Hivi nchi jirani na rafiki wa kweli wa Tanzania ni ipi?

Hivi nchi jirani na rafiki wa kweli wa Tanzania ni ipi?

Japo hakuna rafiki wa kweli kwenye nchi, jirani na rafiki wetu wa kweli ni Kenya. mengine ni bifu za siblings. Burundi tulitaka kuwachapa enzi za Mkapa.
Kenya ndo jirani na ndugu yetu wa kweli,tofauti zetu huwa zinaletwa na watawala tu kwasababu watawala wetu kila mtu huja na lake

Lakini kwa upande wa raia,raia wa kenya na tz wanashibana sana
 
Najua nachokwambia, ishu iliyopo sasa ni huo UGAIDI ila Mtz ukifika Msumbiji kwanza kabisa ni free visa maisha yako yote. Uwe na Passport tu basi. Unaishi kwa amani kabisa
Kwa sasa usahau hilo.

Zamani ilikuwa kama unapaspot haina shida lakn kwasasa kama umtanzania na unajishughulisha na biashara lazima uwe na parmit na paspot uwe nayo.
 
USA wana Canada, Nigeria wana Ghana, Australia wana New zeeland.

Namaanisha yule jirani ambaye hata ukienda kumtembelea unahisi uko nyumbani tu haubaguliwi. Mila zinaendana.

Kwa Tanzania ni nani? Kenya? Uganda? Rwanda? Burundi? Malawi? Msumbiji?
Enzi za mwendazake rafiki yetu wa kweli alikua burundi, wengine wote walibaki wanatushangaa tu maana walikua hawatuelewi

Zama hizi kwa kweli sijui hata rafiki yetu ni nani labda DRC
 
Kila mtu atavutia kwake,kwa sisi jamii tunazotoka mikoa ya Mara,Kilimanjaro na Arusha tutakuambia rafiki wa kweli ni Kenya coz wengi wetu tumechanganya damu na watu wa Kenya.mfano mimi hapa ndugu zangu wengi tu wako Kenya na wameajiriwa na serikali ya Kenya,so mtu kama mimi utaniambia nini kibaya kuhusu Kenya nikakuamini?
 
Kwa sasa usahau hilo.

Zamani ilikuwa kama unapaspot haina shida lakn kwasasa kama umtanzania na unajishughulisha na biashara lazima uwe na parmit na paspot uwe nayo.
Weka hapa hiyo Sheria mpya.
 
Weka hapa hiyo Sheria mpya.
Sheria wanazo wenyewe ndio wanavyotaka na nakwambia hayo sihadithiwi ni yoyote.

Kama unaona siyo kweli ninayosema mtafute unaemjua ambaye yupo cabo delgado umuulize.
 
Hao jamaa ni kama sisi sio majirani nao!
Zambia?

Hujui kuwa Zambia na DRCongo nao ni majirani zetu?

Ni kwa masikitiko makubwa, kwamba kati ya hao wote uliowataja, hakuna rafiki wa kweli, huo ndio ukweli wenyewe.

Lakini ukitaka kulazimisha urafiki basi mpangilio utakuwa hivi kuanzia wa karibu zaidi:

Burundi, Uganda, Zambia, Msumbiji, DRC, Malawi, Kenya, Rwanda na mwisho Zanzibar.
Kha!,Kwamba Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?.
 
Kha!,Kwamba Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?.
Sijasema hivyo mkuu 'Fall Army Worm', ila yanayofanywa na viongozi nyakati hizi yanaelekea sisi wananchi tuuone huu muungano kuwa kama ni wa nchi moja ndogo sana kuitawala nchi nyingine inayosemekana ni sehemu ya muungano huo, kwa watu wake kuwa na haki zaidi juu ya wenzao kwenye muungano huo huo.
Hawa wanapenda wao kujitambulisha kwa uraia wao wa nchi yao zaidi, kuliko jina la nchi yao ya muungano.

Kwa hiyo hawa ni tofauti sana na hao wenzao wanaosemekana wameungana nao.
 
Hapa bila tashwishi ni Kenya ,wale Jamaa tunaweza kuwa na ushindani nao Ila tunaelewana , wanaconsume so much exports toka kwetu ,muziki ,movie ,kilimo ,hata kampuni zetu wanapiga mwingi Kenya ....nmekaa nao nikawaelewa Ila sijawai pata tatizo Kenya ,nlipatwa na issue Nairobi back in 2021 ,Kuna familia walinihost usiku huo vizuri Sana bila siye kujuana kabisa ,hawa wengine sema nivile tunawashinda kiuchumi ndo wananyenyekea
 
Kila mtu atavutia kwake,kwa sisi jamii tunazotoka mikoa ya Mara,Kilimanjaro na Arusha tutakuambia rafiki wa kweli ni Kenya coz wengi wetu tumechanganya damu na watu wa Kenya.mfano mimi hapa ndugu zangu wengi tu wako Kenya na wameajiriwa na serikali ya Kenya,so mtu kama mimi utaniambia nini kibaya kuhusu Kenya nikakuamini?
Kwa hiyo wewe ni mkenya, au siyo?
 
USA wana Canada, Nigeria wana Ghana, Australia wana New zeeland.

Namaanisha yule jirani ambaye hata ukienda kumtembelea unahisi uko nyumbani tu haubaguliwi. Mila zinaendana.

Kwa Tanzania ni nani? Kenya? Uganda? Rwanda? Burundi? Malawi? Msumbiji?
Kwa mtazamo wangu naona ni Kenya na Congo kulingana na watu niliokutana nao.
 
Back
Top Bottom