Ndugu yangu nakushauri usome Quran, utamjua Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Dunia na aliyetuumba sisi na vizazi vivyopita kwa uzuri kabisa. Sio lazima uwe Muislamu ndio usome Quran, wewe soma ili kujifunza I hope utafahamu mengi kuhusu dunia, wanaadamu, maisha baada ya kifo, na pia utamfahamu Mwenyezi Mungu aliyeumba na anayeendesha maisha yetu. kujifunza hakuna mwisho. Mwenyezi Mungu akuongoze wewe na sisi pia. Ameen
QURAN 2: 255
"Mwenyezi Mungu - hakuna Mungu mwingine ila Yeye. Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hasinzii wala Halali. Ni vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilivyo katika ujuzi wake, ila kwa atakalo Mwenyewe. Enzi yake imeenea mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye Aliye juu, na Ndiye Mkuu."