Pre GE2025 Hivi ndio tuseme Wahariri wanaamini Tanzania hakuna ‘Electoral fraud’?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na wewe unaweza ukawa mwandishi wa Habari, wala usijitetee. Lisu kujibu maswali yenu kwa majibu msyyoyataka msianze kupotosha wananchi kwa vipande 30. Amini usiamini kupotosha kwenu ni dhambi, tena ya mauti. Conseguances: watu wanakufa kwa magonjwa, kwa njaa, ukimwi, rushwa, kukosasa ajira, ufukara etc etc, lakini wewe hapo juu umeandika bila aibu ati pesa ipo mitaani, maji safi yapo?? Hii nchi unemployment ni zaidi ya 60%; haina middle class, nyie wahariri mnaona raha kabisa. Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Tatizo la nchi yetu ni kwamba watu wengi wanadhani kuwa chaguzi zikiwa mbovu, barabara zikiwa duni, au huduma za afya zikiwa hafifu, basi hayo ni matatizo ya Chadema pekee—kana kwamba ni Chadema peke yao wanaoteseka. Ukweli ni kwamba, mfumo mbovu wa taratibu, ikiwemo haki za msingi, unawaathiri Watanzania wengi bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Kwa mfano, kuchaguliwa katika uchaguzi ni haki ya kila Mtanzania alimradi anatimiza vigezo vya kisheria. Hata hivyo, wakati huu ambapo Tundu Lissu kupitia Chadema anajaribu kueleza na kupambana na changamoto za sheria na taratibu za uchaguzi, wengi wanadhani ni ajenda ya Chadema pekee. Lakini ukweli ni kwamba, iwapo maboresho yatafanyika, Watanzania wengi watanufaika, hata kama wao wenyewe hawajaingia mstari wa mbele kudai haki hizo.

Ikiwa chaguzi zitakuwa huru, haki, na zenye misingi imara, hata mgombea binafsi asiye na chama atakuwa na nafasi ya kushinda. Lakini kwa hali na sheria zilizopo sasa, mgombea binafsi kushinda jimbo au nafasi yoyote ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano—yaani, haiwezekani. Lakini je, kuna Watanzania wangapi hawana vyama na wangependa kugombea na kushinda ila wanakwamishwa na mfumo wa sasa wa siasa za vyama? Ni wengi. Hata hivyo, wengi wao hawawezi kutoka hadharani kudai haki zao na pengine wanaamini kuwa hizi reform ni kwa ajili ya Chadema tu.

Nikitafakari, mara nyingine naona kama mfumo wa vyama vingi haujawanufaisha Watanzania ipasavyo. Sheria na miongozo iliyopo ina changamoto zake, lakini hata hizo chache zilizopo hazifuatwi kwa usahihi. Pengine, badala ya mfumo wa vyama vingi au hata wa chama kimoja, tunapaswa kuwa na mfumo wa kati—"hybrid mode"—ambao utazingatia mazingira ya Tanzania na mahitaji halisi ya wananchi. Kwa sababu Watanzania wengi, kama mimi, tunachotaka ni maendeleo na usawa wa kugawana rasilimali za taifa, bila kujali ni mtu gani au chama gani kiko madarakani.

Kwa hivyo, tunahitaji mjadala wa kitaifa unaohusisha makundi yote, si Chadema pekee. Tunapaswa kukaa chini kama taifa na kuangalia katiba yetu, miongozo yetu, sheria zetu, na vyama vyetu, ili tupate suluhisho la matatizo yanayomkabili Mtanzania wa kawaida. Haijachelewa—bado tunaweza kufanya mabadiliko yanayowanufaisha wote.
 
