Hivi mnaamini haya magari ya kutembelea ya mchina yanayokuja Africa?

Mchina kashika soko la Africa sio kwa sababu ya ubora, ila bei, lakinj magari yake sio durable. Juzi naona Marcopolo namba C ya Kilimanjaro Express imesimama wakati Yutong namba D ni kama zinapotea, zimechoka.
KLM ipo namba A inapiga kazi daily. Si unaona Abood kila baada ya muda mfupi anatoa fleet mpya, hapo asha dispose za zamani kwa wafanyabiashara wa wilayani huko.
 
Mchina kwenye marketing yupo vizuri sana. Hiyo gari Wana advertise ina 600hp lakini kiuhalisia ukiwa barabara utajua mwenyewe namna utakavyoipata.
Kwamba ile Jetour T2 ninazoona mtandaoni na barabara za Tz zina 600hp? Kama G63 sio? Kuna siku natoka Dom jamaa ana pick up ya kichina Foton anakuja ananiletea dharau ha ha ha nilimuonesha kwa vitendo Mjapan na Mchina tofauti. Yeye ana gari mpya mimi nina chuma chakavu chenye 130k lakini aliona cha moto.
 
Ila wewe humu ni kama balozi wa gari za kichina inakuwaje unakuwa skeptical nazo ghafla?
Gari kama gari naikubali. Sana. Ila Niffer anunue naona kama haimake sense.

Imebidi niende kwenye website ya Jetour, moja nimeomba quotation ya T2 na pili, nimeuliza kuhusu financing (mkopo). Maana nilisikia wameingia mkataba na EXIM Bank wanakopesha unalipa kidogo kidogo.

Sasa sijui hii imekaaje. Kwamba unabaki kusaiana na bank (ambayo itakua maumivu sana), au unaiana na Jetour (ambayo sidhani kama wataweza)!

Wakinijibu, nitaona.
 
Sasa sijui hii imekaaje. Kwamba unabaki kusaiana na bank (ambayo itakua maumivu sana), au unaiana na Jetour (ambayo sidhani kama wataweza
Finance ni wewe na bank. Dealer anapewa cash yake then wewe utapambana na bank kwenye interest. Gari ya 120m utainunua kwa 150m na by the time unamaliza mkopo ishachakaa.
 
Mkuu EV za mchina zimeshika soko la europe... Australia zimeshika EVs na gasoline.
Marekani bila kuzipigs marufuku nako tesla angekuwa anapata tabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…