Bw.Yesu alikuja kukamilisha Torati ambayo ni agano la kale na kutengeneza agano jipya . Agano la kale, lilitakiwa kuwe na hekalu(jengo). Agano jipya, miili yetu ndiyo hekalu la Mungu aliye hai.. Agano la kale, ili Mtu asamehewe makosa aliyotenda lazima atoe dhabihu ya mnyama. Agano jipya ,ni kuomba msamaha katika jina la Yesu Mtu anasamehewa, kwa sababu hiki ni kipindi cha Neema.. NK NK. Kwa hiyo Yesu, alihubiri dini ya upendo kwa adui, msamaha kwa aliyekukosea bila masharti, kutolipiza kisasi, kuhesabiwa haki kwa njia ya kumpokea Yesu. Ndiyo maana alihubiri alisema njoni kwa nini nyote msumbkao na mizigo nani nitawapumzisha. Bw Yesu alisema agano jipya kwa kifo chake pale Golgotha msalabani. Kwa damu yake mwenyewe na si ya mnyama alipaingia patakatifu pa patakatifu ili kuwatakasa watu wote waishio hapa duniani ili kuondoka adhabu ya kifo iliyokuwa sentenced kwa Adamu na uzao wake.