Pre GE2025 Hivi ndio tuseme Wahariri wanaamini Tanzania hakuna ‘Electoral fraud’?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama kigezo ni eloquency nafikiri wapo wengi tu. Kabudi? January? Tax? and the list goes on.. kuna namna watanzania tunajidharau sana.

On top of that English sio lugha yetu ya kwanza au ya pili… by the way BWM alikuwa mwanahabari…
 
Sasa umeandika nini hapo? Kweli Tundu anaongoza manyumbu

Unajifanya kiziwi na kipofu wa ufahamu siyo?

Nimekuambia hivi, chagua hoja moja au mbili tu za CHADEMA/Tundu Lissu zinazobeba maudhui yaliyo ktk movement ya NO REFORMS, NO ELECTION kisha Jenga hoja kanushi ili tukuone kama wewe una akili kweli au ni zoba fulani hivi mpiga mayowe ya ukichaa tu...

Au ngoja nikuchagulie hoja mbili za mfano ili tupime akili na ufahamu wako....;

HOJA #1. MFUMO WA UCHAGUZI KUDHIBITIWA NA RAIS/CCM:

===Je, si kweli kuwa mfumo wetu wa uchaguzi unadhibitiwa na Rais aliyeko madarakani ambaye currently ni Mwenyekiti wa CCM? Wewe unauonaje mfumo huo kwa maoni yako, kwamba huyu Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye naye ni mshindani ktk uchaguzi unadhani atashindwa vipi kutumia mamlaka na madaraka yake ya u - Rais vibaya (abuse of powers) ili kujipendelea yeye na chama chake? Be honest, toa maoni yako. Wewe ukweli wako ni upi dhidi ya uongo au uropokaji wa Tundu Lissu/CHADEMA kwenye hili...?

HOJA #2. UCHAFU NA MGAWANYO USIO HAKI WA MAJIMBO YA UCHAGUZI WA WABUNGE:

===Je, sio kweli kuwa Kuna mgawanyo usio sawa wa majimbo ya uchaguzi? Mfano, ni kigezo gani cha kisheria na kikatiba kilichotumiwa na NEC kwa DSM yenye wapiga kura almost 3,500,000 kuwa na majimbo 10 tu ya uchaguzi huku Zanzibar yote yenye wapiga kura 500,000 kuwa na majimbo 50 ya uchaguzi? Au kwanini Jimbo la Handeni vijijini lenye wapiga kura 24,000 Lina hadhi ya Jimbo sawa na Temeke lenye wapiga kura 475,000? Ni kwanini kuna discrepancy ya namna hii ndani ya NEC na serikali? Wewe una hoja gani against kujitetea kwenye hili...?

Ukijibu vyema, nitakuona una akili sana ndugu Stuxnet na nitawaona CHADEMA na Tundu Lissu ni waropokaji sawasawa na akili zako...🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️
 
Wewe ndio mjinga na mxengerema maji.

Uliona wapi chama tawala duniani lilisaidia chama cha upinzani kukitoa madarakani.

Wewe kama sio juha na mpumbavu Hata uchaguzi ukiwa huru na haki itashinda je kama watu hawajiandikishi .
CCM ina watu zaidi ya mil 10 wa uhakika hata ukiitisha uchaguzi wenye tume iliyoundwa na huyo Mbo we hamuwezi kutoboa bila watu kujiandikisha .

Wewe unaowaita watanzania ni wapumbavu na wajinga kwa sababu ya kukosa mikakati wewe mwenyewe.

Umesadia nini na hizo akili zako unaeoona ziko juu kuliko za watanzania wengine .
Hi unafikiri kuna watu wanawaza hayo mavyama ya siasa kwenye Nchi hizi za Afrika . Kila nchi vijana hawapendi hizi siasa za midomoni .
 
