Hivi Ndivyo Nilivyofanikiwa Kumuacha Aliyekuwa Mke Wangu

Mlifanya jambo jema kukubaliana kumaliza migogoro yenu ndani, nawaombea Mungu hata mkija kuoana muwe mnamaliza migogoro yenu ndani...!

Siku mkiona mnaanza kupeleka Migogoro yenu nje, Kwa Wachungaji, Wazazi ama Marafiki ukumbuke hii kauli yangu Kwamba (Mtakua mmekaribia kiachana)
 
Mkuu,mwanaume anayejielewa hawezi kuvumilia dharau kutoka kwa mkewe,
Ukiona Panya anakuchezea ujue shimo lake lipo karibu.
Hakuna Mwanaume anayependa Dharau, ila umesikia upande mmoja tu umetoa hukumu, Binadamu ana tabia ya kuvutia kwake hasa kama akijua Mshindani wake hayupo...!

Mambo ambayo mtoa mada kaeleza ni tabia ambazo Wanawake wengi wanazo....
Sasa mtoa mada naye anayo Mapungufu yake, lakini yeye hajasema, yeye ametoa ya mwenziye na yeye akiwa Mtakatifu flani, ila kupitia maelezo yake mwenyewe tunaweza kuona pia sehemu ya Upande wake japo alijaribu kuficha, tunajuaje!? Ni pale Mke wake anapomwambia "Tatizo Lenu nyinyi Masai......!" Hii kauli Huwa inakuja baada ya mtoaji kuona Udhaifu flani Tena endelevu wa Upande wa pili, unaweza kuwa Udhaifu wa kawaida ama tabia Mbaya kabisa ambayo Masai wengi labda wako nayo, lakini kauli hiyo ni Moja ya Vitu ambavyo Masai aliamua kumuacha mkewe.

Unaweza kuona hata Masai ana Matatizo mengi tu japo msemaii hayupo, Mimi ni Msukuma na Mke wangu angeweza kuniambia jambo iwe Kwa hasira zake ama Utani kuhusu Kabila langu, haiwezi kuwa nyongeza ya sababu ambayo itafanya nimwache Mke wangu...!

Kwangu Mke wangu yupo Kwa kusudi na wote tunajua, kwamba tupo pamoja Kwa Kusudi, ukijua Hilo hutaanza kulalamika eti siku hizi Mme wangu haniambii ameni miss, ama haniulizi kama nimekula Mchana.
 
Hili ndo tatizo lenu nyie Wamasai, hamna siri.
 
Nilikua nasoma kwa makini huku nacheka, nilipofika hapo raia wa nchi jirani nikajua mwisho ulimuitia migration 😹😹

Ilitakiwa uwe serious masai siku nyingine umuitie migration wamchukue..!! 😹
 
Mbona hayo yote yalikua yanazungumzika?
 
Kuchati na ma Ex sio usaliti?
 
Chai
 
Tabia ambayo siwezi kuivumilia kwa mwanamke ni usaliti tu mengine yote yanavumilika
Mengine yote, Utavumilia na kuuwawa abaki na mali? Maana kuna wenye tamaa mpaka anaona roho yako ndo kizingiti.
 
Nafuu hujamuua
 
Umefanya maamuzi sahihi na kwa muda sahihi. Huyo hana sifa za kuwa mke, bali ni mtu aliezaliwa kutumiwa tu.

a. Alikuwa hana siri
b. Alikuwa mbinafsi
c. Ana kelele na lugha chafu
d. Anadharau kabila lako

Kuvumiliana kwenye ndoa kupo, lakini siyo kwa hayo mambo manne, maana hata watoto watakuwa wa hovyo.

Ushauri kwa wenye ndoa au wapenzi:

Kama hujajiandaa kisaikolojia kusalitiwa na mwenzako, usioe wala kuolewa—ishi single.

Hakuna mwanamke au mwanaume asiechepuka. Tofauti yake ni swala la muda, timing, au uwezo wa kutunza siri.

Wanandoa wengi huamini kisaikolojia kwamba wapo peke yao; hilo ni kosa kubwa. Haiko hivyo na haiwezi kuwa hivyo kamwe.

Ndio maana unapogundua mwenzako ana mtu mwingine, maamuzi magumu hufanyika hapa. Kama wanaume tunakosea, hebu tujijenge kisaikolojia kuepusha mengi.
 
Hakuna mwanamke au mwanaume asiechepuka. Tofauti yake ni swala la muda, timing, au uwezo wa kutunza siri.
Hii kauli itaponza wanawake bro. Kwa wanaume wengi, ukishajua mke ni Chawote mzuka unakata mazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…