Hivi mnaamini haya magari ya kutembelea ya mchina yanayokuja Africa?

Hivi mnaamini haya magari ya kutembelea ya mchina yanayokuja Africa?

Mabasi ya kichina mlisema mabovu, leo yametawala barabarani. Trucks same thing, leo Howo zinatawala. Simu pia ilikuwa hivyo hivyo leo mchina kashika soko la Africa. Ni suala la muda tu.

Magari ya kichina yana bei nafuu na features za kutosha. Kuna gari taa zake za mbele ni projector unawasha unaangalia movie, lakini bei kitonga. Hiyo feature ukiikuta kwenye gari la Mmarekani au Mjerumani, utalipia hadi figo 🤣
Kuna jamaa walijunua FAO wakazipeleka pale Makanya kudump gypsum, wanajuta. Gari haina 5yrs ipo hoi haifai tena. Wakati aliyenunua scania used anadunda nayo.

Mchina kashika soko la Africa sio kwa sababu ya ubora, ila bei, lakinj magari yake sio durable. Juzi naona Marcopolo namba C ya Kilimanjaro Express imesimama wakati Yutong namba D ni kama zinapotea, zimechoka.

Mchina sio mtu, ila kwa Africa atafanya vizuri kwa sababu ya bei.
 
Gari ya nifa , ya mchina haina mda( jokes).😆😆😆 ila kwa voice within me Pascal Mayalla naiona kama takataka na toi la kuchezea watoto wadogo🤔

Wachina kwa kuzalisha vitu kwa ajili ya Afrika ,vyenye ubora unaotakiwa sina imani nao kabisa.

Kama hizi basi ndio bure kabisa, kila siku zinawaka moto, sijui shida ipo wapi?

Xi Jinping
Angalau Niffer ameweza hata kuiagiza toka China na ikashuka Bongo kwa ndege!😄😄😄😄

Wewe Sasa, hata guta la SIDO umeshindwa kununua unajadili ndinga za wenzako! Pumbavu!!!
 
Gari ya nifa , ya mchina haina mda( jokes).😆😆😆 ila kwa voice within me Pascal Mayalla naiona kama takataka na toi la kuchezea watoto wadogo🤔

Wachina kwa kuzalisha vitu kwa ajili ya Afrika ,vyenye ubora unaotakiwa sina imani nao kabisa.

Kama hizi basi ndio bure kabisa, kila siku zinawaka moto, sijui shida ipo wapi?

Xi Jinping
Uko sahihi mchina si kiumbe wa kuaminika nishawah kufanya nao biashara ya bidhaa walichowahi nifanyia nimewakataa mazima.
 
Gari ya nifa , ya mchina haina mda( jokes).😆😆😆 ila kwa voice within me Pascal Mayalla naiona kama takataka na toi la kuchezea watoto wadogo🤔

Wachina kwa kuzalisha vitu kwa ajili ya Afrika ,vyenye ubora unaotakiwa sina imani nao kabisa.

Kama hizi basi ndio bure kabisa, kila siku zinawaka moto, sijui shida ipo wapi?

Xi Jinping
Meku..!Wachina wana uwezo wa kuzalisha bidhaa za ubora wowote ule unaotakiwa, ila kiwango cha ubora kinategemea mambo mawili makuu: pesa anazolipa mfanyabiashara na sheria za nchi husika.
 
1. Mfumo wa "Unacholipia Ndicho Unachopata" (You Get What You Pay For)
Viwanda vya China vinafanya kazi kwa oda. Mfanyabiashara kutoka Afrika akienda China, anapewa machaguo (options) kulingana na bajeti yake:
  • Daraja la Kwanza (Premium): Ubora wa hali ya juu kabisa (kama vile simu za iPhone zote zinatengenezwa China).
  • Daraja la Chini (Low-end): Bidhaa zinazotengenezwa kwa malighafi rahisi ili ziuzwe kwa bei ya chini sana nchini mwetu kwa sababu ya nguvu ndogo ya ununuzi ya wananchi wengi.
Wafanyabiashara wengi wa ndani huchagua kiwango cha chini ili wapate faida kubwa au wauze kwa bei rahisi inayohimilika na wateja wao.

