Kwanza kabisa, kutomtambua Mungu si imani, ni kukosa imani.
Ukisema kutomtambua Mungu ni imani, ni sawa na kusema kunyoa kipara ni mtindo wa kusuka nywele.
Chanzo chq huyo unayemuita binadamu na huu ulimwengu mimi sikijui, na sijawahi kusema nakijua. Lakini najua si Mungu, kwa sababu Mungu hayupo.
Naweza kujua jibu fulani si sahihi, hata bila kujua jibu sahihi ni lipi.
Mathalan, ikiwa mama mzazi wa mtu ni lazima awe mkubwa kuliko huyo mtu, ukinionesha mtu wa miaka 30, halafu ukaniambia mtu huyu wa miaka 30 mama yake mzazi ni binti mchanga wa miezi 6 kwa wakati huohuo, nitajua binti mchanga huyo si mama yake mzazi mtu mwenye miaka 30.
Hata bila ya kujua mama yake mzazi mtu huyu mwenye miaka 30 ni nani.
Naweza kujua jibu fulani si sahihi, hata bila kujua jibu sahihi ni lipi.