Hivi Mungu alisema ukitaka kuandika jina lake uanze na herufi kubwa?

Hivi Mungu alisema ukitaka kuandika jina lake uanze na herufi kubwa?

Mungu ni mkuu huwezi kumuandika kwa herufi ndogo, huko ni kukosa adabu na heshima kwa muumba mwenyezi MUNGU aliyeumba mbingu na dunia ni BWANA wa majeshi
 
Kumekucha wana Jf,

Najiuliza tu hivi mungu alisema wapi ukitaka kuandika jina lake uweke herufi kubwa mfano Mungu ukiandika mungu utakosolewa vibaya mno mungu anatetewa na binadamu kuliko anavyojitetea yeye
Ni kanuni ya uandishi,majina huandikwa kwa herufi kubwa,hata wewe I'd yako,umeandika kwa M kubwa hukuandika kwa m ndogo.Rudi shule ukajifunze up ya,ikiwa hujui hata jina linaandikwa vipi.
 
Kumekucha wana Jf,

Najiuliza tu hivi mungu alisema wapi ukitaka kuandika jina lake uweke herufi kubwa mfano Mungu ukiandika mungu utakosolewa vibaya mno mungu anatetewa na binadamu kuliko anavyojitetea yeye
Kuna tofauti kati ya mungu na Mungu. So kila ukitaja lazima ujue unamaanisha nini.

Mungu; inamaanisha Mungu wa Mbinguni, aliyeziumba mbingu na nchi.
mungu; inamaanisha muungu/mzimu au kitu kingine kinachoabudiwa na watu au jamii flani pekee.

Hivi katika uandishi, ili kutofautisha Mungu muumba wa mbingu na nchi, na miungu mingine, ni lazima iandikwe kwa kutofautisha herufi, ili msomaji aelewe anayeongelewa ni nani hasa.
 
Kumekucha wana Jf,

Najiuliza tu hivi Mungu alisema wapi ukitaka kuandika jina lake uweke herufi kubwa mfano Mungu ukiandika mungu utakosolewa vibaya mno mungu anatetewa na binadamu kuliko anavyojitetea yeye
samia suluhu unaandika vipi?
 
Herufi kubwa ni Mungu wa kweli na herufi ndogo ni Mungu wa michongo. Ni mwanzo wa vyote ndio maana anapewa heshima ya herufi kubwa.
 
Kikanuni hasa inatakiwa Jina lake liandikwe kwa herufi kubwa tupu.

Kama hapa.

Kutoka 3:14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO: akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli: MIMI NIKO amenituma kwenu.
 
Kumekucha wana Jf,

Najiuliza tu hivi Mungu alisema wapi ukitaka kuandika jina lake uweke herufi kubwa mfano Mungu ukiandika mungu utakosolewa vibaya mno mungu anatetewa na binadamu kuliko anavyojitetea yeye
Achia mbali Mungu kama kasema hivyo au la..!! Wewe wakati unajifunza mwandiko, hukufundishwa kuwa jina linaanza na herufi kubwa..!!??
 
Back
Top Bottom