Swahili_Patriot
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 358
- 831
Ninaamini mchina amemuacha usa karibia kwenye kila idara ikiwepo budget. Sote tunajua kuwa usa ana kambi za kijeshi karibia kwenye kila nchi rafiki (Labda Mimi elimu yangu ndogo, Mchina ana technology gani ya kumzidi USA🇺🇸
Nikiangalia wale mabwana kila sector wapo vizuri.
1) Upande wa ndege hawana mpinzani
2) Mambo ya space science ni hatari
3) Magari ni hatari
4) Micro chips usiseme
5) Computing hawana mpinzani
6) Kwa kilimo ni hatari
7) Kwenye madawa wamo
8) Ujenzi ni hatari
9) Technology ya simu wanatisha
Na mengine mengi tu. Sasa Mimi najiuliza Mchina ana kitu gani cha kuwazidi hawa mabwana.
Upande wa Uchumi kuna gap kubwa mno. USA ana 28.7 trillion USD GDP. Mchina ana 18.5 trillion USD GDP. Gap hiyo ni kubwa.
Anguko LA USA sio Leo wala kesho. Labda miaka Mia mbili Ijayo
Despite recently closing hundreds of bases in Iraq and Afghanistan, the United States still maintains nearly 800 military bases in more than 70 countries and territories abroad—from giant “Little Americas” to small radar facilities. Britain, France and Russia, by contrast, have about 30 foreign bases combined.
By my calculation, maintaining bases and troops overseas cost $85 to $100 billion in fiscal year 2014; the total with bases and troops in warzones is $160 to $200 billion.) https://www.politico.com/magazine/story/2015/06/us-military-bases-around-the-world-119321/
Ukiondoa hilo, USA wanatumia matrilion ya pesa kwenye kufadhili ugaidi sehemu tofauti tofauti duniani. Ila tukienda kwa mchina, karibia asilimia 95 za bajeti yake, zinatumika kuisogeza nchi mbele kiuchumi.
Turudi kwenye uhalisia, tangu huu mwaka uanze, ni nani ametumia bidhaa ya mmarekani?? Kama wapo, basi walitumia sio zaidi ya bidhaa 3, nadra sana. Je bidhaa kutoka China?? Je umeona barabara na treni ngapi zinajengwa Africa na wakandarasi wa USA??? Ila China, wapo nchi zooote za kiafrica kujenga sio reli, sio trains, sio nyumba bali kila kitu complex wao wamo. USA ana budget kubwa sana, ila haimnifaishi. Fuatilia jinsi baadhi ya barabara na mazingira ndani ya USA yalivyochakaa, ila China yapo?? USA mitaa mwingine ni majunk tupu, ila China hamna huo ushenzi. USA amempiga mchina kwenye kutumiwa kwa pesa yake kama means of exchange duniani, ila kwenye kila sekta isipokuwa matumizi ya kijeshi, USA amegalagazwa kama mtoto wa darasa la 7 anayepigana na tyson mwenyewe.