Hivi Mungu yupo au ni mipango ya watu kujipatia ajira na pesa?

Ndugu yangu nakushauri usome Quran, utamjua Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Dunia na aliyetuumba sisi na vizazi vivyopita kwa uzuri kabisa. Sio lazima uwe Muislamu ndio usome Quran, wewe soma ili kujifunza I hope utafahamu mengi kuhusu dunia, wanaadamu, maisha baada ya kifo, na pia utamfahamu Mwenyezi Mungu aliyeumba na anayeendesha maisha yetu. kujifunza hakuna mwisho. Mwenyezi Mungu akuongoze wewe na sisi pia. Ameen

QURAN 2: 255
"Mwenyezi Mungu - hakuna Mungu mwingine ila Yeye. Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hasinzii wala Halali. Ni vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilivyo katika ujuzi wake, ila kwa atakalo Mwenyewe. Enzi yake imeenea mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye Aliye juu, na Ndiye Mkuu."
 
Wewe mwenyewe ni Mungu ndio maana ukimwaga mimba inatunga, umeumbwa kwa mfano wake, mfano namba moja ni kuuendeleza uumbaji wake.
Mkuu nalitambua hilo ,cha msingi watu wanatakiwa waingie ndani mwao wenyewe wamjue Mungu wenyewe ,sio kuamini story za watu wazmani walioingia ndani wakamjua, kuna tofauti kati ya alie enda marekani na anaesimuliwa hadithi za marekani kwenye vtabu.
 
Lakini sisi

Ha

Kuuliza sio ujinga
Ndio; kuuliza sio ujinga. Lakini pia zingatia kwamba maswali unayouliza wakati mwingine huashiria umri wako na tena kiwango chako cha uelewa au kufikiri - yan "Hukufunua".
 
Ogopa hiyo kauli,Tajiri wa Titanic alisema meli yake haitazamishwa hata na Mungu, safari ya kwanza ikazama.

Fikiria shahawa zinakua mtu, mbegu inaota, unavuta hewa free.
Badala ya kumtishia mtoa maada na kumwambia aogope, ni vzuri ungejibu swali lake kwa kutumia hoja na mifano hai
 
Ww ushawaho kufa ukakutana naye? Au una uhakka gan kwamba hayp yaloandkwa hapo n ya kweli?

Je kama mwandisho alilenga tu kuwajaza hofu binadamu?
 
Nithibitishie kwamba yaliyoandikwa kwny Quran ni sahh!
 
Badala ya kumtishia mtoa maada na kumwambia aogope, ni vzuri ungejibu swali lake kwa kutumia hoja na mifano hai
Hajamtishia mtoa mada ila amemuonya tu kuwa kauli kama hiyo sio nzuri kutokana na jinsi alivyojieleza na amempa mfano wa meli ya Titanic. Yaani inaonekana mtoa mada anamalalamiko dhidi ya huyo anayeitwa Mungu. Kwa mujibu wa maelezo yake mtoa mada ni kwamba Mtoa mada anapitia hali tete (yupo kwenye wakati mgumu sana) na amekuwa akimwomba Mungu msaada na ametumia hata fedha yake katika harakati hiyo lakini hajafanikiwa na wahubiri/watangazaji wengi wa habari za Mungu wameendelea kuhubiri na wamemjulisha kwamba ni Mungu mwema, mwenye huruma na anawapenda watu na huwasaidia watu wamwombao msaada. Sasa Mbona yeye kwake imekuwa sivyo? Imekuwa kinyume? i.e. hajapata majibu anayotarajia. Yaani "Mungu amemwangusha".
Mtoa mada ameingiwa na wasiwasi kuhusu habari za Mungu alizoaminishwa kwa muda mrefu na wahubiri/wapiga debe/wachungaji/viongozi wa dini n.k. isije ikawa ni habari Fake. Na kwa hiyo ana wasiwasi kwamba Mungu naye ni kitu Fake.
Lakini hapo mtoa mada amesahau kwamba hata 'Ukimya' wa Mungu nao unaweza ukuwa ni jawabu pia.
Mtoa mada amefikia hatua za mwisho za kukata tamaa, ndo maana anahoji kama huyo anayeitwa Mungu ni kweli yupo? Kwa maneno mengine kama yupo, basi anamshitaki hapa jamvini kwamba kama yupo mbona hajaweza kumjibu/kumsaidia katika mapito (Magumu/machungu) anayopitia sasa ilihali amemlilia sana na kumwomba amsaidie au amwepushie? Na mbaya zaidi "wapiga debe" walimhakikishia pasi na shaka kwamba yupo na atamsikiliza na kumsaidia.
Kwa mantiki hiyo anatumia kale ka msemo "Akili za kupewa ongeza na za kwako"
Asante.
 
Nithibitishie kwamba yaliyoandikwa kwny Quran ni sahh!
QURAN 4: 82
"Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake hitilafu nyingi '

Hebu rudia aya nilyoileta pale juu Quran 30:21-27 uangalie kama kuna uongo wowote hapo. Haya ni ambayo ni kweli katika uhalisia wa maisha yetu ya kila siku
-ni kweli Mvua inatoka mawinguni na ardhi ikipata maji inanawiri na kutoa mazao mapya
-ni kweli kuwa binadamu tumeumbwa kwa udongo scientifically proved
-ni kweli wanadamu tumetofautiana rangi na lugha na tumetawanyika duniani kote
- ni kweli binaadamu wote tunalala usiku na mchana tunatafuta riziki ya kuendesha maisha yetu
-ni kweli wanaume wanapata utulivu kutoka kwa wake zao
-ni kweli mbingu imesimama bila nguzo yeyote
aliyosema hayo ni Mwenyezi Mungu, je kuna uongo wowote hapo?
 
Kwema wakuu, kwa hali ilivyo najiuliza je kweli Kuna Mungu au ni business za watu kutufanya mazuzu na kula pesa zetu?
Taifa kubwa la Marekani kwenye dollar yao wameandika In God we trust, wewe ni nani hujavumbuwa hata vuzi la bata use na mashaka na uwepo wa Mungu?

Ungeuliza uhalali wa dini kama ni za kweli au magumashi ningekuelewa na ningekujibu dini ni project na investment za binadamu, lakini Mungu yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…