Acha ubishi wa kijinga, sababu kubwa ya kushuka kwa Kenya "Exports" ni kuongezeka kwa gharama kubwa za uzalishaji Kenya ukilinganisha na Uganda na Tanzania, hii inamaanisha gharama za bidhaa Kenya ziko juu haziwezi kushindana na Uganda na Tanzania.
Jiulize inawezekanaje bei ya Diesel, Petrol na Lubricants ambavyo vyote hutoka Uarabuni na kupitia Mombasa kwenda Kampala, Rwanda na Burundi, lakini ni ghali zaidi Kenya kuliko hizo nchi zingine zote za EAC?, hii ni kwasababu Kenya kuna kodi nyingi sana.
Haya yote ukiyaweka kwa pamoja, ndiyo yanayosababisha gharama za maisha kuwa juu Kenya kuliko nchi zingine. Tanzania 80% ya wanainchi wanaoishi vijijini wanajilimia chakula chao, wakati huko Kenya 70% ya watu vijijini wanategemea kununua chakula, ndio sababu Kenya lazima kuagiza chakula toka nje kila mwaka.