Hivi mtu kujidai haamini uwepo wa Mungu, halafu hapo hapo anaamini dini flani, hii inaitwaje?

Hivi mtu kujidai haamini uwepo wa Mungu, halafu hapo hapo anaamini dini flani, hii inaitwaje?

Hahaha hata kwenye Movie hamuwezi kuwa ma sterling wote, kila mmoja nan ushiriki wake tofauti, na hakuna aliye bora zaidi ya mwenzake kwa sababu tu ya nafasi anayoshiriki.

Dunia hii sote humu hatujui vyanzo vyetu zaidi ya kufahamu tumezaliwa na wazazi wetu walizaliwa na inaendelea hivyo. Hizo social ties tulizo nazo hazitufanyi tuwe bora kuliko wengine, kama unaamini amini hivyo hivyo na asiye amini sawa na wewe naye awe huru kufanya kama wewe ulivyo huru.

Kuhukumiana imekuwa kawaida sana duniani humu, tuishi kwa amani kila mtu amzoee na amvumilie mwenzake kwa alivyo na ayatendayo.

Kama wewe mrefu basi shukuru, ila usimuone mfupi kwamba hajakamilika. Hakuna standard, hizo norms zote tumejiwekea tu, hivyo mtu kuwa nje ya normal yako haikufanyi umuone siyo mkamilifu.

Wenye dini na wasiokuwa nazo wote binadamu, tuache ku judge wenzetu. Hawakuchukulii space yako na hawakufanyi usikamilike, hivyo ishi ulivyo, na uwaache walivyo.
 
Back
Top Bottom