Hivi Mungu na Shetani bado wanawasiliana?

Hivi Mungu na Shetani bado wanawasiliana?

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Ukisoma kitabu cha Ayubu 1: 6 - 9
Ayubu 1: 7-9

[7]BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

[8]Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.

[9]Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure?

Mimi napenda kufikiria nje ya boksi.. ukiangalia hii communication pattern kati ya Shetani na Mungu, mbona ipo ki friendly sana?

Yaani ni kama pande mbili ambazo zinaelewana sana tu na huwa zinawasiliana kila siku..

Kwa hiyo communication pattern, hivi kweli Mungu na Shetani wana bifu kali kiasi hicho? au wana same mission ya kumfanya mwanadamu azidi kuwa mtii kwa Mungu?
 
Ila kipindi kile cha Japheth, shedrack na Abednego walipotupwa kwenye tanuru ya moto yule malaika wa nne aliyeonekana alikuwa mwamba mwenyewe Yesu.

Unaambiwa Gabriel alitumwa Kwanza kwenda kuwaokoa shetani akamzuia njiani Kwa kumshushia kibano kikali hakarudi mbinguni hoi akamuambia Mungu ngoma kali.

Mwamba Mikaeli Yesu mwenyewe akasema tu thisbulsh akaamua kushuka. Unaambiwa nusu sekunde tu alishafika kwa akina shedrack huku akimtembezea shetani na malaika zake mkong'oto wa haja na wa aina yake.
 
Amna walizinguana pale alipomnyima yesu mikate mlimani.
Sagodi alisusa...shetty akasema isiwe kesi mi ntamsulubu yesu.
Yesu msalabani nae akatemwa na mshua wake.
Huyu mshua anasusa sana.
ndo vile ulipatikana kwa mganga hakuna budi kuchagua mizimu.😂😂😂😂
#kila mtu na iman yake
 
Ukisoma kitabu cha Ayubu 1: 6 - 9
Ayubu 1: 7-9

[7]BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo...
Haikuishia hapo baada ya shetani kuteketeza utajiri wote wa Ayubu, shetani na mungu walikutana tena Mungu akamwambia shetani umeona utiifu wa mja wangu, shetani akasema nyoosha mkono kwenye afya yake kama hata kudhihaki,

Mungu akamwambia nimekupa mamlaka mfanye chochote uwezacho lakini usichukue uhai wake, (sijako andikobneno kwa neno ni massage ninayoikumbuka). Ukiqngalia hapo ni kama mungu na shetani ni watu wa karibu sana,
 
Amna walizinguana pale alipomnyima yesu mikate mlimani.
Sagodi alisusa...shetty akasema isiwe kesi mi ntamsulubu yesu.
Yesu msalabani nae akatemwa na mshua wake.
Huyu mshua anasusa sana.
1_mXW8KyGPtl8XvQ1bDit5fg.jpeg
 
Back
Top Bottom