Usiwe unafuata tu dini bila kusoma maandiko. Jitahidi kusoma na kuelewa. Jazba haitasaidia. Jielimishe upate ukweli.
Quran 6: 14. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.
Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. (Wa ' Ana ' Awwalu Al- Muslimin ). S. 6:161-163
Sema (Ewe Muhammad): Hakika Mimi nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu, kwa kumsafishia Dini Yeye ( tu ). Na nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wale ambao ni Waislamu ( kujisalimisha kwake ). S. 39:11-12 Pickthall
Je, nani alikuwa Muislamu wa Kwanza?
1. Katika Suran 6: 163 Koran inadai kuwa Muhammad ndie Muislam wa kwanza.
2. Katika S. 02:30 , 34-35 , 37 Koran inadai kwamba, ni Ibrahim na waumini walio zaliwa kabla ya Muhammad ndio walikuwa Waislam wa Kwanza.
3. Katika S. 5:110-111 Koran inadai kuwa eti Isa Bin Maryam ndie alikuwa Muislam wa kwanza.
4. Katika S. 2:37 Koran inadai kuwa eti Adam ndie aliye kuwa Muislam wa Kwanza.