Uko sawa kusema wahariri wako na upande, wameshawishiwa huko. Na sisi hilo tunajua. Pia uko sawa kusema Lisu alitakiwa awashawishi .
Sisi uraiani tunawaona kama kondom tu zinazotumika na kuwa dumped baadae. Kizazi kinachonunulika kwa vipande vya fedha ni tatizo. Na ukweli ndio huu, wasanii, wanahabari aina hizi sio kizazi cha kukitegemea. Kama mwanahabari yuko na upande wake kila habari anayoileta itakuwa imepikwa na ni uselesss news. Sishabikii upinzani na nawaina hawajajipanga lkn sio muumini wa Uchawa na walamba miguu, hii nchi inahitaji maendeleo kwa kizazi kingine inahitaji viongozi na sio comedian na wezi wa rasilimali. Kinachoendelea katika vyama ni uchumia tumbo tu
 

Unashindwaje kama hujawandaa wanachama wako kusomeka kwenye Daftari la wapiga kura .

Kwa mfano 2026 Ikaundwa katiba mpya halafu madiwani na wabunge wa CCM wakafa wengi Kuelekea 2030 unaingiaje kwenye uchaguzi wa kupata hizo nafasi wakati huna wapiga kura ?
 
Good analysis, terribly pathetic finishing.
 

"Tanzania ni Nchi Moja na ni Jamhuri ya Muungano "
Hivyo ndivyo Katiba yetu inavyoanza .
Wewe hilo la Tanzania ni Nchi mbili umelitoa wapi?
 
Rubbish, wewe unaongea kama mjinga flan hivi,sorry to say so. unashabikia ujinga. CDM is right na ikiwezekana wasishiriki uchaguzi kabla ya Reforms. Wakifanya hivyo na wao watakuwa ni Wajinga kama wewe.
Sidhani kama umeongea kwa kuangalia madhila yanayotokea kwenye Chaguzi za nchi yetu. yanayo sababishwa na vyombo vya uchaguzi, sidhani kama uliona madhara ya uchaguzi wa 2020 jinsi maelfu ya wanachama na wagombea wa upinzani walivyoteswa bila sababu na wengine wapo ndani mpaka sasa. Tanzania kwasasa hakuna uchaguzi kuna uteuzi Wa wawabunge kwahiyo upige kura usipige wabunge na madiwani wata patikana tu, kura yako siyo inayo mchagua yoyote bali wanao amua nani apite nani asipite na kwa kura ngapi ni hao walioshika mamlaka, mimi sitajisumbua kupiga kura mwaka huu kwasabu nipige au nisipige kura yangu haina maana yoyote. Najua tu kwa vyovyote CCM itapita kwa asilimia 105 ya nini kwenda kujisumbua
 
WASOMI NDIO WANAOTUANGUSHA. Uchawa mwingi mpaka kwa wahariri. Ukiangalia ile video ni dhahiri kuna watu walikuwa wanatetea kundi fulani dhidi ya maslahi ya taifa. Wakati lisu anatetea mstakabali wa taifa wao wanatetea mtu fulani.
Ili mjue watu wameuchoka mfumo wa uchaguzi uliopo angalia idadi ya watu wanaoenda kupiga kura. Wananchi wengi huwa wanasusia uchaguzi maana ni kupoteza muda na pesa zinatumika bure wakati viongozi wameshajulikana nani atakuwa nani.

Na mwaka huu mfumo usipobadilika tutashuhudia idad ndogo sana ya wapiga kura maana watu wamechoshwa na mfumo huu nadhan mumejionea yaliyotokea uchaguzi wa serikali za mitaa. Kuanzia uandikishaji mpaka uchaguzi ni aibu tupu.

MABADILIKO NI HITAJI LA TAIFA KWA MSTAKABALI WA TAIFA
 
Kwahiyo wahariri ni wendawazimu??

Naomba anayejua kutag anisaidie kuwatagi tukianza na Pascal Njaa
Halafu japo sikuwahi kumwelewa Pascal Mayalla , ila nilikuwa najiambia huenda ana kitu ambacho wengine wanaona mimi sioni.

Sasa kwenye hilo la hicho kikao na Lissu nilimsikiliza, mwamba hamna kitu mule.
Ogopa mtu anajiongelesha ilimradi.

Yaani jamaa amejikomba kwa muda mrefu kwa watawala na ameambulia holla, he deserves hollah kwa kweli.
 
