Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo mbinguni na ardhini yupo ndugu yangu; usiahadike na hii pumzi aliyokupa ukamkufuru kwani baada ya kufa utaenda kukutana nae.
QURAN 30: 20-27
20. Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote (duniani)
21. Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
22. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana lugha zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wanao jua.
23. Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuutumia) mchana katika kutafuta kwenu fadhila (riziki) zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao sikia.
24. Na katika Ishara zake hukuonyesheni umeme (wa radi) kwa kukutieni hofu na tamaa (ya mvua). Na hukuteremshieni maji kutoka mawinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao zingatia.
25. Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapo kuiteni mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi. (mtafufuliwa kutoka makaburini)
26. Na ni vyake Yeye vilivyopo mbinguni na vilivyopo katika ardhi. Vyote vinamtii Yeye.
27. Na Yeye ndiye aliye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine(kwa kuwafufua wafu). Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima."