Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Kitendo cha Mungu kumtupa Ibilisi duniani ni kitendo cha uonevu mkubwa sana kwa binadamu.

Ibilisi sio levo za binadamu ni levo ya Mungu maana yake Mungu yeye angekomaa naye Ibilisi hukohuko mbinguni mpaka kieleweke. Kutuletea Ibilisi huku duniani ni kutuonea tu maana hatuna uwezo wowote wa kupambana naye.

Kama Ibilisi aliweza kupigana vita kuu mbinguni akiwa na malaika wake sasa binadamu ataweza kweli kupambana na kiumbe kama hiki?

Kiumbe ambacho kiliweza kupambana na malaika wa Mungu na kikafanikiwa kuwashawishi baadhi ya malaika kwenye vita kuu mbinguni na wakaasi sasa wewe binadamu utaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Kama mbinguni tu Ibilisi alisumbua sana ambako ndiyo kuna Mungu na malaika huku duniani tutamuweza kweli?

Kama Ibilisi anauwezo wa kuingilia mipango ya Mungu na kuiharibu kama ule wa bustani ya Edeni na Mungu hamfanyi chochote anaishia tu kuwapa adhabu zisizo na maana yoyote Adam na Hawa. Hiki kiumbe sisi binadamu tutakiweza kweli?

Ilifikia hatua Mungu mwenyewe aliamua kumtoa kafara mwanaye wa pekee( Yesu) ili aweze kupambana na Ibilisi ila mission ikabuma. Sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Hivi unajua kama Ibilisi anaongea na Mungu moja kwa moja? Maana yake Mungu na Ibilisi huwa wanaonana. Unajua mazungumzo ya Mungu na Ibilisi kuhusu Ayubu? Sasa sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi anayeweza kuongea na Mungu moja kwa moja?

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani?
Hapa binadamu tumeonewa sana.

Jukumu la kupambana na Ibilisi ni jukumu la Mungu mwenyewe na sio la binadamu hivyo Mungu amtoe Ibilisi duniani na akaishi naye mbinguni sisi huku hatumuwezi.

Ndio maana imekuwa ni kawaida tu kumkuta mtu ni mfia dini haswa ila ni mzinifu,muongo,muuaji,mchawi,tapeli,mwizi, mnafiki n.k.

Nani kakudanganya kuna binadamu anaweza kupambana na Ibilisi?
umeandika kwa uchungu sana
 
Hizo habari za Mungu na Ibilisi kuwepo ni hadithi za kutunga za watu tu.

Ndiyo maana mpaka leo hakuna mtu aliyethibitisha uwapo wa Mungu wala Ibilisi.

Ndiyo maana maelezo ya kuwapo Mungu yana contradictions nyingi sana ambazo hazijatatuliwa mpaka leo.
Ibilisi na team yake wapo, na anapatikana na ukihitaji kumwona anaonekana...

Ni maamuzi yako tu..
 
Ibilisi na team yake wapo, na anapatikana na ukihitaji kumwona anaonekana...

Ni maamuzi yako tu..
Unajuaje hayo uliyoandika ni kweli na si hadithi unazojipigia mwenyewe tu?
 
Huko juu tunaambiwa mkono ulichezwa na dakika za mwisho kabisa zilionesha shetani anaenda ku win ile battle Lakini plan B aliyokuja nayo Mungu ndio iliyokuja kubadilisha mchezo mzima.
Huwezi Ibilisi aliumbwa na Mungu mwingine mwenye nguvu ndio maana anasumbua sana.
 
Mambo yalianza kuharibika pale bustanini ambapo badala ya Mungu kutoa msamaha kwa adam na ev. Yeye akawamiminia laana.

Cha kwanza aliweka uadui kati ya mwanadamu na shetani

Pili akamwambia binadamu atakula kwa jasho atazaa kwa uchungu na hakika atakufa.

angesamehe kama mwanae anavyo tushauri tusamehe saba mara sabini Tusimge fika huku.

Alitoa msamaha kwa damu ya Yesu Kristo
 
Mambo yalianza kuharibika pale bustanini ambapo badala ya Mungu kutoa msamaha kwa adam na ev. Yeye akawamiminia laana.

