Hivi Mungu na Shetani bado wanawasiliana?

Hivi Mungu na Shetani bado wanawasiliana?

Yani unaambiwa Mwamba Yesu alivyokuwa anashuka kuwaokoa akina shedrack njiani alikuwa anatembeza mkong'oto wa haja na wa aina yake. Shetani alitimua vumbi shetani ni muoga sana ukimjulia. Ndo maana ukiwa na Yesu ana keep a very big distance anajua vizuri moto wake

Pia siku ile Mwamba Yesu alivyofufuka unaambiwa wale waliobeba jiwe kubwa kufunika kaburi walikuwa shetani na malaika zake shetani. Binadamu wa kawaida wasingeweza kubeba lile jiwe kwasababu lilikuwa zito na kubwa.

Na walikesha siku tatu mfululizo kulinda kaburi na kusubiri kweli atafufuka?

Ilipofika jumapili morning Kali Mwamba akaamka na kupiga lile jiwe teke na kuanza kuwatembezea mkono nje kabla ya kupaa kwa baba yake.

Shetani unaambiwa alichomoka balaa huku haamini akilia na kulaani damn binadamu kakombolewa.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mungu na shetani hawana bifu, shetani ni kiumbe wa Mungu. Bosi ni mmoja tu hapo. Shetani ndio alichagua kukaidi amri ya Mungu akapokea malipo yake, lakini sio kwamba kuna nguvu mbili zinavutana, hapana. Bali sisi wanadamu pia tulichagua kukaidi amri ya Mungu (Adam na Hawa) hivyo kuingia kwenye mamlaka ya shetani. Mungu anatusihi turejee kwake ili tuishi kwa kadiri ya kusudi lake. Shetani hakumwumba mwanadamu hivyo hana mpango wowote wa baadaye kwake zaidi ya kumtakia uangamivu
Sasa kama shetani na Mungu hawana bifu... ni kwanini sasa shetani atake mwanadamu apotee?
 
Exactly, Shetani anasubiri tu hukumu yake kwa sasa ndio maana anazidi kuivuruga dunia kuchochea mambo yasiyo ya kimaadili na mambo mengine mengi mabaya ili siku atajapokuja kuhukumiwa aende na wengi

Ana hasira kinyama mbwa yule
Bado inafikirisha kwanini muda huu shetani anasubiri hukumu hadhibitiwi? Maana hata katika milki zetu za kibinadamu mtu anayesubiri hukumu akivunja masharti ya dhamana hutupwa mahabusu hadi hukumu yake, kwanini shetani hadhibitiwi anaachwa tu? Huoni anapendelea kwa hasara yetu binadamu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Vipi umemaliza kucheza na majini hapo masjid?

Shetani alifukuzwa mbinguni yeye na theluthi ya malaika walioamua kumfuata na ndio hao wanaitwa malaika zake.
Wewe huja elewa aliposema shetani anawezaje kuwa malaika? Ni hivi katika Uislamu shetani sio malaika, shetani ni moja ya majini ama viumbe waliokumbwa kwa moto na malaika wameumbwa na nuru na kwamba shetani kama angekuwa malaika asingesaliti

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Walishatosana kitambo....shetani na kichwa chake kama gobole havumiliki
 
Ni sawa na usiku na mchana, (mwanga na Giza) mwanga anampisha Giza na Giza linampisha mwanga. Wanaelewana na wanashirikiana.
 
Sasa kama shetani na Mungu hawana bifu... ni kwanini sasa shetani atake mwanadamu apotee?
Shetani anatafuta kuharibu uumbaji wa Mungu, lakini Mungu hana cha kuharibu kwa shetani kwa sababu vyote ni mali yake. Hakuna kitu chochote alichoumba shetani.

Uhusiano wa Mungu na shetani ni sawa na uhusiano kati ya baba na mwanae. Baba ndiye aliyemzaa mwana, ikitokea mtoto anakaidi maagizo ya baba, mfano kuwa mwizi, mzinzi nk baba anaweza kumfukuza atoke nyumbani mwake. Lakini hiyo inaweza isimzuie kuja kuwaona ndugu zake mara moja moja. Ndivyo ilivyokuwa kwa shetani baada ya kuasi, Mungu alimfukuza toka mbinguni akawa hana kikao, anatangatanga duniani. Hata hivyo alikuwa na ruksa kwenda mbinguni kwenye kusanyiko la wana wa Mungu, ingawa yeye alishapoteza hadhi hiyo kutokana na kukaidi kwake maagizo ya baba yake.

Vipi ikitokea mtoto huyu mbabe akaamua kujitangaza kuwa ni baba wa mji na hivyo kuanzia sasa waliokuwa kaka na dada zake watakuwa wanae, halafu mama atakuwa mkewe? Hapo baba ataweza kumfukuza kabisa tena asionekane nyumbani kwake. Wala NAFASI YAKE kama mwana haitaonekana tena! Ndivyo ilivyokuwa kwa shetani. How?

Alipoasi mwanzoni Mungu alimfukuza toka makao yake, lakini alikuwa na kibali cha kujihudhurisha mbinguni (Ayubu 1🙂. Baaada ya kuona haitoshi, shetani aliamua kuvipiga vita ili achukue mamlaka kwa nguvu, ndipo Mungu alipomwondoa kabisa mbinguni na NAFASI YAKE haikuonekana tena:

Ufunuo wa Yohana 12
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁷ Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
⁸ nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
⁹ Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
¹⁰ Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.


Hili neno linajibu swali lako kama shetani bado anakwenda mbinguni? Nafasi yake ilifutwa, kwa maana kwamba HANA MSAMAHA TENA. Mwanadamu anapotenda dhambi huondoka kwenye uwepo wa Mungu, lakini akitubu akasamehewa hurudi kwenye NAFASI YAKE kama mwana wa Mungu. Kwamba huweza kujihudhurisha kwenye uwepo wa Mungu. Lakini akitenda dhambi ya mauti (blasphemy) NAFASI YAKE huondolewa kabisa mbinguni na hatakuwa na msamaha tena. Umeelewa?

Kaini kwa mfano aliondolewa kwenye uwepo wa Mungu na nafasi yake haikuonekana tena, akawa kama shetani, akaishi kwa kutangatanga bila ya ulinzi wa Mungu.

Mwanzo 4
¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹² utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
¹³ Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
¹⁴ Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.


Nafasi ya Kaini ilifutwa kabisa mbinguni, akaishi mbali na uwepo wa Mungu. Ndivyo ilivyo kwa mtu anayetenda dhambi ya mautimauti (1 Yoh 5:16).
 
Back
Top Bottom