Ni kweli tabia ya kukereka kereka kwa vitu vidogo ni tabia ya kutokuwa na shukrani, roho mbaya na stress.
Njia bora asubuhi ukiwa unatoka andika kimemo kibandike jikoni, kwamba leo nataka kula maji na sabuni mke wangu.
na ukiona hili swali linakukera ni kwamba na wewe hujui unataka kula nini, umempa mtu mwingine majukumu ya kujua wewe unataka kula nini, kuna siku na yeye hajui unataka kula nini. Au mara moja moja ingia jikoni tengeneza zaga, mwambie mama chanja watoto karibuni tule, kazi ya kulea familia haijawahi kuwa rahisi kwa pande zote, tuvumiliane na turahisishiane maisha, kwani kuna tatizo gani ukiulizwa leo tunakula nini ukaropoka wali maharage, unapata kigugumizi sababu hata wewe hujui unataka kula nini 😀