2. Udhaifu wa Udhibiti wa Ubora Mipakani (Standards & Regulation)
Nchi zilizoendelea (kama Marekani au nchi za Ulaya) zina mifumo mikali sana ya kukagua bidhaa kabla hazijaingia sokoni (mfano: viwango vya CE au FDA). Bidhaa yoyote ya China isiyokidhi viwango hivyo inakataliwa mipakani.
Barani Afrika, mamlaka za udhibiti (kama TBS kwa Tanzania au KEBS kwa Kenya) wakati mwingine zinakabiliwa na changamoto za rushwa au ukosefu wa vifaa vya kisasa, hivyo kuruhusu bidhaa hafifu kuingia kirahisi.

3. Bidhaa za Juu za Kichina Zinazofanya Vizuri
Ili kuona kuwa China inaweza kuzalisha vitu bora, angalia makampuni makubwa ya kiteknolojia na miundombinu yanayokubalika kimataifa na yanayotumika Afrika:
  • Simu na Vifaa vya Kielektroniki: Bidhaa za Huawei, Xiaomi, na Oppo zina ubora wa juu sana unaoshindana na makampuni ya Marekani au Korea Kusini.
  • Magari na Mitambo: Makampuni kama BYD (yanayoongoza kwa magari ya umeme duniani kwa sasa) na XCMG (mitambo ya ujenzi) yanazalisha vifaa imara sana.
 
Mkuu, zile bus za mwendokasi, zilianza kazi mwaka 2016 nadhani, na hazijafanyiwa service ya maana, zinapiga safari deile, overloaded, engine nyuma nk, ila mpaka leo, takribani miaka 10, zipo na zinapiga kazi. Majuzi hapa road nimekutana na HOWO truck ni namba C lipo mang'anyu, naamini zipo kadhaa barabarani, sasa namba C official ya mwisho ilitoka 2014 (miaka 12 iliyopita).
Mwendokasi like za mwanzo nyingi zimekufa. Ndio maana kuna kipindi njia ya Kimara kulikuwa na shida sana ya usafiri. Sasa hivi almost fleet yote ni yale mapya namba E. Halafu at least mwendokasi sio kazi ngumu, speed max 40-50kph hakuna milima wala stress kwa gari. Howo kibao namba D zishatupwa. Ukipita pale gerezani kuna yard ya Yepi Merlez hio midude Howo ipo kibao washamalizana nayo. BTW haina maana kuwa zoooote zitakufa mapema pia wengine wanabadili engine na diff.
 
Mwanzo nilikua na mawazo haya siku moja niliikuta GWM pick up mnadani watu wanairuka na bei inashuka nikaaema ngoja niichukue itanisaidia kwa kazi zangu ingawaje inaweza kuwa sio ngumu ngumu daah ile gari baada ya kuikagua vizuri ni Toyota engine na vitu vingine nilivyofika nayo mjini wazala wakaipandia bei jamaa wa kurekebisha minara ya voda mpaka kesho inafanya kazi na mara nyingi ipo site za mbali..

Kisa cha pili nakonunua powertools za CAT wao wanatumia mchina kwa wafanyakazi wote niliipenda Haval H 2 bank walipomalizana nazo nikaomba moja ninunue kabla haijapelekwa mnadani wakaniuzia aisee ile H 2 ni gari kweli camera gari lote mpaka paa la juu speed ipo na balance service yake kwa SA sio gharama kubwa ngoja niwakague TRA ntaileta home..

Pick up za kazi ni Mahindra za kuanzia 2017 kuja mbele hiyo ya 2020 tu single cabin ni rand 100,000 na TRA hawajaiweka kwenye kikokoteo chao nao nawasubiri maana haya ma Ford ranger na Hilux yabaki kwa ajili ya safari ndefu tu mimi ni mbishi nikitumia kitu na kukielewa nimekikagua mno..
 
Ila we jamaa ni kanafki😃
Huyu demu ana Hela za mchezo, asa ndio gari gani ili?
1838.jpg

Ila sina Imani na Mchina, usikute Jetour wamempa kama awatangazie. Maana wako Nyerere Rd.
 
Wengine tunayaamini, kama tunapita madaraja waliojenga, kuvaa kofia, saa, raba, viatu na nguo zao, kutumia household, phones, electronic gadgets, household items, kusafiri kwenye mabasi ya mchina, pikiipiki, NK NK why not the cars made in China?!
 
Back
Top Bottom