Hii yote ni matokeo ya kuyaacha maagizo ya MUNGU na kushikamana na ajenda ya 50/50,haki za wanawake, wanawake wanaweza na kila aina ya ujinga uliojazwa vichwani mwa wanawake.Ndoa nyingi ila talaka ndio nyingi zaidi!
Unajua Dar es salaam tu kuna madai zaidi ya mia tatu (300) ya talaka kwa kila mwezi tena yakiongozwa na wanawake.
Ofisi ya takwinu inavyosema ndoa zimepungua sio wajinga miaka ya nyuma 2000- 2009 makanisa hasa rc hapa mjini yalikuwa yanatangaza ndoa zisizopungua 20 kila wikiendi ila kwa sasa ndoa 3 tu kutangaza ni mtihani.
Na hii sio Tanzania tu ni worldwide, kuoa sio ujanja tena hasa kwa kizazi hiki
Heshima na hadhi ya watoto wakiume/wanaume imeporwa/imeondolewa,haki ya mamlaka na utawala imeporwa.
Ninadhani huu sio wakati wa kuhoji kwanini vijana/wanaume hawaoi,isipokuwa,swali liwe,ni kwanamna gani vijana/wanaume watapewa/watarudishiwa heshima na hadhi yao.