Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Kwa mujibu wa Biblia, Ni shetani ndiye aliyemshawishi Adam ila hakuwa na mamlaka wala umiliki wa dunia na vijazavyo. Shetani alipata baada ya anguko la Adam hata hivyo hana umiliki wala maamuzi kwa wachaMungu

Ni wapi tunaweza kusoma kuwa shetani alimshawishi Adamu?
 
Sasa, kama imani inaweza kukufanya ujione unaweza kutembea juu ya maji ukafa, au ikakufanya ujione unaweza kuruka kutoka ghorofani kwenda kwenye Simtank usife, lakini ukafa, hapo tunaona imani si kigezo kizuri cha kufikia ukweli.

Unaweza kuamini kitu ni kweli, halafu imani yako isifanye kitu kile kuwa kweli.

Kwa nini tunapenda kuendekeza imani, badala ya uchambuzi wa kimantiki wenye mashiko zaidi ya imani tu?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787] maswali ya mashanbulizi[emoji16][emoji16]
 
Hakuna Cha mtiani Wala nini,
Kujichanganya ndio tumekalia.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787] maswali ya mashanbulizi[emoji16][emoji16]
Hawa watu wanaoleta maneno ambayo hayana definition inabidi tuwakabe kama wezi wa Tandale.

"Positive Energy" maana yake nini?

Nikimchamba vibaya sana malaya mchafu anayeeneza UKIMWI, kwa maneno ya ukweli, akawa njia panda ya kuweza kujiua kwa aibu au kupata elimu na kuachana na umalaya akafanya kazi nzuri isiyoeneza UKIMWI hiyo ni positive energy kwa sababu inaweza kumsaidia aache kueneza UKIMWI au ni negative energy kwa sababu nimempa ukweli bila kituo na anaweza kujiua kwa maneno yangu?

Unapimaje hapo?
 
Hiyo dhana kuwa Mungu asingekuwa na huruma angeshatuangamiza umeijenga kwa misingi ipi?

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu Mungu amekuwa akiangamiza kila wakati inapotokea uasi wa binadamu umeshamiri, alifanya hivyo enzi za gharika kuu na enzi za moto wa Sodoma.

Kama tunaweza kujua interval ya maangamizi hayo makuu mawili ni miaka mingapi, na miaka mingapi imepita tangu angamizo la mwisho hadi leo….. basi tunaweza kubashiri ikiwa huruma yake mpya ni ya kweli au pengine uasi haujazidi kipimo chake au kama bado anatuvutia kasi tu.
 
Suala la imani ni suala binafsi. Huwezi kulitenganisha na binadamu kwa sasa. Labda sayansi ije na majibu ambayo yamesababisha imani ikawepo. Kinyume na hapo ni kuheshimu tu imani za watu ilimradi ipo ndani ya sheria za nchi. Hao wanaokufa kwa kujirusha ghorofani na wengine kufia majini kwa jina la imani walivunja sheria za nchi ni vile hawakukamatwa kabla hawajafa.

Suala la kuwa makini nalo ni kutumia logic kuuliza maswali ya kiimani na ukataka majibu ya logic kutoka kwa mwamini. Hapo tu ndipo ambapo huwa sikuelewi.

Yaani unataka mtoto anayeamini kuwa baba yake ndo mwenye nguvu kuliko wababa wote atumie logic na kuachana na imani yake huku ukitegemea yeye achukue hayo maamuzi baada ya kushindwa kuthibitishia kuwa baba yake ana hizo nguvu.

Ukitaka kidogo akuelewe logic yako Mchukue baba yake, mtandike viboko mbele yake halafu mwambie unaona, baba yako hana nguvu kuliko wababa wote na sio kutaka yeye ashindwe kukuthibitishia halafu ahitimishe kuwa baba yake hana nguvu.
 
Hiyo ni positive Energy but at the sametime ni Negative Energy
Huruma ya Mungu iko wapi ikiwa kamuacha Ibilisi atawale?
 
Thibitisha kwanza kwamba IBILISI yupo [emoji23] nipuuzwe natania tu
Ibilisi na Mungu ni mambo ya imani. Imani ni hakika ya mambo yasiyoonekana. Sasa kutaka mtu athibitishe mambo yasiyoonekana sidhani kama ni sahihi na kama akiweza basi hiyo siyo imani tena
 
Umenipa mtihani mkubwa[emoji16]

Uyo bwana ndio angejibu hili swali
Kutokana na uelewa wake Wama energy [emoji16][emoji16]
Mimi naona umetumia zote na zimetusaidia
 
Huwezi thibitisha mambo ya iman kwani imani ni hakika ya mambo yasiyoonekana. Kama ukiweza kuthibitisha basi siyo imani tena bali ni kujua. Sentesnsi sahihi ni kuamini Ibilisi /Mungu yupo na siyo kujua ibilisi /Mungu yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…