Cha kwanza aliweka uadui kati ya mwanadamu na shetani

Pili akamwambia binadamu atakula kwa jasho atazaa kwa uchungu na hakika atakufa.

angesamehe kama mwanae anavyo tushauri tusamehe saba mara sabini Tusimge fika huku.

Ye si ndio Mungu mwenyewe jamani au
 
Lazima tuwe na Mipaka katika Matamshi yetu...

Naomba kwanza kuweka kumbukumbu sawa; I was born and raised in a conservative Christian family until I was 20 in my first year Chuo kikuu baada ya kukutana na Mtu ambaye baadaye amekuja kuwa the love of my life NDIPO NILIPOAMUA KUBADILI DINI ingawa am not that much practicing anyway but I hope Mungu atanisaidia:

Naomba sasa kulizungumza hili in ISLAMIC perspective kwa ajili ya kushare uzoefu...

According to the aforementioned perspective HAYAKUWA MAISHA HAYA YA DUNIA ILA NI SEHEMU YA MTIHANI kwa Mwanadamu kutoka kwa Mola wake Mlezi. Baada ya Kuumbwa, kupewa akili na miongozo ya namna ya kuishi hapa duniani MWANADAMU AMEWEKEWA MITIHANI ILI KUMPIMA NI YUPO ANA MKHOFU MOLA MLEZI NA KUFUATA MIONGOZO YAKE NA NANI ATAKENGEUKA NA KUFUATA MATAMANIO YA NAFSI YAKE....

KWA HAKIKA VITIMBA VYA SHETANI NI VITIMBI DHAIFU; hawezi shetani kukushika kukulazimisha jambo lolote bali hukushawishi na WEWE UTALITEKELEZA KWA UTASHI WAKO MWENYEWE....

ATAKUPAMBIA juu ya NGONO, KUDHULUMU MALI NA HAKI ZA WENGINE, UBAKHILI KWA KUKUHOFISHA UTAFILISIKA, ATATUPAMBIA VILIVYOVICHAFU KUWA VIZURI NA MIFANO MINGINE MINGI...

MUNGU AMETUWEKEA KILA UPANDE WAZI ILI IWE JUU YA KILA MMOJA KUCHAGUA na siku ya malipo hakutakuwa na kusema hatukujua...

Na shetani siku ya HUKUMU ATAJIENGA NA KILA ATAKAMLAUMU YEYE...

MUNGU ni muweza wa kila jambo na hakuna wa kushindana na YEYE na Shetani ni kiumbe dhaifu ambaye MUNGU amejaaliwa awe mtihani kwa wanadamu...

Mungu wetu ni MUNGU mwenye Rehema na Huruma kwa viumbe wake.... tujiuulize Kwa maovu tunayoyafanya leo kama ZINAA, MAUAJI, HOMOSEXUALITY, ULEVI, DHULMA didi ya wanyonge na MACHAFU MENGINE YOTE, ZAKA HATUTOI Angekuwa ni MUNGU ASIYE NA HURUMA angeshatuangamiza Lakini KWA HURUMA YAKE AMEENDELEA KUTUPA MUDA HUENDA TUTATUBIA.. ambaye atabaki na nyendo zake mbaya mpaka mwisho wa MAISHA YAKE BASI ITAKUWA NI HASARA KWAKE...

Naomba kuwasilisha wanajamvi wenzangu..

PERFECT
 
Tatzo linakuja pale ambapo biblia ikiwa ni kitabu cha story na wala hakina ukwel itakuaje?! Nani anaweza kututhibishia kama biblia ni kitabu kama kinavyo aminiwa?
 
Kuna wanamantiki wengi pia wameainisha Mungu yupo.
Asante.

Ila, haya si mawazo yangu tu.

Ni mawazo ya kimantiki na yameainishwa hivyo na wanamantiki wengi tu.
 
Kuna wanamantiki wengi pia wameainisha Mungu yupo.
Kwa mantiki gani?

Mimi nimesoma mantiki zote muhimu za kujadili Mungu, zinazotetea uwepo wa Mungu na zinazopinga uwepo wa Mungu.

Soma"Philosophy of Religion: An Anthology"

Nakiambatanisha hapa kwa watakaopenda kusoma.

Angalia "Part Three: The Problem of Evil", page 143. Soma kwa makini.

Hapa ndipo nimepata kuanza kupingia uwepo wa Mungu miaka zaidi ya 26 iliyopita..
 
