Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Watu wanafurahisha sana mida mingine, mtu kakurupuka huko kaja na mifano isiyo na kichwa wala miguu; “kunyoa kipara ni moja ya mtindo wa kusuka nywele? “ hii ni nini sasa lmfao? kipara huwa kinanyolewa? pia, kipara na kusuka wapi na wapi?. Hii ndo changamoto ya kukurupuka kwenye kufikiri, kwa hicho kibonzo kwa upeo wake aliona ni hoja, pia kwa asiyekuwa na uelewa wa kuchanganua mambo katika dimension zote anaweza akaona jamaa ameweka jiwe pale, lakini kwa wanaouelewa mchezo wangeuliza kwa nini asingeandika “kipara ni moja ya mtindo wa kunyoa nywele?”, hivyo tu imejitosheleza. Najua shabaha yake ilikuwa kuandika swali lenye mkinzano wa kimaana, kama ni hivyo alitakiwa aandike “kipara ni moja ya mtindo wa kusuka nywele?” na si hivyo alivyoandika – huo ni ufahamu mbovu. I NEVER ABANDON MY WEAK STUDENT

Hakuishia hapo akatoa na mfano wa pili wa “MAMA wa miaka 30 na MTOTO wa miezi 6” akieleza kwamba ukiambiwa “mtoto wa miezi 6 ndiye aliyemzaa mama wa miaka 30”, huu mfano kwenye LOGIC ni ABSURDITY - ni uongo, haiwezekani, sababu unapingana na BASIC LAW OF LOGIC ambayo ni LAW OF CONTRADICTION au NON CONTRADICTION, Hilo ni sahihi na mimi naunga hoja

Cha ajabu, huo huo mfano kwa mujibu wa nadharia ambayo yeye anaisadikisha - anaiamini ya CAUSALITY IN QUANTUM PHYSICS hilo jambo lipo - ni sahihi, nadharia inalazimisha kulielezea hivyo. CAUSALITY IN QUANTUM PHYSICS inasema “effect precipitates the cause in loop or cycles” au “effect happen before the cause in infinite quantum loop or cycles”. Tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni kwamba “MATOKEO hujiri/huwepo/hutokea kabla ya (V/K)ISABABISHI kwenye tabaka la mzunguko lisilo na mwanzo wala mwisho”. Kwa maana hiyo ni kwamba kwenye infinite quantum loop “MTOTO hutokea kabla ya MZAZI”, mimi nauliza je ni sawa? ni sahihi? inawezekanaje?. Yaani “uwepo wako “mtoto” utangulie uwepo wa wazazi wako?” = “mtoto uzaliwe kabla ya wazazi wako” huo ni uongo, haiwezekani, ni lazima visababishi viwepo/vitangulie kabla ya matokeo, au walau basi wangeleta “assumption” kwamba cause ‘visabanishi' viwe simultaneous na matokeo ‘effect' lakini visababishi ‘cause' viwe superior/greater/faster kuliko matokeo ‘effect', la sivyo wazazi na mtoto watakuwa na umri mmoja hahahaha

NB: Wanaosoma huu uzi naomba watafute uzi wenye mada: wanaopinga uwepo wa MUNGU ni wakaidi 2 ndo utanielewa vizuri

Uzi wa wasioamini uwepo wa MUNGU ni wakaidi 2 nilimwambia kwa kuwa anaamini “INFINITE QUANTUM LOOP” basi ATUTHIBITISHIE uwepo wake, hakufanya hivyo – na nina confidence interval 100% kwamba hawezi kuthibitisha hilo na cha ajabu anaamini uwepo wake, lakini likija suala la uwepo wa MUNGU hata akithibitishiwa convincingly kwa inference – empiricism – rationale – noumenal – phenomenal hataki kuamini, Sasa hii ni nini?
1.Hujathibitisha Mungu yupo.

2. Hujaondoa contradiction ya problem of evil. Kama hata umeielewa.

3. Hujui kusoma kwa ufahamu.

4. Hujui kufikiri kimantiki.

5. Hujui kufikiri kidhahania.
 
Dawa ya kumshimda ibilisi ni kumwamini Yesu. Ukiiamini kazi ya Yesu msalabani utapata ushindi maana uzao wa mwanamke (Yesu) ulishamponda Ibilisi kichwa. Saivi ni mkia tu unachezacheza.


YESU NI BWANA NA MWOKOZI
 
Hayaeleweki ndio maana yanaaminiwa tu.
Haieleweki katika akili za binadamu matter, energy, space, uhai na ulimwengu wote kwa ujumla vilikujaje duniani ndio maana imani zinakuwepo
Kwanza kabisa, unajuaje mambo yaliyo nje ya uwezo wa akili za binadamu kuyaelewa kwa kutumia akili za binadamu?
 
Sihoji imani, nahoji ukweli uko wapi.

Kimantiki, Mungu hayupo.

Kwa sababu, dhana ya kuwepo kwake ina contradiction inayoonesha Mungu hayupo.

Huo ndiyo ukweli.

Kwenye imani sitaki kukuingilia kwenye imani yako.

Imani si lazima ifuate ukweli.

Unaruhusiwa kuamini hata uongo.
Ni nani aliyekuumba wewe? Em tuambie mwanzo wako?

Rakims
 
Hayaeleweki ndio maana yanaaminiwa tu.
Haieleweki katika akili za binadamu matter, energy, space, uhai na ulimwengu wote kwa ujumla vilikujaje duniani ndio maana imani zinakuwepo
Sawa.

Nikikwambia mimi ndiye Mungu muumba yote, na jambo hilo lipo nje ya uwezo wa binadamu kulielewa, hivyo amini tu, utaamini?
 
Siwezi kukuamini kwa sababu uko ndani ya uwezo wangu kukuelewa. Naweza kufahamu ulizaliwa lini, madhaifu yako na taarifa zako nyingine nyingi za kibinadamu. Naweza kukuelewa vizuri kwamba huwezi kuwa mungu.
Sawa.

Nikikwambia mimi ndiye Mungu muumba yote, na jambo hilo lipo nje ya uwezo wa binadamu kulielewa, hivyo amini tu, utaamini?
 
Siwezi kukuamini kwa sababu uko ndani ya uwezo wangu kukuelewa. Naweza kufahamu ulizaliwa lini, madhaifu yako na taarifa zako nyingine nyingi za kibinadamu. Naweza kukuelewa vizuri kwamba huwezi kuwa mungu.
Unajuaje kwamba sipo katika uwezo wako wa kunielewa, ila wewe huelewi tu, kwa sababu sipo katika uwezo wako wa kuelewa?

Na pia, unajuaje kuwa Mungu yupo kweli nje ya uwezo wako wa kumuelewa, na si kwamba hayupo, ila wewe umeaminishwa tu kwamba yupo nje ya uwezo wako wa kumuelewa?

Umesema unaweza kujua mimi si Mungu kwa sababu unaweza kujua tarehe yangu ya kuzaliwa,madhaifu yangu, anaweza kunielewa.

Kama hiki ndicho kigezo huoni kwamba kama Mungu hayupo, huwezi kujua siku yake ya kuzaliwa, madhaifu yake etc, kwa sababu hayupo. Na hivyo utaamini yupo wakati hayupo?
 
Kitendo cha Mungu kumtupa Ibilisi duniani ni kitendo cha uonevu mkubwa sana kwa binadamu.

Ibilisi sio levo za binadamu ni levo ya Mungu maana yake Mungu yeye angekomaa naye Ibilisi hukohuko mbinguni mpaka kieleweke. Kutuletea Ibilisi huku duniani ni kutuonea tu maana hatuna uwezo wowote wa kupambana naye.

Kama Ibilisi aliweza kupigana vita kuu mbinguni akiwa na malaika wake sasa binadamu ataweza kweli kupambana na kiumbe kama hiki?

Kiumbe ambacho kiliweza kupambana na malaika wa Mungu na kikafanikiwa kuwashawishi baadhi ya malaika kwenye vita kuu mbinguni na wakaasi sasa wewe binadamu utaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Kama mbinguni tu Ibilisi alisumbua sana ambako ndiyo kuna Mungu na malaika huku duniani tutamuweza kweli?

Kama Ibilisi anauwezo wa kuingilia mipango ya Mungu na kuiharibu kama ule wa bustani ya Edeni na Mungu hamfanyi chochote anaishia tu kuwapa adhabu zisizo na maana yoyote Adam na Hawa. Hiki kiumbe sisi binadamu tutakiweza kweli?

Ilifikia hatua Mungu mwenyewe aliamua kumtoa kafara mwanaye wa pekee( Yesu) ili aweze kupambana na Ibilisi ila mission ikabuma. Sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi?

Hivi unajua kama Ibilisi anaongea na Mungu moja kwa moja? Maana yake Mungu na Ibilisi huwa wanaonana. Unajua mazungumzo ya Mungu na Ibilisi kuhusu Ayubu? Sasa sisi binadamu tutaweza kweli kupambana na Ibilisi anayeweza kuongea na Mungu moja kwa moja?

Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani?
Hapa binadamu tumeonewa sana.

Jukumu la kupambana na Ibilisi ni jukumu la Mungu mwenyewe na sio la binadamu hivyo Mungu amtoe Ibilisi duniani na akaishi naye mbinguni sisi huku hatumuwezi.

Ndio maana imekuwa ni kawaida tu kumkuta mtu ni mfia dini haswa ila ni mzinifu,muongo,muuaji,mchawi,tapeli,mwizi, mnafiki n.k.

Nani kakudanganya kuna binadamu anaweza kupambana na Ibilisi?
Ni hadithi tu za kusadikika
 
Nani kasema Mungu na Shetani ni maadui? Wale ni washikaji tena bila shaka ni mtu na mdogo wake wanaogombania kiti cha ufalme. Ili kufanikisha malengo yao zana za vita ni sis wanadamu. Ni kama Russia na USA kwa vile wote ni wakubwa hawawezi pigana direct wanamtumia Ukraine. Shetani hayuko mbinguni wala duniani yuko kila mahali ni kama Mungu naye yuko kila mahali, shetani ana nguvu kama Mungu na uwezo wake ni wa kimungu ndo maana Mungu hawezi pigana naye, uko mbinguni ana kundi la Malaika analitawala na Duniani hivyo hivyo ana kundi lake, kilichobaki na wote wawili kuendelea kushindana kuongeza makoloni(binadamu na malaika) ili atakayepata wafuasi wengi ndiye atawale.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Swali lako liko biased, kwa nini unauliza "nani" ?
Kwa jibu lako tu mkuu kwa kujibu swali juu ya swali inaonyesha ni kiasi gani bado huna uelewa hata na kile nilichouliza sawa let's see how you will understand this;
wacha nikuulize kwa impartiality,
Nini chanzo chako wewe?

Rakims
 
Kwa jibu lako tu mkuu kwa kujibu swali juu ya swali inaonyesha ni kiasi gani bado huna uelewa hata na kile nilichouliza sawa let's see how you will understand this;
wacha nikuulize kwa impartiality,
Nini chanzo chako wewe?

Rakims
Chanzo changu mimi ni Baba na Mama yangu.

Kwa nini umeuliza hivyo?
 
Chanzo changu mimi ni Baba na Mama yangu.

Kwa nini umeuliza hivyo?
Okay generation jinsi inavyokwenda chanzo chako nyuma ya bin Adam ni nini kwa uelewa wako maana umekubali Mungu hayupo. Umekubali kwa imani au umekubali kwa akili?

Rakims
 
Okay generation jinsi inavyokwenda chanzo chako nyuma ya bin Adam ni nini kwa uelewa wako maana umekubali Mungu hayupo. Umekubali kwa imani au umekubali kwa akili?

Rakims
Adam ni nani na unahakikishaje alikuwapo?

Generations sijui zimetokea wapi, kuna utata mwingi, lakini jibu la Mungu si sahihi.

Kwa sababu Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote aliyeumba dunia hii hayupo.

Hilo si jambo la imani tu, ni jambo la kimantiki.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom