Hivi mkeo unamuachia Tsh. ngapi unapotaka kwenda kazini?

Hivi mkeo unamuachia Tsh. ngapi unapotaka kwenda kazini?

Mimi ninanunua mchele,unga maharage gas na mkaa then kwa siku HAKUNA formula itategemea na siku hiyo nataka kula Nini kwa mfano nyama Basi lazima niache 5000 ambayo NI nusu uzuri tuko wawili TU hatuna mtoto na wife NI mama wa nyumbani Bado sijamuanzishia mradi...Ila kumbuka hapo nakuwa nishaenda naye sokoni weekend kununua vitunguu nusu vya 2000,nyanya za 3000,karoti 1000,hoho 1000, dagaa wa 3000 ,nyanya chungu 1000,..tangawizi za 1000, n.k.....af sometimes na Nazi ya buku muhimu kila siku na asbh ye namwachiaga jero anapenda mihogo au mandazi anakunywa na chai ...so kwa wastani jua NI 2000-5000,,, sometimes inavuka 7000...
Safi sana. Umetisha sana Mtu wa Nguvu. A true Gentleman.🤝🏽
 
We ngoja kuna watu wataoa kwa kusoma coment za wadau tuu huu uzi, enewey usioe kama huna kipato cha uhakika mwanaume ukiacha elfu kumi hakikisha na ingine unaweka akiba ,
 
Kwani katika ile Katiba yetu WABATA hili lipo kweli!!? Mimi sijawahi kuliona.
 
wanawake wengi hampendi kuona wageni wamekuja kwenu hasa ndugu wa waume zenu. Hapo utajinunisha tu ilimradi na kuhakikisha mboga ni marage na kabichi tu week nzima ata kama nyama zimejaa frijini.

Wengine huenda extra mile na kufunga friji na funguo kabisa hadi akirudi yeye kutoka kazini jioni ndio afungue.

Hasara ya aina hii ameipata bro wangu mmoja na mshua mkubwa..Kukanyaga majumbani mwao ni ishu sababu wake waduanzi
Eeh yaani mgeni kaja,mtu anajinunisha plus kulalamika hana pesa,full kisirani yaani wanawake sie Mungu anatuona.

Yaani kuna anko wangu alioa mwanamke yule alikuwa mchoyo,anamaind kula,ukienda kwake ushibe kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una utu mno, hongera! Wengi wakifanikiwa huwa na viburi kwa ndugu waliosota nao. Ila wewe umewakumbatia nduguzo baada ya kufanikiwa, kiasi cha kukaa nao. Huu ni zaidi ya ubinadamu.
Ingawa tunajua kuwa ndugu hawanaga shukrani (watajaa kwako vinono vikiwepo na vikiisha watakimbia), ila kama mungu kakubariki wahudumie tu hasa swala la chakula na makazi.

Nimezipokea pongezi zako mkuu, asante sana.
 
Back
Top Bottom