Attachments

Kitendo cha Mungu kumtupa Ibilisi duniani ni kitendo cha uonevu mkubwa sana kwa binadamu.

Ibilisi sio levo za binadamu ni levo ya Mungu maana yake Mungu yeye angekomaa naye Ibilisi hukohuko mbinguni mpaka kieleweke. Kutuletea Ibilisi huku duniani ni kutuonea tu maana hatuna uwezo wowote wa kupambana naye.

Kama Ibilisi aliweza kupigana vita kuu mbinguni akiwa na malaika wake sasa binadamu ataweza kweli kupambana na kiumbe kama hiki?

Kiumbe ambacho kiliweza kupambana na malaika wa Mungu na kikafanikiwa kuwashawishi baadhi ya malaika kwenye vita kuu mbinguni na wakaasi sasa wewe binadamu utaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Kama mbinguni tu Ibilisi alisumbua sana ambako ndiyo kuna Mungu na malaika huku duniani tutamuweza kweli?

Kama Ibilisi anauwezo wa kuingilia mipango ya Mungu na kuiharibu kama ule wa bustani ya Edeni na Mungu hamfanyi chochote anaishia tu kuwapa adhabu zisizo na maana yoyote Adam na Hawa. Hiki kiumbe sisi binadamu tutakiweza kweli?

Ilifikia hatua Mungu mwenyewe aliamua kumtoa kafara mwanaye wa pekee( Yesu) ili aweze kupambana na Ibilisi ila mission ikabuma. Sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Hivi unajua kama Ibilisi anaongea na Mungu moja kwa moja? Maana yake Mungu na Ibilisi huwa wanaonana. Unajua mazungumzo ya Mungu na Ibilisi kuhusu Ayubu? Sasa sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi anayeweza kuongea na Mungu moja kwa moja?

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani?
Hapa binadamu tumeonewa sana.

Jukumu la kupambana na Ibilisi ni jukumu la Mungu mwenyewe na sio la binadamu hivyo Mungu amtoe Ibilisi duniani na akaishi naye mbinguni sisi huku hatumuwezi.

Ndio maana imekuwa ni kawaida tu kumkuta mtu ni mfia dini haswa ila ni mzinifu,muongo,muuaji,mchawi,tapeli,mwizi, mnafiki n.k.

Nani kakudanganya kuna binadamu anaweza kupambana na Ibilisi?
Hakuna Ibilisi duniani. All supernatural powers are equal, the difference between them is how each supernatural power operate in the spiritual & physical world.
 
Mtoa mada umeandika mashudu tu.

Ipo hivi.

Iblis sio malaika, hakuwahi kuwa malaika na hakuwahi kuwashawishi malaika walete uasi mbinguni.

Iblis ni jini, bimaana asili yake imetokana na moto ili hali binadamu asili yake ni udongo. Malaika wao asili yao ni Nuru na ni viumbe ambavyo havimuasi Mungu bali vinafanya yale waliyoamrishwa tu na havina uwezo wa kupinga kama ilivyo kwa majini na wanadamu.

Majini na wanadamu ndio viumbe pekee vilivyopendelewa na Mungu kwa kupewa free will ( uwezo wa kuamua kutenda ama kutokutenda), Majini na wanadamu ndio viumbe pekee vinavyoweza kuasi ama kutii amri za Mungu. Hii free will tuliyopewa na Mungu ni amanah ambayo tumekabidhiwa kuwa iwapo tutamuamini Mungu na kisha kufuata maamrisho yake na kuacha makatazo yake basi pasi na shaka tutalipwa malipo mazuri (kuzawadiwa Pepo/paradise) na iwapo hii amanah hatutaitunza na kuamua kutokumuamini Mungu na kufanya yale aliyotuamrisha basi tutakutana na adhabu chungu ya moto wa jahannam. Case closed...hili agano lilishafanyika baina yetu na Mungu.

Viumbe vingine vyote kuanzia milima,mbingu,bahari na ardhi vilikataa kuibeba hii amanah kwa kuelewa uzito wa adhabu ya Mungu iwapo vitakengeuka, vyenyewe viliamua kutii moja kwa moja ila mwanadamu alikubali kuichukua hiyo amanah licha ya kuwa ni kiumbe mdhaifu sana na mwenye kujidhulumu nafsi yake na pia ni mjinga.
 
Back
Top Bottom