Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

😂😂😂😂 eti angeamua kukomaa nae huko huko mbinguni! JF ina watu jamani!
 
Ibilisi kama upo jitokeze, pitia uzi wa kijana wako riki boy wa kula matunda kimasihara. mana la eden moja limeleta shida tumalize mjadala ukileta mlejesho
 
Umeeleza vizuri

Uzuri wa dini ni yetu ya kiislamu ni kwamba katika kuhoji mambo ya mungu kumewekwa mipaka, ambayo inaafikiana na akili.

Watu wanajiuliza kwanini mwenyezimungu amefanya hivi, au amesema hivi?

Sasa shida inaanzia pale mtu anapobuni majibu yake mwenyewe kutoka kichwani kwake, kuzungumzia asilolijua.

Allah subhaanahu wataa'la ameawatuma wajumbe(mitume), hao ndio waliotumbia kuhusu yeye na tukawaamini, sasa inakuwaje unapokuwa na swali kuhusu Allah, majibu yasiyoke kwa mtume ambaye ndiye aliyetukhabarisha habari zake, maana yeye ndiye anayejua zaidi.
(Hakuna tunachojua kuhusu Allah ila kile alichotukharisha mtume)

Sasa mtu anajiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe!!!
 
Wakati huo wewe ulishindwa kupambana na nyoka huyo alafu unataka watoto wapambane naye.
hata wakifa nitazaa wengine nikifa Mimi ikining'ata wao watahangaika na hilo ndo fumbo la Imani enendeni kwa amani

Kama hujapata amani hakikisha unarudi jumapili ijayo
 
Hata mimi ninahisi inshu za shetani na Mungu ni blaaa blaaa tupu
Pole, hujanielewa, mimi nilikusudia kumuigiza "imitate" mpingaji mmoja hapa JF, na si kwamba nilichokuwa nimeandika nilikuwa namaamisha, na ndo maana kwenye hiyo comment baada ya emoji ya kicheko niliandika 'nipuuzwe' nilikuwa 'natania tu'

Suala la wewe unahisi ni BLAH BLAH hilo ni wewe mwenyewe naomba usininasibishie na mimi, naheshimu hisia zako

Upande wa pili wa shilingi: mimi naamini juu ya uwepo wa SUPREME BEING kwa 100%, achilia mbali jaribio la wanasayansi walipo-calculate probability ya uwepo wake na kupata 60+%
 
Kiranga:vip kwa uelewa wako unafikili Dunia na binadamu na huu Ulimwengu ilitengenezwa na nani kama sio Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwanini umekubali kuzaliwa?
alafu siku ya kiama unapigwa moto na uyo ibilisi,wengine hatumjui hata anafananaje.kwa kweli hao kina adam angemalizana nao uko eden sio kutuuzia kesi yao ambao hatukuepo
 
Past human life experiences inaweza kuwa ndiyo mwanzo wa biblia .Kwa mfano unaposema usizini,nafikili waliangalia kwanza maana ya tendo la kuzini ni nini,Je matokeo ya kuzini ni yapi?Kukataza kuzini kwenye jamii ni kulinda jamii kimaadili,hasara za kuzini ni kupata magonjwa ya zinaa,kupata watoto nje ya ndoa na hatimae kukosa malezi na ndio wanageuka kuwa wezi,makahaba ,wazinzi na wahuni, kwa kifupi amri za Mungu zilitokea kutokana na binadamu kustalabika kwa kuwa na serikali zao tunaweza kusema amri za Mungu ni KATIBA ya Kuitawala jamii ya kale.

Baada ya hiyo hoja naomba uniambie he binadamu na huu Ulimwengu je chanzo chake ni kipi?Mimi siwezi kupinga hoja yako ya kukataa kwamba Mungu hayupo upo sahihi kabisa kwa Imani na msimamo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga:vip kwa uelewa wako unafikili Dunia na binadamu na huu Ulimwengu ilitengenezwa na nani kama sio Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini swali liwe "nani"?

Huoni kwamba swali lako lina bias tayari?

Tumekuta jani la muembe mlangoni.

Hatujui limefikaje.

Hatujui kama limeletwa na upepo, muuza maembe, watoto wa shule, na kadhalika.

Wewe unaanza kuuliza, Mmasai gani kaleta jani la muembe hapa mlangoni?

Unajuaje kuwa ni Mmasai?
 
Ok sawa una hoja nzuri Sana na Mimi sikupingi kwa Imani yako kuhusu kutomtambua Mungu naomba unisaidie chanzo Cha binadamu na huu Ulimwengu .Una hoja nzuri zenye facts kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa, kutomtambua Mungu si imani, ni kukosa imani.

Ukisema kutomtambua Mungu ni imani, ni sawa na kusema kunyoa kipara ni mtindo wa kusuka nywele.

Chanzo cha huyo unayemuita binadamu na huu ulimwengu mimi sikijui, na sijawahi kusema nakijua. Lakini najua si Mungu, kwa sababu Mungu hayupo.

Naweza kujua jibu fulani si sahihi, hata bila kujua jibu sahihi ni lipi.

Mathalan, ikiwa mama mzazi wa mtu ni lazima awe mkubwa kuliko huyo mtu, ukinionesha mtu wa miaka 30, halafu ukaniambia mtu huyu wa miaka 30 mama yake mzazi ni binti mchanga wa miezi 6 kwa wakati huohuo, nitajua binti mchanga huyo si mama yake mzazi mtu mwenye miaka 30.

Hata bila ya kujua mama yake mzazi mtu huyu mwenye miaka 30 ni nani.

Naweza kujua jibu fulani si sahihi, hata bila kujua jibu sahihi ni lipi.
 
Nashukuru sana kwa ufafanuzi wako kwamba Mungu hayupo naheshimu mawazo yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtizamo wangu na hekima yangu ni kwamba hii uliyoandika hapa sidhani kama unamuongelea Mungu mmoja ambaye anajua kila kitu na kwa hesabu zake na maarifa yake nadhani unaongelea mungu ambaye ni moja kati ya miungu mingi ya kufikirika na wanadamu na IBILIS unaemuongelea hapa ni yule yule wa kwenye series za kizungu na kinaijeria ambaye hayupo peke yake ana ndugu zake na wake zake na mademu zake na watoto wake na maradhi yake al muhimu Mungu unaemzungumzia wewe hapa ni wale waigizaji wa filamu za kingereza na kijapani lakini sio Mungu wa Adam na Muhamad au Mungu wa Mussa na Harun au Mungu wa Yakobo na Isaya mi naona unamuongelea Mungu wa Supernatural,Vampire Diaries na Spartacus kama ni hao nitafanya quote nyingine lakini kama ni Mungu huyu huyu ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa hana mshirika anafanya atakalo na afanyi atakalo mi nadhani urudie THREAD mkuu na headline yake iwe MIUNGU YA MOVIES.
Usinielewe vibaya.

Rakims
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…