Hivi ndivyo Jimmy Carter alivyobaki. Ndiyo tujue sasa dunia haina urafiki

Hivi ndivyo Jimmy Carter alivyobaki. Ndiyo tujue sasa dunia haina urafiki

Jimmy Carter ni rais wa Marekani wa 39 ambaye mnamo oktoba 1 mwaka 2023 alikuwa akisherehekea miaka yake 99 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1924.

Rais huyo mstaafu alitwala Marekani kuanzia mwka 1977 mpaka 1981.

Miongoni mwa mafanikio ya utawala wake ilikuwa ni kufanikisha kutiiana saini ya kurejesha uhusiano kati ya Israe na Misri mnamo mwaka 1979.

Kwa sasa Raisi huyo amepelekwa kwenye nyumba zenye huduma za afya za kuhudumia wazee baada ya kupata maradhi ya saratani isiyotibika tena.

Katika umri huo Jimmy Carter ndiye raisi aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi na aliyebaki hai muda mrefu zaidi baada ya kuondoka madarakani.

Muhimu kwa binadamu wengine ni kujifunza kwamba katika maisha inafika muda heshima zote zinaondoka na hata marafiki binafsi, urasimu wa kimadaraka vinaisha na kuonekana mzigo na familia na kutokuwa na umuhimu wowote wa kutafutwa ushauri kutoka ofisi uliyoihudumia.

Inafika wakati vyakula vyote vizuri unavimiliki lakini hata ukivitumia havibadilishi afya ya mwili.

Dawa zozote za kutibu za hali ya juu haziwezi tena kutibu maradhi yanayokupata.

View attachment 2977746View attachment 2977693View attachment 2977691
Kazeeka na alifiwa na mkewe.Ila nae hana siku nyingi atamrudia Muumba.Ila Mungu kampa upendeleo kuishi mpaka uzee huu.
Halafu mleta maada hakuna cha ajabu ,hii ndo nature ya maisha kwa waliojaliwa kuishi muda mrefu.
 
Nionavyo mimi wewe ndio una shida ya kuwaza.
Unamuona mzee kama huyo aliyewahi kuwa raisi wa taifa kubwa halafu unasema kila kitu ni kawaida tu.Huchukui funzo hata moja.
Toa hoja acha bla blah!

Wadau wengi wanakuuliza point yako ni nini hasa?

Unadhani kila mtu anawaza kama unavyowaza kwenye bichwa lako?

Wewe mbona babu yako alipozeeka na kuugua mbona hukuja kuanzisha uzi?

Unataka nini hasa?
 
A point of correction. Jimmy carter yupo kwenye hospice care, nyumbani kwake.

Yeye na mkewe waliamua wasitunzwe tena na familia zao, sasa Atafiki daktari maalum au muuguzi kuwatunza wao.

Kwasasa ana terminal disease. Any time annaweza kututoka, kwa maono yake yeye.

Yupo kwake na mkewe ila anatunzwa na wauzui hajaenda kwenye nyumba ya wazee. Ila tu anahitaji muda wake, na Mungu na Matibabu ya kawaida. He is at the end.

Ila pia huyu bwana bado alikua anatumika na serikali hasa bunge na. Ushauri mbali mbali.

Alionekana hata mwaka jana kabla hajafika 99, kwenye vikao mbalimbali.
Mkewe alifariki mwaka jana kama sikosei.
 
Jaribu kukaa chini na ufikiri vyema.Utajua tu.
Ukishindwa tafuta wakubwa zako watakuzindua.
Acha ubishi, jibu swali, point yako ni ipi hapo?
Kama haukuwa tayari kwa mjadala usingefungua uzi.
Yaani uzi ufungue wewe halafu maswali tuwaulize wengine?
 
Mkuu kibaiolojia watu wote tupo sawa, wote tunakunya, wote tunaumwa, wote tuna hisia, wote tutakufa..... so what’s a big deal kama tajiri atajamba au atacheka au ataumwa au atakufa?

Masikini wana mentality ya kuwaona “matajiri” wanajifanya ni watu special sana, na ndio maana wakifa wanaanza kusema yako wapi sasa kafa kama tunavyokufa sisi

Huwezi kukuta tajiri ana mentality kama hizi masikini akifa
Kwa bahati mbaya maskini anaangalia walio juu yake i.e Matajiri lakini matajiri hawana muda kuangalia walio chini yao i.e maskini. Kwakuwa maskini wanatazama juu na kuwaona matajiri ndo mana wanawazungumzia. Otherwise nakubaliana na ww kuwa hizo ni mentality za maskini.
 
Toa hoja acha bla blah!

Wadau wengi wanakuuliza point yako ni nini hasa?

Unadhani kila mtu anawaza kama unavyowaza kwenye bichwa lako?

Wewe mbona babu yako alipozeeka na kuugua mbona hukuja kuanzisha uzi?

Unataka nini hasa?
🤣🤣🤣 wengi hatujamwelewa huyo jamaa!
 
nisaidie kuwaza basi we juha. nyie ndo tajri akifa mnaweka vikao, et alikuwa anaangaikia nn sasa mbona kila kitu kaacha wanafaid wengine.
Jamaa ana mentality za kimasikini sana huyo! Kwahiyo watu wasitafute mali kwamba watakufa.
Hajui kwamba mtu anaweza kuwa masikini na Pepo aisiione vile vile! Sisi wote ni wa Mungu inategemea na mtu anaegemea wapi!
 
Sasa wakati huo ukifika 99 years si poa tu!

Shida ni kufa below 60!
Hakuna 99 wala below ya 60, maenyezi mungu katuumba kua na tamaa ya kuipenda dunia kuliko akhera ingawa kwenye vitabu vya dini tunaambiwa akhera ni bora zaid kuliko dunia lakin hakuna anapataka. Kwahiyo ipo hivi kila umli unaofika unaona ulipotoka si parefu yani unaona umezaliwa juzi tu hata ukifika hiyo miaka 60 au 70 bado hautaridhika na kuona u ekaa sana bado utaona juz tu huku madogo wakikuona ww umeifaid dunia huku wakitaman kufika umri wako na wakati huo wewe unaona mambo yako kibao hujayakamilisha kwqhiyo ndio ipo hivyo usishangae kuona huyo mwamba bado nae anataman sana kuish nae anamambo yake
 
Miili mliyopewa ni kwa ajili ya matumizi ya duniani, sasa unaanzaje kuipenda ahera usiyoijua kwa kutumia mwili ulioumbwa kwa matumizi ya duniani?
Subiri uwe na mwili wa ahera ndiyo uanze kuishi kiahera
 
Kwa bahati mbaya maskini anaangalia walio juu yake i.e Matajiri lakini matajiri hawana muda kuangalia walio chini yao i.e maskini. Kwakuwa maskini wanatazama juu na kuwaona matajiri ndo mana wanawazungumzia. Otherwise nakubaliana na ww kuwa hizo ni mentality za maskini.
huyu juha kama ana watoto, watakuwa wanasali kila siku wakiomba afe tu.
 
Miili mliyopewa ni kwa ajili ya matumizi ya duniani, sasa unaanzaje kuipenda ahera usiyoijua kwa kutumia mwili ulioumbwa kwa matumizi ya duniani?
Subiri uwe na mwili wa ahera ndiyo uanze kuishi kiahera
au anywe sumu afe awai akhera atuachie dunia yetu na maisha yaliyojaa ubatili na kujilisha upepo.
 
Back
Top Bottom