Hivi mtoto wa kike kama haolewi anapaswa kuendelea kuishi na wazazi mpaka umri gani?

Hivi mtoto wa kike kama haolewi anapaswa kuendelea kuishi na wazazi mpaka umri gani?

Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.

Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasababu mbalimbali.

Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-

1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?

2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?

Kwanini nimeleta uzi huu?

Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mimi Sexless, kungwi la kitaifa.

Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.

Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.
Mama D, njoo huku utusaidie kupata majibu sahihi
 
Vijana wa kileo hatuko tayari kuoa majangili, majambazi na matapeli wa kike.........huko kanda ya ziwa kumeibuka mtindo mbovu sana mwanamke anakubali kuolewa kwa lengo moja la kwenda kuchuma mali za mume.....yaani anakubali ndoa baada ya mwaka mmoja tu anajigeuza anadai talaka na mwisho wa siku anakomaa wagawane mali alizozikuta pasu kwa pasu ......NYINYI WANAWAKE MKAOLEWE NA BABA ZENU AU KAKA ZENU ..
Kumekucha🤣 sasa kwanini ugawane mali na mtu ambae hajaichuma??? Kama kachangia door mats abebe hizo arudi nazo kwao.
 
Ushauri wa mamako hauna maana kwa zama hizi ambapo ndoa siyo Jambo la kutumainiwa ama kutegemewa na mtoto wa kike.

Yaani mtu anaitafuta 40 ashindwe kupambania maisha yake kwa kusubiria kitu asichokuwa na hakika nacho?
Mimi
Nimetoa mfano wangu. Point yangu ya kwamba akatafte kazi mkoani hujaiona?
 
Wadada wengi siku hizi are too selective...
Vigezo vingi mpaka unashangaa huyo mwanaume atakua wa namna gani...mara awe hivi,awe na hiki,watakaa sana nyumbani
 
Mimi
Nimetoa mfano wangu. Point yangu ya kwamba akatafte kazi mkoani hujaiona?
Kwann mkoani mkuu? Kwann asiombe hata mtaji ajiajiri mwenyewe hata mama ntilie lkn atafute sehemu hata jirani na kwao apange na aanze maisha yake binafsi?

Kwann mwanamke aishi kwa kumhofia mtu asiyejulikana (mkwe)?
 
Akakae wapi na kazi hana?
Ni kujipendekeza tu. Watoto wa kiume wa miaka 19 wanatoka mikoa ya mbali na kuja mjini hawana ndugu wala nn mwishowe wanatoboa.

Sasa Kwann huyu asiombe kuishi peke yake na akaanzisha genge la mbogamboga?
 
Akakae wapi na kazi hana?
Ni kujipendekeza tu. Watoto wa kiume wa miaka 19 wanatoka mikoa ya mbali na kuja mjini hawana ndugu wala nn mwishowe wanatoboa.

Sasa Kwann huyu asiombe kuishi peke yake na akaanzisha genge la mbogamboga
 
mwanamke ni kiumbe dhaifu ambaye anapaswa kuchungwa.....na wachungi ni baba, mume au kaka.....
Mwanamke ni kiumbe dhaifu dhidi ya nn? Na anachungwa ili iwe nini? Naona kama huu mtazamo umepitwa na wakati sana.

Unamlinda mwanamke asishawishiwe na mwanaume enzi hizi za kidijitali?
 
Ni kujipendekeza tu. Watoto wa kiume wa miaka 19 wanatoka mikoa ya mbali na kuja mjini hawana ndugu wala nn mwishowe wanatoboa.

Sasa Kwann huyu asiombe kuishi peke yake na akaanzisha genge la mbogamboga
Kuna tofaiti kubwa Sana Kati ya mtoto wa kike na mtoto wa kiume hata wewe unaelewa
 
Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lakini hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashangazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.
Mtoto hakui kwa wazazi, siku meza ikipinduka watamhitaji kuwasaidia maana hawatakuwa na uwezo tena wa kujihudumia
 
Kuna tofaiti kubwa Sana Kati ya mtoto wa kike na mtoto wa kiume hata wewe unaelewa
Ndiyo nataka kujua Kama hizi tofauti zina maana tena ktk zama hizi za 59/50? Au tunapambana na kitu kilichopitwa na wakati?
 
