Hivi mkeo unamuachia Tsh. ngapi unapotaka kwenda kazini?

Hivi mkeo unamuachia Tsh. ngapi unapotaka kwenda kazini?

Uzi tayari!
Kiasi gani cha matumizi unachomwachia mkeo ili kukidhi mahitaji ya kutwa na maandalizi ya chakula cha jioni?

Ambao hatujaoa njooni tujifunze hapa!
Wote tunaenda kazini na wote tunalipwa mshahara na huko kazini hakuna salary ya mwanaume wala wa mwanamke!!! Wote sawa. Hakuna wa kumwachia mwenzake hela ya matumizi kudadeki kila mtu ale kwa jasho lake na bajeti ya matumizu ya nyumbani tunachangia 50% kwa 50%.
 
Na ukiona kwako ni family kubwa na wageni wanapenda kufikia hapo jua ya kwamba mke sio mchoyo,

Hakuna kitu tunajiaribia sisi wanawake kama uchoyo wa chakula,,ukitaka uchukiwe basi kuwa mchoyo aisee hakuna mtu atatamani kuja kwako. Japo hawafuati kula hapo kwako,

wageni/family inabidi ipewe uhuru kwenye chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
wanawake wengi hampendi kuona wageni wamekuja kwenu hasa ndugu wa waume zenu. Hapo utajinunisha tu ilimradi na kuhakikisha mboga ni marage na kabichi tu week nzima ata kama nyama zimejaa frijini.

Wengine huenda extra mile na kufunga friji na funguo kabisa hadi akirudi yeye kutoka kazini jioni ndio afungue.

Hasara ya aina hii ameipata bro wangu mmoja na mshua mkubwa..Kukanyaga majumbani mwao ni ishu sababu wake waduanzi
 
Nyumba inachangamka sana na chakula kinanoga yaani raha sana,

Wakiondoka nyumba inapooza sana,

Mwanzo ilikuwa ngumu sana kuzoea maisha ya family ya wat u wanna tu na kila mmoja akiamka na mishe zake kukutana jioni,mkipika chakula mnaangaliana tu,,

Sent using Jamii Forums mobile app
Raha ya nyumba iwe na watu wengi aisee sio mnakaa kipweke pweke hapanogi yani. Watu wawepo hasa ndugu zenu miksa na watoto waishi vizuri na company za wenzao inajenga bond nzuri mno.
 
Bora hata huyu anaacha buku mbili, kuna wengine hawaachi hata Mia.

Akirudi jioni anataka akute msosi mezani.

Mtasaidiwa sana na vijana wa genge.
Mjengoni kuna kila kitu anzia sukari wese gas na nafaka zote + nyama. Hio buku bee ni kwa ajili ya kubadilishia mboga za majani na dagaa mchele labda😅
 
Back
Top Bottom