Sasa kama shetani na Mungu hawana bifu... ni kwanini sasa shetani atake mwanadamu apotee?
Shetani anatafuta kuharibu uumbaji wa Mungu, lakini Mungu hana cha kuharibu kwa shetani kwa sababu vyote ni mali yake. Hakuna kitu chochote alichoumba shetani.
Uhusiano wa Mungu na shetani ni sawa na uhusiano kati ya baba na mwanae. Baba ndiye aliyemzaa mwana, ikitokea mtoto anakaidi maagizo ya baba, mfano kuwa mwizi, mzinzi nk baba anaweza kumfukuza atoke nyumbani mwake. Lakini hiyo inaweza isimzuie kuja kuwaona ndugu zake mara moja moja. Ndivyo ilivyokuwa kwa shetani baada ya kuasi, Mungu alimfukuza toka mbinguni akawa hana kikao, anatangatanga duniani. Hata hivyo alikuwa na ruksa kwenda mbinguni kwenye kusanyiko la wana wa Mungu, ingawa yeye alishapoteza hadhi hiyo kutokana na kukaidi kwake maagizo ya baba yake.
Vipi ikitokea mtoto huyu mbabe akaamua kujitangaza kuwa ni baba wa mji na hivyo kuanzia sasa waliokuwa kaka na dada zake watakuwa wanae, halafu mama atakuwa mkewe? Hapo baba ataweza kumfukuza kabisa tena asionekane nyumbani kwake. Wala NAFASI YAKE kama mwana haitaonekana tena! Ndivyo ilivyokuwa kwa shetani. How?
Alipoasi mwanzoni Mungu alimfukuza toka makao yake, lakini alikuwa na kibali cha kujihudhurisha mbinguni (Ayubu 1
🙂. Baaada ya kuona haitoshi, shetani aliamua kuvipiga vita ili achukue mamlaka kwa nguvu, ndipo Mungu alipomwondoa kabisa mbinguni na NAFASI YAKE haikuonekana tena:
Ufunuo wa Yohana 12
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁷ Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
⁸ nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
⁹ Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
¹⁰ Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Hili neno linajibu swali lako kama shetani bado anakwenda mbinguni? Nafasi yake ilifutwa, kwa maana kwamba HANA MSAMAHA TENA. Mwanadamu anapotenda dhambi huondoka kwenye uwepo wa Mungu, lakini akitubu akasamehewa hurudi kwenye NAFASI YAKE kama mwana wa Mungu. Kwamba huweza kujihudhurisha kwenye uwepo wa Mungu. Lakini akitenda dhambi ya mauti (blasphemy) NAFASI YAKE huondolewa kabisa mbinguni na hatakuwa na msamaha tena. Umeelewa?
Kaini kwa mfano aliondolewa kwenye uwepo wa Mungu na nafasi yake haikuonekana tena, akawa kama shetani, akaishi kwa kutangatanga bila ya ulinzi wa Mungu.
Mwanzo 4
¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹² utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
¹³ Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
¹⁴ Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
Nafasi ya Kaini ilifutwa kabisa mbinguni, akaishi mbali na uwepo wa Mungu. Ndivyo ilivyo kwa mtu anayetenda dhambi ya mautimauti (1 Yoh 5:16).