Hivi mtoto wa kike kama haolewi anapaswa kuendelea kuishi na wazazi mpaka umri gani?

Hivi mtoto wa kike kama haolewi anapaswa kuendelea kuishi na wazazi mpaka umri gani?

Wanaomsema wako sahihi maana ndio nature, viumbe vyote tumeumbwa hivyo kwamba inategemewa kufikia umri fulani uwe umetimiza hatua kadhaa za kuendeleza kizazi, it's biological and natural, ila kwa maisha haya ya leo, imetulazimu twende kinyume na mambo mengi ya asili.

Anapaswa yeye asihangaike nao, apambane kujikwamua kimaisha hususan kwenye kusaka kipato, kama akiweza aongeze hata elimu apate masters na kuendelea kujichimbia, haina ulazima wa kuolewa almradi tu aoelewe, atateseka kwenye ndoa.
Hapa umeandika points tupu.

Lakini majukwaa mengine unaandikaga mavi kishenzi!!
 
Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.

Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasababu mbalimbali.

Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-

1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?

2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?

Kwanini nimeleta uzi huu?

Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mimi Sexless, kungwi la kitaifa.

Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.

Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.
Mtoto kwao hakuna muda maana hapo ndo kwa wazazi wako. Hata ndoa ikivunjika utarudi tu kwenu. Labda baba mtu awe kauzu. Mtu huwezi kulazimisha kuolewa eti muda wa kukaa nyumbani umekwisha, seriously.
 
Hapa umeandika points tupu.

Lakini majukwaa mengine unaandikaga mavi kishenzi!!

Ha ha ha!!! Sio lazima kila kila mmoja aandike unachokitaka wewe, utamu wa mitandao ya kijamii unakua free bila kushikiliwa akili.
 
Back
Top Bottom