Jamani, lazima mjue "ukipenda lazima uwe na wivu", wivu ni kipimo cha mapenzi kwa mahusiano husika.
Kumbuka, wivu lazima uwe na kiasi, kama vile vilivyo vitu vyote duniani vinavyohitaji ukiasi, maana wivu ukizidi inakuwa ni kero tena inaweza hata kuhatarisha hata hayo mahusiano yenyewe.
Hata chakula ukila bila kiasi lazima utavimbiwa, dawa ukinywa bila kiasi itakuwa ni sumu hata kupelekea kukuua.
Sasa kwenye mapenzi wivu ni lazima uwepo , na uwe wa wastani , maana yake usivuke mipaka ukawa utaabishaji kwa mwenza.
Mimi mwenyewe nitakuwa na wivu kwa nitakayempenda , lakini nitajitahidi kujitambua na kuudhibiti wivu kwa nimpendaye.
Pia kama naye atakuwa na wivu kwangu ni jambo jema maana nitajua kuwa kweli naye ananipenda.
Na kama mpenzi anajifanyisha utajua tu kupitia wivu na kubaini kiwango cha penzi lake kwako kwa urahisi kabisa.
Unajidhibiti vipi na wivu kwa mpenzi wako!,
Ni kwa kuwa na mawasiliano hai muda wowote ule kwa kila mmoja atakapokuwa anamuhitaji mwenzi wake kwa wakati, jambo ambalo litawajengea uaminifu kwa kila mmoja na kupelekea kuaminiana sana , na kusababisha wivu uwe wa kiasi "automatically", kwa pande zote.
Kwa wapenzi kukiwa na mawasiliano mazuri kunajenga kuaminiana, na mapenzi bila mawasiliano mazuri hapo penzi wala upendo , happy kutakuwa na mapenzi ya kinafiki ya kuviziana na kudanganyana.
Kwahiyo wivu ni muhimu sana uwepo, ila uwe wa kiasi kati ya wapendanao.
Ukimwamini mpenzi wako , utajikuta hata kama hujala unanenepa unanawili hasa.
Lakini imani hiyo itajengwa na mawasiliano mazuri pekee, lugha nzuri kwa umpendae, kupatikana muda wowote utakaohitajika na mpenzi wako nk.
Pia uwazi baina ya wapendanao ndiyo jambo la pili la muhimu kufanya uwe kuudhibiti wivu kwa mpenzi wako. Uwazi unasaidia kujenga na kuinua kiwango cha imani kwa mpenzi wako na kusababisha wivu uwe wa kiasi. Maana atakuamini mno na kufanya muishi maisha ya furaha na amani, hata kama umechelewa wapi basi mpenzi wako hatakuwa na wasiwasi maana anakuwa anakuamini kwamba hutamsaliti.
Na kupelekea kuudhibiti wivu.
Nafikiri kwa sasa inatosha....