Umeongea

Umeongea vizuri sana je CDM iliandaa bahasha zozote kwa ajili ya hao wahariri. Kama ujuavyo vyombo vyetu vya habari ni njaa tupu issue kubwa kama hii inatakiwa pia na mbinu za ushawishi kwa baadhi ya watu. Hasa huyo Balele.
Usimchukulie poa mtu. Huyo Balile unayemuongelea vibaya sio mwenzio kimaisha. Kwanza ni professional , na pia ni mtu wa dini
 
Usimchukulie poa mtu. Huyo Balile unayemuongelea vibaya sio mwenzio kimaisha. Kwanza ni professional , na pia ni mtu wa dini
Kwani mmi nimemchulia,, na poa, Kwani Balele mimi nimesema Anakosa lolote mimi nimewaambia CDM wafanye kama wanavyo fanya wenzao wote wakiwaita waandishi wa habari wakitaka habari zao ziandikwe vizuri. Wawe na uhusiano mzuri na waandishi wa habari badala ya kuwafokea. Wawachukulie kuwa ni muhimili kamili wa nchi japokuwa hua wanaonekana kuwa watu wa kawaida. Ila wakiwachukulia poa watakuwa wanalalamika kila siku kuwa habari zao zinaandikwa zile mbaya tu nzuri haziandikwi. Ushawishi na mahusiano mazuri ndiyo yataweza kupata nafasi kwen,, nye vyombo vya habari vya nchi hii.
 
Kwani mmi nimemchulia,, na poa, Kwani Balele mimi nimesema Anakosa lolote
Umeandika mwenyewe hivi:
"Kama ujuavyo vyombo vyetu vya habari ni njaa tupu issue kubwa kama hii inatakiwa pia na mbinu za ushawishi kwa baadhi ya watu. Hasa huyo Balele."
 
 
Umeandika mwenyewe hivi:
"Kama ujuavyo vyombo vyetu vya habari ni njaa tupu issue kubwa kama hii inatakiwa pia na mbinu za ushawishi kwa baadhi ya watu. Hasa huyo Balele."
Kwani niongo kwenye kikao kimoja niliwahi kuona waandishi wa chombo fulani wakigombania posho zilizotolewa na mdau aliye waita kila chombo kilitakiwa kiwe na muakilishi mmoja chombo hicho kikawa na wawakilishi wawili wote wanataka wapatiwe takrima.
 
Unakubali kuwa kukiondoa chama tawala ni kazi ngumu kwani chama tawala kinatumia nguvu kubwa ya dola, lakini mwishoni unatumbukia kwenye ujinga wa kusema Samia 5 tena! Akili za watanzania ndivyo zilivyo mbovu ndio maana CCM inasitawi sana.
Kwa akili zetu wananchi zilivyo, kuna uwezekano CCM huwa haiibi kura aisee
 
Kwani niongo kwenye kikao kimoja niliwahi kuona waandishi wa chombo fulani wakigombania posho zilizotolewa na mdau aliye waita kila chombo kilitakiwa kiwe na muakilishi mmoja chombo hicho kikawa na wawakilishi wawili wote wanataka wapatiwe takrima.
Sasa ulitaka kukataa nini kuwa umemchukulia poa Balile kuwa ni miongoni mwa waandishi wa kulegezwa na posho?
 
Kwa mfumo wa sasa siyo Daftari la Wapiga Kura wala Sanduku la Kura vinatumika kupata washindi wa uchaguzi.

Kigezo ni WiZI, kuingiza kura bandia, kutangaza matokeo ya uongo, nk.

Wapiga kura wapo ila kwa sasa siyo wajinga, hawaendi kujiandikisha kwa kuwa wanafahamu hata wakipiga kura idadi ya kura zao haizingatiwi, haina tija.
Mifumo ikibadilika watajiandikisha tu..


View: https://youtube.com/shorts/4kAdyEwuvD8?si=JLB0VBzgBqwmbI9z
 
🌤️🙋‍♂️✍️🎯👏👌👍👊🤝🙏💐🎖️🆒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…