Hivi Mungu yupo au ni mipango ya watu kujipatia ajira na pesa?

Hivi Mungu yupo au ni mipango ya watu kujipatia ajira na pesa?

Usiwe mzembe, Fanya uchunguzi utaujua ukweli, Mungu yupo na anajidhihirisha ukimhitaji, jifunze elimu ya kiroho utajua mengi zaidi
 
Wajinga ni wengi mkuu
ila kuna watu mkuu wanatugeuzaga wengine kama mazombie.
unakuta mtu anajiita profesa wa historia lkn ukimuuliza kwann vita ya kwanza na yapili zilipiganwa majibu anayokupa .moyoni unajisemea sisi bado watumwa.

nimekutoa nje ya mada mkuu.
 
mkuu,
unajua information zote ni muhimu haijalishi za uwongo au kweli.
mkuu ulichokiona uwenda kikawa inspirational kwangu unaweza kushare nijifunze.
Mkuu ntakwambia lakini jambo la msingi ni kuwa Mungu yupo na hajipendekezi kwa mtu yeyote, mtu mwenyewe anapaswa kuchukua hatua ya kwanza na ya dhati ya kumtafuta Mungu kisha Mungu atajifunua kwake, kuwa mtu wa kiroho sio hzo habari za kwenda kanisani, ni uhusiano BINAFSI BAINA YA MTU NA MUUMBA....
 
Usiwe mzembe, Fanya uchunguzi utaujua ukweli, Mungu yupo na anajidhihirisha ukimhitaji, jifunze elimu ya kiroho utajua mengi zaidi
nipo namtafuta mungu wa kweli.
nachimbua kila kona.

mpaka hapa nilipofikia mambo ni tofauti mkuu.

wewe aliwahikujidhihilisha kwako?
au aliwahikujidhilisha kwa watanzania?
 
Mkuu ntakwambia lakini jambo la msingi ni kuwa Mungu yupo na hajipendekezi kwa mtu yeyote, mtu mwenyewe anapaswa kuchukua hatua ya kwanza na ya dhati ya kumtafuta Mungu kisha Mungu atajifunua kwake, kuwa mtu wa kiroho sio hzo habari za kwenda kanisani, ni uhusiano BINAFSI BAINA YA MTU NA MUUMBA....
hakika hiyo point yakunihasa niwe mtu wa kiroho imenigusa.
 
ila kuna watu mkuu wanatugeuzaga wengine kama mazombie.
unakuta mtu anajiita profesa wa historia lkn ukimuuliza kwann vita ya kwanza na yapili zilipiganwa majibu anayokupa .moyoni unajisemea sisi bado watumwa.

nimekutoa nje ya mada mkuu.
Ni hatari sna mkuu kuifanya elimu kama chanzo cha kipato nakuacha kuitafuta elimu ili uelimike .
 
Ogopa hiyo kauli,Tajiri wa Titanic alisema meli yake haitazamishwa hata na Mungu, safari ya kwanza ikazama.

Fikiria shahawa zinakua mtu, mbegu inaota, unavuta hewa free.
📌📌📌
 
Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo mbinguni na ardhini yupo ndugu yangu; usiahadike na hii pumzi aliyokupa ukamkufuru kwani baada ya kufa utaenda kukutana nae.

QURAN 30: 20-27
20. Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote (duniani)

21. Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.

22. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana lugha zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wanao jua.

23. Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuutumia) mchana katika kutafuta kwenu fadhila (riziki) zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao sikia.

24. Na katika Ishara zake hukuonyesheni umeme (wa radi) kwa kukutieni hofu na tamaa (ya mvua). Na hukuteremshieni maji kutoka mawinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao zingatia.

25. Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapo kuiteni mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi. (mtafufuliwa kutoka makaburini)

26. Na ni vyake Yeye vilivyopo mbinguni na vilivyopo katika ardhi. Vyote vinamtii Yeye.

27. Na Yeye ndiye aliye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine(kwa kuwafufua wafu). Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima."
Jazak ALLAH Kheyraan 🙏📌📌📌
 
Wewe mwenyewe ni Mungu ndio maana ukimwaga mimba inatunga, umeumbwa kwa mfano wake, mfano namba moja ni kuuendeleza uumbaji wake.
Yah nalitambua hilo mkuu tena kwa mapana yake Buda.
 
Ndugu yangu nakushauri usome Quran, utamjua Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Dunia na aliyetuumba sisi na vizazi vivyopita kwa uzuri kabisa. Sio lazima uwe Muislamu ndio usome Quran, wewe soma ili kujifunza I hope utafahamu mengi kuhusu dunia, wanaadamu, maisha baada ya kifo, na pia utamfahamu Mwenyezi Mungu aliyeumba na anayeendesha maisha yetu. kujifunza hakuna mwisho. Mwenyezi Mungu akuongoze wewe na sisi pia. Ameen

QURAN 2: 255
"Mwenyezi Mungu - hakuna Mungu mwingine ila Yeye. Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hasinzii wala Halali. Ni vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilivyo katika ujuzi wake, ila kwa atakalo Mwenyewe. Enzi yake imeenea mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye Aliye juu, na Ndiye Mkuu."
😍😍😍
 
AYYAT QURSIYU😍😍😍🤲🤲🤲
 
QURAN 4: 82
"Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake hitilafu nyingi '

Hebu rudia aya nilyoileta pale juu Quran 30:21-27 uangalie kama kuna uongo wowote hapo. Haya ni ambayo ni kweli katika uhalisia wa maisha yetu ya kila siku
-ni kweli Mvua inatoka mawinguni na ardhi ikipata maji inanawiri na kutoa mazao mapya
-ni kweli kuwa binadamu tumeumbwa kwa udongo scientifically proved
-ni kweli wanadamu tumetofautiana rangi na lugha na tumetawanyika duniani kote
- ni kweli binaadamu wote tunalala usiku na mchana tunatafuta riziki ya kuendesha maisha yetu
-ni kweli wanaume wanapata utulivu kutoka kwa wake zao
-ni kweli mbingu imesimama bila nguzo yeyote
aliyosema hayo ni Mwenyezi Mungu, je kuna uongo wowote hapo?
❤️❤️❤️
 
Unamaanisha kitu kitokee tu from no where…ahaha …..kuna madogo fulani wa kishua wanaamini mchele unatengenezwa kiwandani, nilicheka sanaa…..

Yaani unaamini iPhone imetengeneswa na mtu,ila nature eti imetokea yenyewe…ahaha
Na hapo hapo unaamini Mungu ametokea tu ha ha ha

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Kwema wakuu, kwa hali ilivyo najiuliza je kweli Kuna Mungu au ni business za watu kutufanya mazuzu na kula pesa zetu?
Kwa ufahamu wako binafsi Mungu ni nani, maana isije ikawa unajadili kitu usicho na ufahamu nacho
 
MUNGU yupo!!,,,wa2 wengi wanaamini shetani yupo lakini hawaamini MUNGU yupo....
Unajua shetani n mjanja sana, na ukiangalia vitu vng duniani nikudistract watu kutoka kwa Mungu...
Na ukizingatia yeye niye mtawala wa dunia kwa sasa (1 yohana 5:19)
 
Mungu na dini ni vitu 2 tofauti kabisa.Mungu hana dini ila dini ni michongo ya wenye akili. Mfano kuna yesu wa tongoran kule kenya, baada ya miaka 1000 aman2000 atakuwa na wafuasi dunia nzima huyu and wataamini kabisa kuwa yesu alizaliwa kenya na alikufa akafufuka siku ya tatu ama vyovyote vile ambavyo watakuwa wameaminishwa. Vivyohivyo yesu wa nazaret tunavyoaminishwa sisi kwa sasa.
Mimi naamini katika Mungu mmoja na siamini dini yoyote
 
Back
Top Bottom