Hivi mtu unafelije somo la hesabu? Zero brain kabisa wanafunzi wa siku hizi

Hivi mtu unafelije somo la hesabu? Zero brain kabisa wanafunzi wa siku hizi

Status
Not open for further replies.

Rosemin

Member
Joined
May 21, 2023
Posts
70
Reaction score
532
JE HOFU YA MITIHANI NA MADAI YA UGUMU WA SOMO LA HISABATI NDIYO SABABU YA KUFELI KWA NUSU YA WATAHINIWA MWAKA HUU? Somo la Hisabati limeendelea kuwa pasua kichwa nchini, ambapo katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu, zaidi ya nusu ya watahiniwa wamepata ufaulu D ambao hauridhishi.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya wanahabari katika ofisi za Baraza hilo, jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta, Dkt. Said Mohamed amesema mbali na matokeo hayo ufaulu wa somo la Hesabu umeshuka kwa asilimia 4.46 ikilinganishwa na mwaka jana.

#Azammedia ikizungumza na baadhi ya wahitimu na walimu kwa nyakati tofauti wametaja miongoni mwa sababu za hofu ya mitihani na baadhi kutojiandaa vyema kwaajili ya mitihani hiyo kuwa sehemu iliyochangia matokeo hayo.

Aidha kwa upande wa walimu, wamesema bado wanafunzi wamejengewa hofu na uoga kuhusu somo la Hisabati kuwa ni gumu na kupelekea kushindwa kufanya vizuri.

Imeandaliwa na kuhaririwa na @official_jennifersumi

#watahiniwa #barazalamitihani #somolahisabati #walimu
 
Wakati nasoma nilikuwa mweupe kwenye somo hilo Mungu ni mwema kumbe kwenye kuhesabu idadi ya noti mtaani hali-apply.

Jamaa yangu mmoja alikuwa ananifariji kusema ”watu wote tujue hesabu tunataka kugundua nini kipya dunia hii?”
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom