Hivi Mungu amemshindwa shetani kabisa? Basi shetani tumpe maua yake

HAPANA

Si busara kumpangia mtu tabia ya kujidhihirisha ama kudhihirisha mambo--bora kuonesha mfano bora wa mwenendo wa kujichagulia, mengine waachie wadau waamue wenyewe...

'Mungu' ama 'mungu' ni maneno tu kuwasilishia dhana na fikra... fikra zaweza kuwa hoja ama viroja; mawaidha yanaweza kuwa porojo ama 'Uono Fasaha'--Inategemeana na utatu wa 'vina vya tafsiri', 'Dhamira' na 'Uono na Ufikirifu Mifumo'...

Muanzisha wa huu uzi ameleta tu hoja ya mjadala...

Kuna namna ya kudadavua msingi wa utata wake wa urazini na kuhoji; lakini haimaanishi kama mjadala una 'tija' kiroho...

Tuwe na Subira kidogo na tuombe kheri, siku si nyingi swali la huyu mdau litapatiwa ufumbuzi na mwangaza... Japo ni safari ni ndefu kidogo, kuyaweka sawa yale yote ya imani, tumaini na upendo...

Kwa upande mwingine mzaha una 'katisha stimu' ya umakini... Utani vile vile...

Waliokuwa na mizaha na utani, na tena wenye kuwa na shilingi/talanta lakini inatumika vibaya, wanaweza kujizungusha kwenye ubatili hata kama shahidi za ufunuo zipo; lakini 'mguso ukiwafikia' wanaweza kujisahihisha...

Ni vema iwepo dhamiri ya 'Nuru ya Ufahamu' -- hii itatuondoa kwenye fikra za kitumwa, kutuweka katika wanda sahihi za kutambua asili za mambo, shughuli na taasisi zetu; kutambua, kujitambua na kutambuliwa...

Hmmm
 
Hata huyo Mungu ni wakulaumiwa kwa kushindwa kuumba Dunia isiyo na uovu wala matatizo.

Majanga ya asili kama radi, mafuriko, matetemeko ya ardhi na vimbunga kama huyo Mungu ndiye Muumbaji wake basi ni wakulaumiwa sana.

Ulipenda kuzaliwa kwenye Dunia yenye matatizo na majanga ya asili ambayo huwezi kuya eliminate yakaisha kabisa?

Huoni kwamba huna free will?
 
Shida wengi wanataka kumuelewa Mungu kama babu yao au mjomba wao........hizo hadithi ukizichukulia kimwili utabaki tu hapohapo
Kama hazitakiwi kuchukuliwa kimwili basi hazina maana yoyote kwa binadamu.
 
apo kazi kwako,kumfata Mungu au shetani unakoona wewe kuna usalama zaidi,,na kama ni msoma maandiko majibu ya maswali yako yote yapo mle.
Hayo mambo hautayaweza mdogo wangu bora twende zetu kwenye zile mada zetu za kula tunda kimasihara.
 
Haya turudi kwenye mada
Kwanini shetani hauliwi?

#YNWA
 
Na maustaadh nao wanasemaje juu ya ubabe wa sheitwan jee Allah naye amemgwaya huyu kiumbe sheitwan?
 
Hata huyo Mungu ni wakulaumiwa kwa kushindwa kuumba Dunia isiyo na uovu wala matatizo.
MUNGU kaumba dunia tupu, akumba mfumo wa kuyawezesha maisha kuwepo. Uovu ni wa binadamu.
Majanga ya asili kama radi, mafuriko, matetemeko ya ardhi na vimbunga kama huyo Mungu ndiye Muumbaji wake basi ni wakulaumiwa sana.
Dunia lazima ifanye kazi kwa mfumo. Umetengeneza gari, ili litembee si ni lazima vyuma visagane?
Ulipenda kuzaliwa kwenye Dunia yenye matatizo na majanga ya asili ambayo huwezi kuya eliminate yakaisha kabisa?

Huoni kwamba huna free will?
Freewill tunayo sababu baada ya kuzaliwa nature ilitupa akili ya namna ya kukabiliana na majanga.

Baharini kuna dhoruba ila binadamu tunajenga nyumba zinazoelea na tunaifuatuata dhoruba.
 
Turudi kwenye mada
Kwanini shetani hauliwi?

#YNWA
Kwanini shetani anatakiwa kuuwawa boss? Binafsi naona uwepo wa shetani ni mpango wa MUNGU tena aliujua wakati wa uumbaji na akauruhusu.
 
Kama Mungu yupo basi hata wenye dini zao hawamjui vizuri
 
Majibu yote kuhusu Mungu na kuhusu Shetani yanapatikana baada ya kufa πŸ‘πŸ™„

Everybody wants to go to heaven but nobody wants to die πŸ™„πŸ˜³πŸ‘

Sasa utafikaje ??🀠🀠
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…