Pre GE2025 Hivi ndio tuseme Wahariri wanaamini Tanzania hakuna ‘Electoral fraud’?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Hao tayari wako compromised. .... Toka wakati wa Bandari.... huyo Kikeke na Crown media yake ni mali ya MWENYE KIFUA KIPANA. So you should know who is behind it.
 
"Mfano mzuri ni kilichotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu chamani". Tueleze kasoro zilizotokea kwenye huo uchaguzi ili tuweze kufananisha.
 
"Tanzania ni Nchi Moja na ni Jamhuri ya Muungano "
Hivyo ndivyo Katiba yetu inavyoanza .
Wewe hilo la Tanzania ni Nchi mbili umelitoa wapi?
Unajuwa maana ya United republic of Tanzania au unajitoa ufahamu. Nakupa mifaano ya nchi zaidi ya moja kuungana. United Kingdom, United states of America, United arab emirates zingine endeleza wewe......
 
Dar miundombinu ni mizuri sana, je, mbunge wako amewahi kukufikia?
 
Unajuwa maana ya United republic of Tanzania au unajitoa ufahamu. Nakupa mifaano ya nchi zaidi ya moja kuungana. United Kingdom, United states of America, United arab emirates zingine endeleza wewe......
Tanzania tuna rais mmoja na bunge moja, achana na hilo la wawakilishi ambao hawatungi sheria za nchi.
 
Kuna baadhi yao hawaoni uzito wa yanayosemwa na akina Lissu juu ya demokrasia Tanzania kiasi kwamba mhariri mzima anauliza aliko Mbowe.
 
Yote kwa yote, chama chochote cha upinzani kijifunze kwamba kutwaa madaraka, hususan kukiondoa chama tawala, siyo lelemama wala zoezi la usiku mmoja - it's a serious, constant business.
Ni rahisi tu wakibeba mitutu au kutumia ugaidi wanakitoa asubuhi tu. Issue hapa ni namna ya kukitoa kidemokrasia, hao wakiruhusu katiba iheshimiwe mbona wanaondoka asubuhi tu. Si walisema kumuangusha Mbowe haiwezekani lakini uchaguzi ulipokua huru na haki aliondoka mapema kabisa.

Same to Samia, uchaguzi ukiwa huru na haki anaondoka wala haihitaji constant business sijui mapambano ni haki kuheshimiwa tu.
 

## "...nimewaambia CDM wafanye kama wanavyo fanya wenzao wote wakiwaita waandishi wa habari wakitaka habari zao ziandikwe vizuri. Wawe na uhusiano mzuri na waandishi wa habari badala ya kuwafokea..."

• Hiyo👆👆👆statement yako una maanisha nini bro?

• Kuwa na uhusiano mzuri na waandishi ni kwa kuwafanyeje?

• Na ile juzi pale wewe uliona atmosphere ya uhusiano mbaya kwani kati ya CHADEMA na waandishi wa habari?

• Unaweza ku - describe huo uhusiano mbaya ukoje au ulikuwa vipi?

• "Hao wengine" (japo hujawataja lakini tunajua una maanisha CCM/serikali) uhusiano wao mzuri na waandishi wa habari ukoje?

• Kila mkiitwa kwenye PC zao mnapewa bahasha za khaki zenye posho/hongo ndani yake ili mkaandike/mtangaze vizuri uongo na utumbo wao, au siyo.?

• Sasa aina hiyo ya journalism ya mpaka uhongwe hela Ili uandike/utangaze habari itakuwa journalism kwa ajili ya kuilisha jamii ukweli au mtakuwa wanahabari mawakala wa shetani mnaotumiwa na viongozi wabaya wa CCM kuiharibu jamii kwa kuilisha uchafu na uongo wao..?

• Dhana na mantiki ya pendekezo lako hapa ni kuitaka CHADEMA nao wawe wanagawa bahasha za khaki/hongo kwa waandishi wa habari zao, au siyo..?

• Hivi waandishi wa habari waliozoea kuhongwa Ili watangaze au waandike habari zile anazotaka aliowahonga ambazo mara zote ni uchafu na uongo kwa jamii, wanawezaje kuhongwa tena Ili waandike ukweli...?

## BY THE WAY: Ile juzi, Tundu Lissu na CHADEMA hawakuwa wanawafokea hao waandishi wa habari. Bali, Tundu Lissu specific alimkemea na kumuonya Deodatus Balile kuacha ujinga (nonsense thoughts and questions) badala yake ajikite kwenye uelewa na ufahamu juu ya katiba ya JMT ya 1977 pamoja na sheria mbalimbali zinazosimamia chaguzi za Tanzania. Alikuwa anasisitizwa kwa ukali aache upotoshaji. That's all...
 
Wanajua sana kuwa ipo lakini teuzi zinawabana.
 
Hoja kuu ni bunge, wao kila jimbo (state) linatunga sheria zake ambazo haziingiliwi na jamuhuri.
Nenda kasome kidogo vizuri state wana vikao vyao vinaongozwa na Mayor huku kwetu kama madiwani na kuna congress hawa wantunga sheria za nchi kupitia Federal Goverment. Hapa Zanzibar wana baraza lao la wawakilishi pia wanasheria zao watunga za ndani ila kuna bunge la jamhuri wana deal na mambo ya Tanzania. Zanzibar wana mambo yao wanajiamulia hata kodi zao wanajipangia ndio maana bidhaa ya Zanzibar inapigwa tax tena huku na mambo mengine.
 
Tanzania hakuna wahariri kuna vibaraka wa chama tawala, na watawala ndio wana hariri kila kitu, wao wanaongozwa nini kiandikwe nini kitoke, lini na kwanini.
 
Wanapigania matumbo yao
Wakivizia teuzi

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…