi buni hata mchezo wako au ukafufua wako wa kale .Hata kucheza tu unataka kucheza kizungu!!! very funny!!

Sisi waafrika ndio peke yetu duniani ambao vyetu vya zamani tuna vizomea!!! tunachekelea mi video game ya wazungu na kuzomea vyetu.Hivi unaona raha gani hadi mtoto michezo a import toka nje ya nchi!!!
 
Weka vitu vitano ambacho ni matokeo ya ubunifu na uwezo wa kutumia akili kutoka africa, kabla ya video games.
 
Unadhani kwanini hao wajapan walimchukua?

Unadhani kama angebaki hapa angekuwa nani sasa hivi?

Point yako ni nini?
Walimchukua kule sababu kwanza walimuona ana akili wabunifu na nchi zao zinahitaji watu wenye akili wabunifu ,Sisi hatuhitaji wabunifu tunahitaji vitu vilivyobuniwa tayari sisi ni users tu!!! Wakaona aweza kufanya vizuri kule kwao kwenye maabara zao za ubunifu kuliko huku aweza wapa business kule akitengeneza waweza uza sana huku sababu sisi tunaabudu vitu made in Japan kuliko made in Tanzania!! Hata mimi nikigundua kitu naenda ulaya au marekani nitengenezee kule niiletee mibwege ya Africa inayoamini katika made in EUROPE and USA kwa sababu ukitengenezea hapa inakuponda!!


Angebaki angekuwa lofa tu sababu wajinga wangesema kimti tu sio deal sababu vichwa vyao vimezoea ready made za nje ya nchi wasingeona kuna maana yeyote wangemwona yule mtoto mjinga tu kumbe wao ndio mipumbavu mikubwa
 
Weka vitu vitano ambacho ni matokeo ya ubunifu na uwezo wa kutumia akili kutoka africa, kabla ya video games.
Kwanza sijawahi cheza video games mimi wala watoto wangu huwa naona ujinga mtupu ,Michezo kwangu ni ile ya kucheza physically KWANGU VIDEO GAMES SIO UBUNIFU NI UPUMBAVU TU WA KUPUMBAZA AKILI
 
Uzi unazungumzia Traditional Culture au michezo ya watoto mbonabunachanganya mambo.
 
Kwanza sijawahi cheza video games mimi wala watoto wangu huwa naona ujinga mtupu ,Michezo kwangu ni ile ya kucheza physically KWANGU VIDEO GAMES SIO UBUNIFU NI UPUMBAVU TU WA KUPUMBAZA AKILI
Feudalism thought; unajaribu kuweka watoto wako kwenye Vacuum ya ukoloni.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Yaani hii kila saa inaonyeshwa kuanzia asubuhi mpaka usiku.

Mi huwa nawashawishi wanangu wasilipende, sijui cartoon gani lile bora watazame Alvin & Chipmunks!
 
Reactions: amu
Mtoto anayejenga interest kwenye kuangalia Animation Movie, Gaming nk...ana percentage kubwa kuja kuwa mbunifu na kujenga Malengo makubwa.
 
Mjini ndio hakuna hiyo michezo, ila kijijini hadi keshokutwa watoto wanacheza hiyo michezo.
 
Mtoto ni wewe, wewe ni mtoto uliyekuwa nawewe ndio yule mtoto alitengeneza magari ya migomba tunekubaliani.

Weka connection ya list yako yote ya hiyo michezo na maisha ya sasahivi. Imesaidia nini kwako binafsi na kijamii ?!
Imenifanya kuwa mbunifu na surviver imenifanya niwe dare devil.
 
Unahisi ambaye hakufanya sio wabunifu na surviver, je sio ma Dear Devil ??
Wengi wao soft soft tu kama lotion. Hivi unajiuliza kwanini watu weupe namaanisha wachina, wazungu uwa wanapenda wapa watoto wao buildin blocks wachezee?
 
Wengi wao soft soft tu kama lotion. Hivi unajiuliza kwanini watu weupe namaanisha wachina, wazungu uwa wanapenda wapa watoto wao buildin blocks wachezee?
Soft soft kivipi unataka kutuambia wewe mkakamavu kwa kuruka ukiti wa meme wa meme.
 
Michezo ya kiswahili ni gender based? hiyo sikubali hata uniamshe nikiwa bado nipo ndotoni, humu jf Kuna watu wengi wanaonesha jinsi walivyoanza ngono mapema na sababu kubwa ni hiyo michezo na mmoja wapo kati ya mingi ni kombolela.
Kama darasani wanachanganyika kwanini nyumbani wasichanganyike?


Kufanya kitu fulani mradi fulani kafanya huko ni kutumia akili vibaya, bila shaka wewe unatambua vibaya na vizuri sasa niambie kwa akili yako tamaduni za Africa ni mbaya au nzuri?,
Zina faida yoyote ile yenye kuonekana? kama zipo ziweke hapa.



Now jiulize ukoloni umeingia mwaka gani Africa, kabla ya ukoloni na dini kuingia Africa bila shaka tulikuwa tunafuata tamaduni zetu. Sasa weka vitu vitano vikubwa tulivyovifanya ambayo vina faida yoyote mpaka leo kwa Tanzania/Africa na dunia nzima kabla ya ukoloni.

Pia Wewe kama unafuata tamaduni za africa weka faida moja chanya uliyoipata tangu umeanza kufuata tamaduni za kiafrika,
Wewe kama kizazi cha michezo ya kiswahili weka faida uliyoipata utotoni hadi leo hii kutokana na michezo hiyo,
Weka maendeleo ya jamii za kiafrika ambazo bado zinazofuata tamaduni za kiafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…