Kwa mila na tamaduni zilizokuwa zimezoeleka huko nyuma ilikuwa kwamba mtoto wa kike ataondoka kwa wazazi wake kwa kuolewa.
Kwa miaka ya karibuni mifumo na taratibu za maisha zimegeuka kabisa. Idadi kubwa ya watoto wa kike hawaolewi kwasabb mbalimbali.
Kufuatia mabadiliko haya ndiyo sababu ninakuja kwenu wanaJF na maswali yangu haya:-
1. Kwakuwa kuolewa ni nadra sana siku hizi, je, mtoto wa kike azeekee kwa wazazi wake?
2. Kama jibu la swali la kwanza hapo juu ni HAPANA, je, ni umri upi sahihi wa mtoto wa kike (asiyeolewa) kuondoka kwa wazazi wake na kwenda kujitegemea?
Kwann nimeleta uzi huu?
Kuna mdada mmoja kaja kuniomba ushauri mm
Sexless, kungwi la kitaifa.
Anasema ana miaka 32 (msomi wa chuko kikuu) hajabahatika kuolewa wala hajapata kazi. Bado yupo kwa wazazi lkn hivi sasa anatukanwa na majirani, makaka na mashngazi. Wazazi wake hawana shida naye kabisaaa, wako peace kabisa.
Tutoe ushauri utakaosaidia wadada wote nchini wenye changamoto kama ya huyu mteja wangu.