Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

umeandika kwa uchungu sana
 
Ibilisi na team yake wapo, na anapatikana na ukihitaji kumwona anaonekana...

Ni maamuzi yako tu..
 
Ibilisi na team yake wapo, na anapatikana na ukihitaji kumwona anaonekana...

Ni maamuzi yako tu..
Unajuaje hayo uliyoandika ni kweli na si hadithi unazojipigia mwenyewe tu?
 
Huko juu tunaambiwa mkono ulichezwa na dakika za mwisho kabisa zilionesha shetani anaenda ku win ile battle Lakini plan B aliyokuja nayo Mungu ndio iliyokuja kubadilisha mchezo mzima.
Huwezi Ibilisi aliumbwa na Mungu mwingine mwenye nguvu ndio maana anasumbua sana.
 

Alitoa msamaha kwa damu ya Yesu Kristo
 

Ye si ndio Mungu mwenyewe jamani au
 

PERFECT
 
Tatzo linakuja pale ambapo biblia ikiwa ni kitabu cha story na wala hakina ukwel itakuaje?! Nani anaweza kututhibishia kama biblia ni kitabu kama kinavyo aminiwa?
 
Kuna wanamantiki wengi pia wameainisha Mungu yupo.
Asante.

Ila, haya si mawazo yangu tu.

Ni mawazo ya kimantiki na yameainishwa hivyo na wanamantiki wengi tu.
 
Kuna wanamantiki wengi pia wameainisha Mungu yupo.
Kwa mantiki gani?

Mimi nimesoma mantiki zote muhimu za kujadili Mungu, zinazotetea uwepo wa Mungu na zinazopinga uwepo wa Mungu.

Soma"Philosophy of Religion: An Anthology"

Nakiambatanisha hapa kwa watakaopenda kusoma.

Angalia "Part Three: The Problem of Evil", page 143. Soma kwa makini.

Hapa ndipo nimepata kuanza kupingia uwepo wa Mungu miaka zaidi ya 26 iliyopita..
 

Attachments

Hakuna Ibilisi duniani. All supernatural powers are equal, the difference between them is how each supernatural power operate in the spiritual & physical world.
 
Mtoa mada umeandika mashudu tu.

Ipo hivi.

Iblis sio malaika, hakuwahi kuwa malaika na hakuwahi kuwashawishi malaika walete uasi mbinguni.

Iblis ni jini, bimaana asili yake imetokana na moto ili hali binadamu asili yake ni udongo. Malaika wao asili yao ni Nuru na ni viumbe ambavyo havimuasi Mungu bali vinafanya yale waliyoamrishwa tu na havina uwezo wa kupinga kama ilivyo kwa majini na wanadamu.

Majini na wanadamu ndio viumbe pekee vilivyopendelewa na Mungu kwa kupewa free will ( uwezo wa kuamua kutenda ama kutokutenda), Majini na wanadamu ndio viumbe pekee vinavyoweza kuasi ama kutii amri za Mungu. Hii free will tuliyopewa na Mungu ni amanah ambayo tumekabidhiwa kuwa iwapo tutamuamini Mungu na kisha kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake basi pasi na shaka tutalipwa malipo mazuri (kuzawadiwa Pepo/paradise) na iwapo hii amanah hatutaitunza na kuamua kutokumuamini Mungu na kufanya yale aliyotuamrisha basi tutakutana na adhabu chungu ya moto wa jahannam. Case closed...hili agano lilishafanyika baina yetu na Mungu.

Viumbe vingine vyote kuanzia milima,mbingu,bahari na ardhi vilikataa kuibeba hii amanah kwa kuelewa uzito wa adhabu ya Mungu iwapo vitakengeuka, vyenyewe viliamua kutii moja kwa moja ila mwanadamu alikubali kuichukua hiyo amanah licha ya kuwa ni kiumbe mdhaifu sana na mwenye kujidhulumu nafsi yake na pia ni mjinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…