Mtoto hakui kwa wazazi, siku meza ikipinduka watamhitaji kuwasaidia maana hawatakuwa na uwezo tena wa kujihudumia
Kwani kusaidia ni mpk uwe unaishi nyumbani maisha yote? Watu wako uUaya na wanasaidia wazee huku Afrika
 
Tujifunze wakati wa MUNGU ni sahihi.
Si vyema kulazimisha au kusimanga binti juu ya ndoa, hali ni mbaya huko nje.wanaume hawataki kuoa na majukumu.

Tujengee mabinti hawa uwezo wa kujikwamua kiuchumi kwanza,kuolewa watadecide baadae wenyewe.
Mambo yalichange, wanaume wa kuoa ni wa kuhesabu.

Sio wote ni husband material.
Mabinti wawezeshwe na wapewe muda.
 
Kwenye mpira timu ikishafungwa tunashauri wasipaki basi wafunguke tu hawana cha kupoteza.Huyo hana cha kupoteza ATOKE tu akasake maisha.Kuanzia miaka 30 mwanamke anatakiwa apeleke stress zake mbali na wazazi
 
hali ni mbaya huko nje.wanaume hawataki kuoa na majukumu.
Kwahiyo ndiyoashindwe kujitegemea? Hujasikia kitu kinaitwa usawa wa kijinsia? Sasa inakuwaje mtu kakaa nyumbani karibia miaka 40 hajishughulishi anasubiri mwanaume?
 
Kwann mkoani mkuu? Kwann asiombe hata mtaji ajiajiri mwenyewe hata mama ntilie lkn atafute sehemu hata jirani na kwao apange na aanze maisha yake binafsi?

Kwann mwanamke aishi kwa kumhofia mtu asiyejulikana (mkwe)?
Duh. Narudia tena. Mimi
Nimekupa mfano wangu sijalazimisha huyo mtu afanya hivyo.

Alafu kama ushauri wa kumpa unao naona ni sawa pia. Sijasema akapange kwasababu ya wakwe. Nimesema abaki kwao ajishughulishe awe productive au atafute kazi hata mkoani ajitafute
 
Kwenye mpira timu ikishafungwa tunashauri wasipaki basi wafunguke tu hawana cha kupoteza.Huyo hana cha kupoteza ATOKE tu akasake maisha.Kuanzia miaka 30 mwanamke anatakiwa apeleke stress zake mbali na wazazi
Why atoke kwa wazazi?unless hujawa parent,unawezaje ruhusu mwanao akahangaike huko nje na Una nyumba.
Aseee hilo jambo ni ngumu Sana.
 
Why atoke kwa wazazi?unless hujawa parent,unawezaje ruhusu mwanao akahangaike huko nje na Una nyumba.
Aseee hilo jambo ni ngumu Sana.
Kushughulisha akili ni kuhangaika?Nyie si mnasema wanawake ni JESHI kubwa?Mwanajeshi anaogopaje kujitegemea?
 
Kwahiyo ndiyoashindwe kujitegemea? Hujasikia kitu kinaitwa usawa wa kijinsia? Sasa inakuwaje mtu kakaa nyumbani karibia miaka 40 hajishughulishi anasubiri mwanaume?
Kwani wanaume hakuna wanaokaa hadi wanagonga 40?
It's raining everywhere sio kwa wa kike tu,na tena boys wengi ndio wamekua useless kujidai wana mamlaka ya kila kitu home.
Wakajitegemee wakiona wanataka kufanya hivyo ila si kufukuzwa au kwa kuwatupia lugha za kuudhi.
 
Back
Top Bottom