Issue ni mtu au uchaguzi? So wasomi hadi wenye masters, Balile kama sikosei ana degree 3, ana Batchelor ya sheria, halafu ana Batchelor ya mass communication na masters yake so hata watu wa level kama yake nao wapo busy na personalities na sio issues? Hi nchi tumelogwa, sio bure. I thought kingejadiriwa alicho kisema Tundu na sio kumjadiri Tundu, is more than stupid
 
Ni kichaa peke yake ndio anaweza kuamini kuwa Tanzania hakuna Electral fraud, hao wengine ni waganga njaa
 
Nyie ni watu wajinga na umaskini ndio shida kubwa kwenu. Mnafikiri hata akija rais kutoka chama gani hiyo miradi ya maji na barabara haitakuwepo?! Hamjui hata kwanini siasa za vyama vingi ni muhimu.
HUYU JAMAA ALIEANZA NA LISU AJIFUNZE.... NI TAKATAKA KABISA
 
Chadema wametimiza wajibu wao wakutuonesha wahariri niwatu waaina gani ktk hii nchi, wakati mafanikio ya uwazi ukweli na uwajibikaji duniani kwakiwango kikubwa yanaletwa na waandishi wa habari,wasomi na wafanyakazi hapa kwetu nikinyume chake, hicho wanachokifanya wahariri wanadhihirisha uhalisia wao na sivinginevyo,,
 
Nyie ni watu wajinga na umaskini ndio shida kubwa kwenu. Mnafikiri hata akija rais kutoka chama gani hiyo miradi ya maji na barabara haitakuwepo?! Hamjui hata kwanini siasa za vyama vingi ni muhimu.
Mwambie hawara yako aache KUTOA mapovu. Watz hawataki kukakamaza SHINGO. Mmmbafff kabisa
 
Hatuna wahariri, tuna wakariri tuu siku hizi.
Enzi za wakina Stan Katabaro, Jenerali Ulimwengu, ndizo zilikuwa na watu kweli.
 
Mungu akubariki sana ndugu.
Huu mchango wako ni elimu bora sana ya uraia na haki za msingi za Mtanzania.
Kongole sana sana ndugu.
 
Mimi ningekuwa Lissu hata siku moja nisingehangaika na hawa wapumbavu wanaofikiria matumbo yao tu. Watu wa aina hii ni kuwadharau. Kwanza Lissu ni jina habari inayouzika kuliko wanasiasa wote wa Tanzania akiwemo Samia, halafu anakuja kuwapa soko la bure. Amekosea sana.
 
Daaaah!!!
Kweli kuna watu na viatu!
 

Asali hupofusha Kaka
 
Hujawaelewa wahariri.
Wahariri walimpa TL fursa adhimu ya kufafanua zaidi msingi wa hoja za Chadema za 'No reform, No elections", na walidodosa kubainisha jinsi msimamo huo ulivyo vigumu kutekelezeka katika mazingira na utamaduni wa kitanzania...

Bahati mbaya TL alipofikishwa kwenye 'ukuta'... kama wasipopata uungwaji mkono na watanzania walio wengi, atafanyaje...
Majibu yake yameumbua na kupambanua uwezo wake wa ustahimilivu wakati wa kujadili na kushughulikia mambo nyeti ya kitaifa yenye mitazamo kinzani.
 
Lissu ana akili nyingi, hapendi zuruma na ni mtu ambae anaishi kwa principles. Lakini kuna muda huwa naona kama vile anaipigania jamii ambayo sio sahihi. Katika jamii yetu ya wazee walioshikiria mifumo, vijana wa makamo ambao ni machawa waandamizi na hawa madogo wa GenZ sina uhakika kama mbinu za Lissu zitaleta matokeo instantly. Atakachokifanya Lissu ni kutuachia material ambayo uenda vizazi vijavyo vitatumia kama miongozo ya mabadiriko. Very inteligent man, the problem is he exist in wrong place at wrong time.
 
Wahariri wa jana ni dhahiri walihongwa.
Tena sio hongo ya pesa.
Ni hongo ya pombe.

Mhariri mzima unauliza kwamba;
"Kwanini Chadema msiende kwenye uchaguzi kwa shabaha ya kushinda viti vingi vya ubunge, halafu baadae ndio mjielekeze kuboresha mifumo ya Uchaguzi."

Sina hakika kama nili-qoute swali lake vizuri....
Sasa huyu mhariri alikuwa sober kweli?

Mwingine akauliza "Kwanza mbowe yupo Wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…