Hivi mtoto wa kike kama haolewi anapaswa kuendelea kuishi na wazazi mpaka umri gani?

Hivi mtoto wa kike kama haolewi anapaswa kuendelea kuishi na wazazi mpaka umri gani?

Mmh! Kwann isiwe hata kabla ya kufikiria kubeba ujauzito? Mm nilidhani kuwe na umri tu ukifika mdada aone aibu kuendelea kupishana na babake maliwatoni
Kwa mazingira ya kwetu na uarabuni, mwanamke si mtafutaji bali analetewa; kwa hiyo kuweka umri maalumu kwa mwanamke akajitegemee inakuwa ngumu; ila kiustaarabu, pale mihemko ya mwili itakavyokuwa ikimsumbua sana kuitaji tendo la ndoa, ni busara zaidi akajitegemee ili asiwakere ndugu na jamaa.
Nb: Tendo la ndoa ni hitajila msingi, mtu akilikosa mda mrefu; linaathiri afya ya akili.​
 
Hapana. Wanamshambulia kwa kuendelea kukaa nyumbani at the age of 32. Kwann asiondoke nyumbani kwao akajitegemea? Wala siyo kuolewa ama kazi
Aondoke kwenda wapi kama hana kipato?
 
Kimsingi mwanamke ni kuchungwa nyakati zote za maisha yake.....mwanamke hana ukomo wa kukaa nyumbani........ wazazi Wana wajibu wa kumuhudumia mpaka atakapoolewa na kama Hana mume na wazee hawana uwezo basi kaka zao wanawajibika kumuhudumia dada yao mpaka apate mume

Kaka wa wapi haoo wachache mno wanaohudumia dada zao
 
Kukaa na wazazi ikienda sana mwisho 30 si mtoto wa kike, wala wa kiume.

yaani mkubwa hvo unakaaje kwenu?
tena kwenye nyumba ya baba yako[emoji848]
mwanamke akishabahatika kupata elimu ya juu anajiona me kasoro jinsia.anajiona anajua na anaweza kila kitu...

..mwisho kabisa, kama anataka kuolewa mwambie:
-aache ujuaji

-aache dharau (ajiheshimu yeye na awaheshimu wengne)

-awe myenyekevu (mtu wa kujishusha)

-awe mpole
-asiwe na kiburi.
 
Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.

Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasababu mbalimbali.

Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-

1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?

2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?

Kwanini nimeleta uzi huu?

Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mimi Sexless, kungwi la kitaifa.

Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.

Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.
Kuoa na Kuolewa ni MAJALIWA
 
Bado kidogo ataolewa. Kwa tafiti yangu isiyo rasmi wanawake/wasichana wengi ambao hawakai nyumbani huwa ngumu kuolewa na mara nyingi huishia kuwa madanga na masingo mama labda kama Yuko kikazi mbali na hm vilevile awapo mbali na nyumbani yampasa kuwa na ndugu karibu tofauti na wanaume akiwa nyumbani kuoa inakuwa ngumu sana. Nimemaliza
 
Kuoa na Kuolewa ni MAJALIWA
Hapa hoja ni umri wa miaka 32 kuendelea kukaa nyumbani. Je, ni sahihi? Na kama si sahihi mtoto wa kike anapaswa kuondoka kwao afikishapo miaka mingapi?
 
Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.

Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasababu mbalimbali.

Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-

1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?

2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?

Kwanini nimeleta uzi huu?

Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mimi Sexless, kungwi la kitaifa.

Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.

Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.
Kama wazazi wake hawana shida, hayo makelele ya nje aachane nayo. Yeye aendelee kupambana na maisha yake. Siku hizi kuolewa ni bahati, Pengine angeolewa angekuwa ameashaachika. Aendelee kusubiri wakati wa Mungu ukifika ataolewa, akishindwa kabisa kuvumulia basi azae tu, Mungu atamkuza mtoto wake.
 
Hapa hoja ni umri wa miaka 32 kuendelea kukaa nyumbani. Je, ni sahihi? Na kama si sahihi mtoto wa kike anapaswa kuondoka kwao afikishapo miaka mingapi?
Kwanini ALAZIMISHWE kuondoka nyumbani kwao kwa sababu ya UMRI? Kama hajaweza kuwa na maisha ya kujitegemea yeye mwenye anaweza kukaa kwao mpaka atakapotwaliwa na Mola.
 
Hapana. Hajanituma nimtafutie mchumba. Mada hii ni ya mimi kungwi kutaka kujielimisha namna nzuri ya kutoa ushauri juu ya umri sahihi wa mtoto wa kike kuondoka nyumbani hata kama hajaolewa.
Sawa hajakutumq umtafutie mchumba. Lakini ni bado hajapata. Utakapo mshauri ni vyema pia umpa ushauri kuwa kuna watu wameonyesha nia ya kutaka kuwa na wewe. Nami pia nimejitokeza.
 
Ukitoka chuo tu hupaswi kukaa kwa wazazi tena uwe kijana wa kike ama kiume.
 
Kwanini ALAZIMISHWE kuondoka nyumbani kwao kwa sababu ya UMRI? Kama hajaweza kuwa na maisha ya kujitegemea yeye mwenye anaweza kukaa kwao mpaka atakapotwaliwa na Mola.
Duuh! Mkuu ile habari ya mtu kuwa mtu mzima au mzee kwa mwanamke haipo kabisa? Kama ipo ni vipi anatimiza majukumu ya utu uzima ikiwa ni pamoja na kujitegemea?
 
Kutokana na mimi kuwa miongoni mwa waliokula chumvi nyingi zaidi hapa JF ,nikujulishe kuwa hakuna kikomo cha umri cha mtoto wa kike kuishi kwa wazazi wake kama hajaolewa, kinachopaswa kufanyika ni wazazi kumwezesha aweze kujitegemea.
 
Back
Top Bottom